Ccm yampiga stop thomas ngawaiya;aambiwa aache tamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm yampiga stop thomas ngawaiya;aambiwa aache tamaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Feb 22, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,019
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  ADAIWA KUFANYA KAMPENI ZA UBUNGE KABLA YA MUDA ULIOPANGWA


  Daniel Mjema,Moshi

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Moshi mjini kimempiga marufuku Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho mkoani Kilimanjaro,Thomas Ngawaiya kufanya kampeni za kuwania ubunge katika Jimbo la Moshi mjini.

  Kwa vipindi viwili mfululizo 2000-2005 na 2005-2010 jimbo hilo, limekuwa likishikiliwa na Philemon Ndesamburo (Chadema) imesababisha CCM kuumiza kichwa kutafuta mbinu za kumng’oa mbunge huyo, katika jimbo hilo.

  Hatua hiyo, imekuja wakati idadi ya wana-CCM wanaojaribu bahati yao ya kumn’goa Ndesamburo ikiongezeka baada ya mhasibu wa zamani wa ofisi ya spika, Gibson Lyamuya kutangaza kugombea ubunge katika jimbo hilo.

  Akitangaza nia yake kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Lyamuya alisema ameamua kujitosa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kuguswa na mateso wanayoyapata wafanyabiashara wadogo machinga.

  Lyamuya alisema kama atapitishwa na CCM, atafanya kila njia kupigania kufufuliwa kwa viwanda vilivyokufa au kufungwa na kutetea maslahi ya walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu wanapewa posho.

  Mhasibu huyo wa zamani wa ofisi ya Spika alistaafu kazi serikalini mwaka jana akiwa na wadhifa wa mhasibu mfawidhi wa Mkoa Kilimanjaro na sasa ni meneja wa kampuni binafsi ya Kinara Financial Services.

  Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa Ngawaiya, anadaiwa kufanya kampeni katika matawi ya kata za Pasa, Kaloleni na Miembeni.

  "Ili kuleta utulivu wa kisiasa katika wilaya yetu na kuepuka siasa za makundi nakukataza kufanya ziara zisizo rasmi ambazo hazijaratibiwa na uongozi wa CCM wilaya na Jumuiya ya Wazazi,"imesema sehemu ya barua hiyo.

  Barua hiyo ya Februari 8, ambayo ilitiwa saini na Allan Kingazi, pia ilimkataza Ngawaiya kuacha tabia ya kujinadi kwa kutumia mbinu yoyote iwe ya kidini, vikundi au Jumuiya za CCM.

  Barua hiyo, ilieleza kuwa baada ya Ngawaiya kutangaza nia yake, alipita katika kata hizo tatu na kuanza kujinadi kwamba tayari ameteuliwa na CCM kuwania ubunge.

  Barua hiyo inadai kuwa Ngawaiya alipoulizwa na viongozi wa matawi na kata kuhusu vitendo vyake hivyo, alijibu kwamba ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kilimanjaro, hivyo ana haki kufanya ziara.

  Ngawaiya alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na barua yake ambayo nakala yake imetumwa pia kwa katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alikiri kuandikiwa barua hiyo, lakini akakataa kata kata kuizungumzia.

  Kwa karibu wiki mbili sasa, Ngawaiya kupitia taasisi yake ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA), amekuwa akitoa misaada ya vitabu katika shule mbalimbali za Manispaa ya Moshi.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  maneno mbofumbofu.............acha mwenye uwezo aongoze na sio ccm wala chadema au chama kingine chochote chenye haki miliki ya jimbo hilo wananchi ndio wamiliki halisi..........tuanze kubadilika tusiendelee kupoteza muda kwa ajili ya hawa wachumia tumbo na wanaoingia kuichambua na kukuta mapungufu zaidi ya asilimia 70 lakini mwisho wa yote wanapitisha miswada kwa zaidi ya 100%
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...