CCM yamkana Shehe Yahya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamkana Shehe Yahya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Safari_ni_Safari, Sep 13, 2010.

 1. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Kampeni wa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema chama hicho na mgombea wake havihusiki na taarifa za kuongezewa nguvu za ulinzi usioonekana kama inavyoelezwa na Mnajimu Sheikh Yahya Hussein.

  Kinana alisema jana kwamba, Rais Kikwete ni muumini mzuri wa dini ya Kiislamu aliyelelewa katika misingi ya dini, anaamini afya njema au maradhi, vyote huletwa na Mwenyezi Mungu na vivyo hivyo katika suala la ulinzi wa afya ya mwanadamu.


  Alisema Sheikh Yahya ni Mnajimu, anao uhuru wa kusema vitu anavyoviona, lakini Rais

  Kikwete wala CCM visihusishwe na mambo hayo.

  Alisema mbali na ulinzi wa Mungu, Rais Kikwete ana kikosi madhubuti cha walinzi waliofundwa vyema kuhakikisha usalama wa Rais.


  Kauli ya Kinana imefuatia taarifa za baadhi ya vyombo vya habari kuwanukuu wanasiasa

  na kiongozi mmoja wa dini wakimtaka Rais Kikwete atoe tamko kuhusu madai ya Sheikh
  Yahya ya kumpatia ulinzi usioonekana.

  Sheikh Yahya alikaririwa akisema atatoa ulinzi usioonekana kwa macho ili kumkinga Rais Kikwete, ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu mwezi kesho.


  Hata hivyo, jana Sheikh Yahya alitoa ufafanuzi wake juu ya taarifa aliyoitoa awali akisema

  ilitafsiriwa vibaya na baadhi ya watu na kusisitiza kila mtu ana jini wake na kusema jini wa
  mgombea wa Chadema, Dk. Slaa anaitwa Subiyani.

  “Mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina nilikuwa

  nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na
  sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waislamu na Wakristu na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao,” alisema.

  Akifafanua zaidi, alisema hata Mfalme Solomon alikuwa na Jeshi la Majini na aliwatumia

  katika ujenzi na vita.

  “Kwa hiyo nawataka viongozi wa kidini na kisiasa wasihusishe mambo haya na uchawi haya ni mambo ya kawaida na yanafanyika ulimwenguni kote hata hao viongozi wa kidini nao

  wanawatumia majini katika kazi zao,” alisema.

  HABARI LEO
  Jumla Maoni (7)

  Maoni SHEIKH ASIJARIBU KUMSAFISHA KIKWETE WALA KINANA ASITUDANGANYE. HUU WOTE NI USHIRIKINA NA VITABU VYA KIKRISTO INAWAKATAA MAJINI HATUNA USHIRIKIANO NAO. CCM INAUHUSIANO NA WANAJIMU KWAKUA SHEIKH ALISHASEMA ATAKAEMPINGA KIKWETE ATAKUFA, NA BADO CCM HAMKUKANUSHA USEMI HUO BALI TAARIFA ILITOKA IKULU KUSEMA MANENO YA SHEIKH YAHESHIMIWE.
  SASA HIVI MMEONA KUA WATANZANIA TUMEWATILIA SHAKA KUBWA NDO MNAANZA KUTUTAJIA MAJINI. MBONA MNAMSEMA SLAA PEKE YAKE KUMPAKAZIA SUBIYANI NA WENGINEO HAMUWATAJII. SI KIINGINE NI KWAKUA MNAMUONA NI TISHIO.
  SHEIKH YAHAYA NA KIKWETE NI DAMUDAMU. Hatudanganyiki

  Maoni Mungu wa mbinguni atusamehe na asamehe nchi yetu Tanzania mapepo na majini ni walimuasi mungu sisi kama wanadamu Tulioubwa kwa mfano mungu wa mbinguni tukaishi maisha yanayo fanana nae tunakuwa na uwadui na mapepo na majini.na shetani ndipo mungu akatupa malaika ili atulinde malaika awakumuasi mungu kwaiyo razima ujue kuna maraika wa mungu na mapepo majini wa shetani

