CCM yamgeuka Lowassa

kwa kweli something is wrong somewhere.ila sishangai sana coz nahisi makamba upeo wake ni mdogo zaidi na ndio chanzo kikubwa cha ukandamizaji wa demokrasia hapa Tz kwa sasa.mzee yule huwa ni nguvu kwanza akili baadae
 
Wote Makamba na Lowassa wanatafuta cheap popularity. Mbona naye Makamba amemzungumzia Lowassa kupitia magazetini? (Kulingana na hiyo taarifa hapo juu). CCM has already fallen apart.
 
Makamba ana akili sana, sema anazitumia tofauti na sisi tunavyowaza. Si ana nywele?

Mbona Lowasa anasifiwa hapa...who knows why he is like that today and may be not like that tomorrow?
 
kwa kweli something is wrong somewhere.ila sishangai sana coz nahisi makamba upeo wake ni mdogo zaidi na ndio chanzo kikubwa cha ukandamizaji wa demokrasia hapa Tz kwa sasa.mzee yule huwa ni nguvu kwanza akili baadae


Hiyo ni kanuni ya Jeshi la Mkoloni
 
Hivi kule Jeshini Makamba alikuwa Kikosi gani. Inawezekana tnshangaa kumbe alikuwa kikosi cha Ngonjera
 
Du! kweli dunia kigeugeu. Leo Lowassa anaonekana shujaa na kupongezwa hapa jamvini! Ama kweli!

Give the devil his due. Ingekuwa kazi ya wachangiaji hapa ni kuangalia mtu na kutoa kasoro tu basi lingekuwa jamvi la wapuuzi. Hata JK akitoa point inachambuliwa na kupewa heshima yake. Huo ndio u-Great Thinker! Pamoja na kero zetu zote kuhusu Lowassa, kauli aliyoitoa huko Arusha ina hadhi ya kiongozi (that's leadership) sio wale wanaofikiri ufumbuzi ni kutumia FFU tu.
 
Drifter

Naungana na wewe kwa asilimia 100. Tunatazamia great thinkers kuchambua hoja kwa uzito wake, sio nani kasema.

Ukiangalia kauli hizo mbili, bila kujali nani kasema na anajikomba kwa nani, ni dhahiri kwamba mtoa maoni wa kwanza EL alikuwa sahihi. Mji wa Arusha si wa madiwani na wanachama wa CCM na CHADEMA. Kuanzisha vurugu kwa sababu za kipuuzi na za kibinafsi hakumsaidii yeyote, zaidi ya kutuudhi sisi wapiga kura na kuacha kujitokeza kwenye chaguzi zijazo! Hatukuwachagua wakapiganie umeya, bali kuleta maendeleo.

kama yapo mapungufu kwenye kanuni, ni wajibu wao wote kurudi nyuma na kufanya marekebisho, badala ya kutuletea ujinga wao. Kura tuwapigie, halafu wasababishe maji ya kuwaswa mitaani!
 
Vurugu zikianzia Arusha hazitaisha.
EL anajua anachokisema. Kumbukeni vita vya kidini KKKT kwa jimbo la Meru. Na mwisho walijitenga.
CCM inataka ya Rwanda yatokee?
 
Ni kiongozi makini, hakurupuki, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na anazijua sana taratibu za Chama.

Hawezi kukikemea Chama chake kupitia magazetini. "Anapo mahali pa kukikosoa kama kimekosea. Ni katika vikao. Nadhani amenukuliwa vibaya."

Hivi hii ngonjera ya CCM ya kusema wana utaratibu wao na issue lazima ziwasilishwe kwenye vikao wana maana gani??? Kwani vikao vipo kila siku?? Huyu jamaa anataka mpaka moto uwake Arusha ndiyo ajuwe kuna matatizo?? Lowasa anazungumza vile kwa kuwa ana uchungu na Mkoa wake sasa yeye Makamba uchungu wake ni madaraka tu. Hivi ingekuwa Tanga angesemaje??

Sitta amesema wamesemema wana utaratibu wao, EL kasema anasema wana utaratibu wao. Sasa mbona haitishi hivyo vikao sasa iliwajadili. Na kwa nini yeye anawakosoa wenzake kwenye media badala ya kusubiri hivyo vikao??
 
Hivi ulishaona wapi mtu usiokuwa na matunda ukapigwa MAWE?
Wana JF, kilichopo Arusha ni hiki: CCM imeshinda Kata 10, CHADEMA Kata 8 na TLP Kata 1. Katika mgawo wa viti maalumu CCM ikapata viti 3, CHADEMA 3 na TLP 1. Na katika Ubunge CCM ina wabunge wa viti maalumu 2, CHADEMA inao 3.Piga hesabu hapo kutokana na mchezo huo ulivyo ndio maana CCM wakalazimika Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Mary Chatanda ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha apige kura Manispaa ya Arusha kumchagua Meya.
 
Hivi ulishaona wapi mtu usiokuwa na matunda ukapigwa MAWE?
Wana JF, kilichopo Arusha ni hiki: CCM imeshinda Kata 10, CHADEMA Kata 8 na TLP Kata 1. Katika mgawo wa viti maalumu CCM ikapata viti 3, CHADEMA 3 na TLP 1. Na katika Ubunge CCM ina wabunge wa viti maalumu 2, CHADEMA inao 3.Piga hesabu hapo kutokana na mchezo huo ulivyo ndio maana CCM wakalazimika Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Mary Chatanda ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha apige kura Manispaa ya Arusha kumchagua Meya.


Napendekeza katiba mpya kusiwe na VITI MAALUMU!!!
 
Mtachonga sana... Ila tu chadema haiwezi kuitumia Arusha kutafuta umaarufu! Mbaya zaidi kupitia huyo mhuni Lema!

chadema ni maarufu tayari, sasa sijui kwanini unasema haiwezi kuitumia arusha kupata umaarufu, ama pinga kwamba chadema siyo maarufu.
 
Huenda Lowasa ana machungu na Arusha yake na ameona mapema madhara ya hali iliyopo kwa mstakabali wa mji huo na ustawi wake tofauti na Makamba. Anyway, to wait and see!
Mh.Lowasa karibu CHADEMA tutakupa kile ambacho umekua ukikitamani siku zote achana na porojo za makamba na genge lake pale lumumba.
 
Back
Top Bottom