  Maoni Wapinzani wa Mh, J K, muache woga, km mmeisha jipanga kushindana mkubali kwa moyo mweupe, tukitegemea ushindani wa sera, nasi wananchi tutachuja PUMBA NA MCHELE wenyewe, Huu woga mnaoanza kuuonyesha, mwishowe mtagongwa na kuta mkiogopa kivuli chake. Km kawekewa majini ili yamlinde asidhulike, sasa anayelifuatilia alitaka yamlinde yeye?? au mmeambiwa baada ya hapo yatapiga kura siku ya uchaguzi?? Kwa kuwa uhuru upo, basi nalo lipeleke km Pingamizi, Hakuna mtanzania mwenye umri wa kupiga kura, atakayeburutwa siku hiyo ya 31 Octoba,kila mtu kwa maamuzi yake atamchagua anayeona anafaa.TUACHE TABIA YA KUTUKANANA KUSIKOJENGA,SISI WOTE NI WATZ,

  Maoni Ccm wakubali tu kuwa wamamtumia sheik ipasavyo kwanwote tunajua siasa nauchawi nikurwa nadoto.

  Maoni I am sorry, sheik yahya aende zake na majini yake asimhusishe Dr slaa na ulinzi wa majini hapa. Dr slaa analindwa na malaika na kama sheik yahya amepeleka huyo jini anayemwita subiyani kwa Dr slaa ili akamdhuru basi ajue hana mafanikio. Na hataweza kumzuia Slaa asiingie Ikulu. Huyu jamaa alisema atampa majini ya ulinzi kikwete, leo anamwingiza Dr Slaa ili iwe nini? Utukome Sheik yahya na majini yako.

  Maoni Huyo sheikh Yahaya asitake kumdhalilisha Rais Kikwete kuwa anatumia nguvu ya giza,Yeye anashida zake asijipendekeze kwa kumdhalilisha Rais ni aibu

  Maoni Huyu mzee yahaya huwa ana tabia ya kutafuta mamlaka kwenye jamii kwa nguvu. Wale watu wa makamo mnakumbuka jinsi alivyokuwa anatafuta mamlaka kupitia dini bila ridhaa ya waamini hapo miaka ya nyuma na kusababisha mifarakano kila wakatu kwa kuingilia taasisi halali za kiislamu. Baada ya kudhibitiwa sasa amehamia uganga kwa kujidai mnajimu huku anawatia watu hofu na kuwazidishia imani ya kishirikina. Sasa anajidai anamwekea kinga rais, yeye ni taasisi yoyote kisheria hadi atangaze kitu kama hicho? Angesema anamuombea kwa mungu usalama tungeelewa, lakini eti yeye atamuwekea ulinzi wa majini, hii ni kitu gani? Huyu mzee inafaa adhibitiwe maana hana tofauti na wale waganga wa kule mwanzana shinyanga wanaosababisha maauwaji ya watu kwa imani za kishirikina
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli kaingia hata kwa dr.slaa?.......
  Hata kinana akimkataa lakini kikwete na makamba wanaye na ni damudamu..........siku hizi tanzania uchawi njenje hakuna kujificha tena, siamini km sheikh yahaya hajahusika kuuwa albino wetu lazima takuwa amefanya hivi........hivi kwa nini hakamatwi kwa uchochezi huyu mpuuzi?
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,731
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni mshirikina, hilo halina ubishi na mwenyekiti wa jopo la waganga wake ni huyu Shekh Yahya, yeye mwenyewe katudhihirishia hivyo sasa ubishi wa nini, yeye mwenyewe kasema kaagiza majini yake yaongeze nguvu kwenye ulinzi wa huyo mgonjwa
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  sheikh yahaya na kiwkete wanapaswa kuombewa.........watubu watuache watz wasituvuruge......km kikwete hawezi kuongoza bila ushirikina wa hadharani kiasi hiki basi aache kampeni na kwa kweli uongozi wake umejaa mambo ya ajabu ni bora angeacha asaidiwe...........
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo, jana Sheikh Yahya alitoa ufafanuzi wake juu ya taarifa aliyoitoa awali akisema
  ilitafsiriwa vibaya na baadhi ya watu na kusisitiza kila mtu ana jini wake na kusema jini wa
  mgombea wa Chadema, Dk. Slaa anaitwa Subiyani.

  "Mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina nilikuwa
  nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na
  sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waislamu na Wakristu na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao," alisema.

  Akifafanua zaidi, alisema hata Mfalme Solomon alikuwa na Jeshi la Majini na aliwatumia
  katika ujenzi na vita.


  "Kwa hiyo nawataka viongozi wa kidini na kisiasa wasihusishe mambo haya na uchawi haya ni mambo ya kawaida na yanafanyika ulimwenguni kote hata hao viongozi wa kidini nao
  wanawatumia majini katika kazi zao
  ," alisema.

  Duh...ina maana hata Kadinali wetu anayo majini?.......Kakobe?....umeme umewaka?..........Mama Lwakatare?.....huyu Babu kiboko kweli
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tutasikia mengi mwaka huu
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  na Janet Josiah(Tanzania Daima)


  MTAALAMU wa Tiba za Asili, Dk. Sadiki Kalimauganga, amelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mnajimu wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Husein na kumpeleka katika vyombo vya sheria kwa kosa la kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete kuwa alianguka jukwaani kutokana na kuzidiwa nguvu za giza.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Kalimauganga ambaye alitaka kugombea ubunge katika Jimbo la Urambo Mashariki kupitia CCM na baadaye kuachia ngazi, alimtaka Sheikh Yahya kuacha kutangaza utabiri kwa Rais Kikwete, utabiri ambao alidai kuwa ni wa uongo.

  “Namwomba Sheikh Yahya aache kuwatabiria uongo viongozi na chama chetu, kwani katika uchaguzi wa mwaka 2005 alitabiri vitu vya ajabu sana, ambavyo hakuna hata kimoja kilichokuwa cha kweli,” alisema.

  Alisema ni jambo la ajabu kwa mtabiri huyo kuuambia umma kuwa Rais Kikwete alianguka jukwaani kutokana na kuzidiwa nguvu na majini waliotumiwa na wagombea wenzake wa urais wakati si kweli.

  Alibainisha kuwa ni udhalilishaji kutangaza hadharani kuwa rais atapatiwa ulinzi usioonekana (majini) katika kampeni zake ili kujikinga na watu wanaomfanyia ushirikina.

  Aliwataka wananchi wakumbuke utabiri wa mnajimu huyo alioutoa maka 2005 kwamba CCM isipomsimamisha mgombea urais wa kike itaanguka, alidai kuwa CCM ilishinda na yeye (Sheikh Yahya) kubadilisha kauli yake kuwa Rais Kikwete ana sura ya kike.

  Alisema kauli ya kumuita kiongozi wa nchi ana sura ya kike ni udhalilishaji ambao haupaswi kuvumiliwa na vyombo vya dola.

  Dk. Kalimauganga aliwataka wananchi kukumbuka kauli nyingine ya mnajimu huyo, mwanzoni mwa mwaka huu akiwa katika chombo cha habari (televisheni) kwamba timu ya Simba Sports Club, haitachukua ubingwa na baadaye ikatwaa ubingwa, hali iliyowafanya mashabiki kutaka kuchoma nyumba yake.

  Alisema kutokana na matukio hayo ambayo alidai kuwa yalikuwa na utabiri wa uongo, anaomba mnajimu huyo asipuuzwe na wananchi pamoja na Rais Kikwete anayeendelea na kampeni.

  Wakati huo huo, Sheikh Yahya amebainisha kuwa hakueleweka kwa wananchi alipotoa kauli ya kumpa ulinzi usioonekana Rais Kikwete.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya alisema kuwa alikuwa anazungumzia majini ambayo ni viumbe kama binadamu lakini wao wameumbwa kwa moto na binadamu wameumbwa kwa udongo.

  “Watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao,” alisema Sheikh Yahya.

  Alisema kuwa Mfalme Solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.

  Alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda Rais Kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.

  Aliongeza kuwa hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.

  Juzi katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.
   
 8. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Alisema mbali na ulinzi wa Mungu, Rais Kikwete ana kikosi madhubuti cha walinzi waliofundwa vyema kuhakikisha usalama wa Rais. [/COLOR]

  Hii inachekesha sana.
  Kudondoka mara zote hizo hicho kikosi kilikuwa wapi? Ni juavyo mimi hicho kikosi kinaweza kupambana na Binadamu na si majini.
  Ulinzi wa Yahaya ni wakimajini na si kama anavyozungumza huyu Kinana.

  Jambo lililopo kwa sasa ni kujua kwamba uchaguzi umefunikwa na nguvu za giza - Kichawi. Ni wakati wa wanamaombi kufunga na kuomba ili kuinusuru nchi kutawaliwa na viongozi wanaoongozwa nanguvu za kichawi.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  viongozi wa dini ipi? hayo ni mafundisho ya kiislamu na wala sio kila mtu anakubaliana na uchawi wa majini ya yahaya...........na sielewi kwa nini kaamua kumchafua hata dr.slaa, kikwete halali kwani imani yake inaruhusu majini na yahaya akisema hata viongozi wa dini wanatumia anadanganya ila aseme viongozi wa kliislamu wanayatumia.............
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Ndimara Tegambwage(Tanzania Daima)


  SITAKI kusikia na kuamini kuwa vyombo vya ulinzi nchini vimeshindwa kazi – Polisi, Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Usalama wa Taifa.

  Sitaki kuamini kuwa tayari walinzi wanakaa tu; lakini wanalipwa mishahara na marupurupu mengine – wanatumbukiza mifukoni na matumboni – bila kufanya kazi yoyote ya kumlinda “Rais wa Jamhuri ya Muungano.”

  Sitaki kuamini kuwa nadharia za kisasa za ulinzi, silaha za kisasa na uvumbuzi unaoendelea katika medani ya ulinzi, vinaweza kutupwa chini na badala yake akatafutwa mtu, watu au vikundi vya kumlinda rais.

  Sitaki kukubali wawepo watu binafsi, vikundi na kampuni za ulinzi; tena za kumlinda rais – na huenda na wananchi na mali zao – ambavyo havitambuliki kikatiba.

  Sitaki kuamini kuwa walinzi – waliosomea kazi hiyo na hata waliopendelewa kuwa katika nafasi hiyo muhimu – wanaweza kukubali “kuwekeana mikataba” na watu binafsi, makampuni na mataifa ili kulinda nchi yao.

  Sitaki kuamini pia kuwa walinzi – wataalamu wa zana na wenye maarifa makuu – wanaweza kujisalimisha kwa Sheikh Yahya Hussein ambaye anaona ulinzi wa rais na ikulu sharti uwe mikononi mwake.

  Sitaki kuamini kuwa rais wa Jamhuri ana taarifa kuwa walinzi wake hawatoshi kumlinda; hawawezi kumlinda na kwamba zana zao na maarifa yao vimeshindwa kumwekea usalama unaostahili.

  Sitaki kuamini kuwa rais anaamini kuwa hana ulinzi wa kutosha; kwamba majeshi yake yamechoka na kuchakaa na sasa sharti atake, apewe au atafutiwe ulinzi wa nyongeza nje ya silaha na maarifa yanayotambuliwa kitaifa na kikatiba.

  Sitaki kuambiwa kuwa rais anaweza kukubali kulindwa na vyombo vingine nje ya vile tunavyofahamu kitaifa na kikatiba. Atakuwa amedharau nchi yake, watu wake, majeshi yake na katiba ya nchi yake.

  Lakini mnajimu Sheikh Yahya Hussein anasema, bila woga wala aibu kuwa “sasa atamlinda Rais Jakaya Mrisho Kikwete” kwa ulinzi maalumu ambao hauonekani.

  Mnajimu huyo wa Magomeni, Dar es Salaam, alisambaza waraka katikati ya wiki hii akielezea jinsi Rais Kikwete alivyoandamwa na wabaya na kwamba kuishiwa nguvu uwanjani Jangwani tarehe 21 mwezi uliopita, kulitokana na uchawi.

  Haijafahamika iwapo Sheikh Yahya ndiye alitengua uchawi uliomwangusha Kikwete; ulikuwa uchawi wa kiwango gani; uliolenga nini na uliotoka kwa nani.

  Kwa kauli ya mnajimu, haikufahamika “amemwokoa” mara ngapi, amemkinga mara ngapi na anaaminika kwa kiwango gani kwa mkuu wa nchi.

  Mwaka jana alipotabiri kuwa atakayejitokeza kushindana na Kikwete, ndani ya chama chake, atakufa kifo cha ghafla, ndipo wengi walianza kumhusisha Yahya na wapangaji wa ofisi kuu ya nchi.

  Kwa nia njema na labda kwa kutambua kazi yake nzuri, msemaji wa ikulu alipoulizwa juu ya kauli ya Yahya, alisema kuna haja ya “kuheshimu kauli” ya kila mmoja. Lakini Jakaya Kikwete hakusikika akisema lolote.

  Haikufahamika iwapo kwa “kuheshimu kauli” msemaji wa ikulu alikuwa na maana ya kila mmoja kuwa na haki ya kutoa kauli au alikuwa anasisitiza umuhimu wa kutambua na kuzingatia utabiri wa Sheikh Yahya.

  Wakati huo, Sheikh Yahya hakusema iwapo amemwekea kinga Rais Kikwete. Hakusema kifo cha ghafla kitaletwa na nani na nini – nyota, mwezi, mizimu katika mzunguko wa kinga-nikukinge au ua-nikuue.

  Bali vyovyote iwavyo, kuibuka tena kwa mnajimu zikiwa zimebakia siku 51 kufanya Uchaguzi Mkuu, kumechukuliwa na wengi kuwa njia ya kuimarisha utabiri wake; kuongeza nguvu za “kinga” yake na hata kuonyesha “mteja wake” kuwa hajamtupa mkono; pamoja na yote yanayojitokeza.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Sheikh Yahya kusema analinda rais aliye ikulu. Uhusiano huu kati ya mtu binafsi na ofisi kuu hauwezi kuwa umejitokeza ghafla.

  Yawezekana pia uhusiano huu umekuwepo kati ya mganga huyu mwenye “ulinzi” (unaozidi ule wa maaskari na mashushushu) na marais waliotangulia; bali hapa hatuna uwezo wa kuwasemea.

  Swali la haraka ambalo kila mmoja anaweza kujiuliza ni: Mlinzi huyu wa majeshi yasiyoonekana, analipwa posho au mshahara? Analipwa kiasi gani?

  Nani anamlipa mlinzi huyu? Fedha hizo zinatoka kwenye kodi za wananchi au yule ambaye anajisikia amelindwa na kufanikisha matakwa na malengo yake?

  Nikiwa bungeni pale Dodoma, mwaka 1997, mbunge mmoja wa CCM aliyekuwa akifurahia hoja zangu, alinitambulisha kwa wageni kutoka jimboni mwake ambao pia walitambulishwa kwa wawakilishi bungeni.

  Alitambulisha wageni saba; wakiwa wanawake watatu na wanaume wanne. Alinieleza kuwa aliyemtambulisha mwishoni “ndiye mtu wangu muhimu” – mganga/mlinzi.

  Uganga na kinga ndani ya nyumba za watu binafsi. Uganga ndani ya ofisi za serikali. Uganga ndani ya Bunge. Uganga ndani ya ikulu – kwa kuombwa au kwa kujipendekeza. Uganga!

  Nimekumbuka ikulu ya Banjul, Gambia ambako tuliambiwa mapema mwaka jana kuwa Rais Sheikh Profesa Alhaj Dk. Yahya Abdul-Aziz Jemus Junkung Jammeh, naye ni mganga wa aina yake; pamoja na “kutibu ukimwi.”

  Katikati ya ulofa huu unaoitwa kinga, watoto wa kike wa hata umri wa miaka 12, wanabakwa na Wazungu – katika mahoteli na mabaa yaliyotapakaa mjini Banjul; kufanywa wajawazito na kutupwa mitaani wakilia na kusaga meno. Umaskini wa kutaga mayai!

  Imani za “kukinga” zimedumaza akili; zimekwamisha uwezo wa kufikiri; zimezamisha matumaini ya wengi huku zikifanya watawala washughulikie kitu kimoja tu: kujikinga.

  Bila shaka hapa Sheikh Yahya alikuwa anajitangaza ili wagombea nafasi mbalimbali wapate kumkumbuka na kumwendea, hasa wakizingatia kuwa ndiye mtoa kinga kwa rais badala ya vyombo vya dola.

  Wale askari wasioonekana; zile silaha zisizoonekana; ule utaalamu usiosomewa vyuoni wala kufundishwa majumbani; ni mashetani ambayo mnajimu anataka yamlinde Kikwete.

  Tunasubiri mgombea urais wa CCM kukubali kwa faragha au hadharani kupata ulinzi huo; jambo ambalo litakuwa na maana moja tu: kwamba amefukuza kazi majeshi yote nchini na kuajiri mashetani.

  Haitakuwa ajabu kuona hata walinzi wake kwenye msafara wake wa sasa wakiondolewa na yeye kubaki na wapiga debe wa umoja wa vijana wa chama chake. Tunasubiri.
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  Km kikwete anajua anaulinzi wa namna hii kwa nini kuendelea kuwaumiza watz kwa kuwalipa watu mihela kibao ambao hawafanyi kazi yoyote......kumbe yahaya ndiyo mlionzi wake?........tafadhari wasitup[otezee muda wetu huu muhimu ktk ujenzi wa taifa na kuamua mustakabali wa taifa letu.....................
  Kwanini basi kikwete kuangukaanguka wkt anaulinzi madhubuti...........
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,474
  Trophy Points: 280
  Huu ndio mwaka wa yahaya jamani tusisahau 2005...ni mwaka wake wa publicity......ubaya ni kwamba anadhania hadhira ya 2005 ndio hii hii

  by the way, ilikuwaje akaenda kutibiwa India kama ana uwezo na elimu ya kutumia majini? si yangemponya in the first place?
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Itakuwa wote waliugua...yeye na hayo majini yake....ni nani alilipa hiyo medical bill yao?
   
 14. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  Watu wa namna hii siamini km wanastahili kuwepo hapa tz....
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,474
  Trophy Points: 280
  hahaha...mkuu in case umesahau,hiyo alilipiwa na JK na hata alivyorudi alimshukuru kwa kulipia hiyo bili....well anayo haki na JK anayo haki kumsaidia, lakini hili la kuwa na 'nguvu za ziada' kama hizi kisha anaugua ndio hapo napiga hesabu zinakataa

  isitoshe, tunaamini kinga ni bora kuliko tiba, kwa nini HAKUZUIA kuanguka kwake in the first place, kuliko kusubiri tukio litokee ndo aje kupayuka kwenye vyombo vya habari? au na yeye alizidiwa? manake avumaye baharini papa..kumbe nyangumi pia wapo
   
 16. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hivi jini wa JK anaitwa nani vile. Huyu ni mlegevu sana, inabidi wambadilishe maana anamdharilisha sana rais wetu kwa kumwacha aanguke hadharani. Sheikh Yahya nafikiri Wadanganyika tuna haki ya kumjua jini anayemlinda Rais wetu!!!
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Anaitwa Kashkash mwana wa Dimdim:lol::lol:
   
 18. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  hahahah! hivi TandaleOne yuko wapi toa maoni yako kuhusu hili! wela welaaa CCM na Majini damu Damu! TandaleOne hivi jini wa Salma Kikwete anaitwa nani vile?
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Sura Al-Jinn (Arabic: سورة الجن‎) (The Jinn) is the 72nd sura of the Qur'an with 28 ayat. The name as well as the topic of this chapter is jinn. Similar to angels, the Jinn are considered to be spiritual beings naked to the human eye. The habitat of angels is considered to be the sky, whereas it is the earth for Jinn. In the Quran, it is stated that humans are created from the earth and jinn from fire in more than one instance and it is also evident from the hadeeth that the angels were created from light.

  In the second ayat the jinn recant their belief in false gods and venerate Muhammad for his monotheism. The jinn apologize for their past blasphemy and criticize mankind for either neglecting them or encouraging their disbelief. Ayats 20-22 are especially important as Tawheed among the Jinn is reaffirmed and the inescapable wrath of Allah is emphasized. The Judgement in ayat 7, and the Punishment in ayat 25, are both references to the Islamic Judgement Day, Yaum al Qiyamah. Ayat 25-28 establish that Qiyamah is known only to Allah and that Allah takes into account all the deeds of a man when judging him.

  "I know not whether the (Punishment) which we are promised is near, or whether my Lord will appoint for it a distant term."
   
Loading...