CCM yamgeuka Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamgeuka Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Dec 24, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MGOGORO wa kisiasa wa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, unaweza kuzaa mpasuko siyo tu kwa wakazi wa Arusha, bali hata kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba, kutofautiana na mmoja wa makada wake maarufu, Edward Lowassa.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Makamba akionesha kutofurahishwa na kauli
  ya Lowassa ya kutaka mgogoro huo wa umeya wa Arusha umalizwe kwa amani kwa kuzikutanisha pande zinazohusika, alisema taarifa ya Lowassa iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, imemshitua sana.

  Pamoja na kuzungumzia amani, Lowassa pia alisisitiza wahusika kuelimishana ili kuunusuru mji huo wa Arusha na Taifa kwa ujumla, usitumbukie katika ghasia.

  Lowassa alivitaka vyama hivyo kukaa meza moja kumaliza vurugu zilizotokana na uchaguzi wa
  kumpata meya wa jiji hilo ambapo iliripotiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisababisha vurugu na kukamatwa na polisi ambapo baadaye aliachiwa.

  Jana, baadhi ya magazeti yalimnukuu Lowassa akisema juzi katika mkutano mjini Arumeru kuwa, “leo nimekuta Mji wa Arusha ukiwa umezingirwa na askari Polisi na sehemu zingine kulikuwa na gari la maji ya kuwasha kwa ajili yakulinda usalama wa mji na watu wake.

  “Hali hii imetokana na uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, nawaomba viongozi wa vyama
  vinavyovutana, wakae haraka ili kuondoa hali hii ili Arusha isije kuwa kama Ivory Coast…Arusha ni yetu sote.” Alisema.

  Hata hivyo Makamba kutokana na taarifa za vyombo vya habari alisema:“Nimeshitushwa sana na taarifa hiyo, nimeshituka kwa vile namjua vizuri Mheshimiwa Lowassa.

  Ni kiongozi makini, hakurupuki, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na anazijua sana taratibu za Chama.

  Hawezi kukikemea Chama chake kupitia magazetini. “Anapo mahali pa kukikosoa kama kimekosea. Ni katika vikao. Nadhani amenukuliwa vibaya.”

  Makamba alisema vurugu zinazoendelea Arusha haziwahusu na wanaopaswa kukemewa kwa kutaka kuigeuza Arusha kuwa Ivory Coast, siyo CCM kwani wao wanaamini uchaguzi uliendeshwa vizuri na mgombea wa chama chao ndiye Meya wa Arusha kwa sasa.

  Makamba alisema hoja ya Lowassa kuwataka wakae meza moja na Chadema, haina msingi
  ambapo alisisitiza “hatuna ugomvi na Chadema na mgombea wetu ameshinda, upande usioridhika na matokeo unapaswa kuyapinga kwa mujibu wa taratibu zilizopo.”

  Alisema uchaguzi huo haukusimamiwa na CCM, bali Mkurugenzi wa Jiji la Arusha hivyo kasoro kama zipo, CCM haipaswi kulaumiwa, akifafanua kuwa “upande ambao hauridhiki na matokeo hayo, unapaswa kuyapinga kwa mujibu wa taratibu zilizopo.”

  Lakini akizungumza kwa simu jana jioni kutoka nyumbani kwake Monduli, Lowassa alisema hajayaona magazeti ya jana yalivyoandika, lakini alichokisema juzi ni kwamba vyama husika vikae na kuzungumza namna ya kumaliza tofauti zao kwa sababu vurugu hazina maslahi kwa Arusha na Taifa kwa ujumla.

  “Niko Monduli, sijaona magazeti ya leo (jana), lakini nilichokisema juzi ni kwamba vyama husika, vikae na kuzungumza kwa nia ya kumaliza tofauti zao. Sijamkemea mtu, sijasema nani mshindi, nani ameshindwa. Nimetoa ushauri, kwa sababu sitaki amani ivurugwe,” alisema Lowassa.

  Alisema katika ushauri wake, hakutaja jina la chama chochote, na anaweza kuwa amenukuliwa
  vibaya, lakini la msingi alilosisitiza ni kuwa suala la kuelimishana.

  “Pengine hawajui utaratibu, ni suala la kuelimishana. Tusipigane mitaani, tuwaelimishe wenzetu. Nisingependa kuona Arusha inakuwa na vurugu, tunahitaji mji wetu uwe na amani,” alifafanua Mbunge huyo wa Monduli.

  Chadema juzi iliandaa maandamano na vijana wa chama hicho kuingia mitaani na kulifanya Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuwatawanya kwa maji ya kuwasha.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Aaahhhaaa, kumbe ndio njia Mzee Makamba anyotuelekeza kwa usahihi wake juu ya mji wa Arusha na uchakachuaji kwingineko nchini eeehh ... hujumbe umefika.

  Jaamae, tukutane Mianzini, Kambi ya Fisi, Esso na Unga Limitedi kama kazi kwa mikakati kamambe ya kuusukumilia mbali kabisa huu mlango wa ubakaji wa demokrasia nchini mwetu ambao hata ukiubisha kwa utaratibu hakuna wa kukusikia sauti ...

  Makamba tunakuja kwenye hiyo karamu ya KRISMASI uliotuandalia kupitia ujumbe huu na wala usipate kabisa shida. Andaeni polisi wa kutosha ambao nao WANAGANGA NA NJAA sawa na sisi, achilia mbali ndugu zao tulionao huku uraiani.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu, habari hii source yake???
   
 4. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huenda Lowasa ana machungu na Arusha yake na ameona mapema madhara ya hali iliyopo kwa mstakabali wa mji huo na ustawi wake tofauti na Makamba. Anyway, to wait and see!
   
 5. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lowassa was supposed to advise the Party rather than seek popularity through Media...unless Makamba "hashauriki"...
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Unaambiwa kila upande wa barabara kama kilometa nzima ama ni majengo aliojinyakulia akiwa waziri wa ardhi ama viwanja katika prime areas vinavyosubiri kuendelezwa. Sasa vita vya matajiri MAFISADI na sisi makabwela unafikiri wakupoteza zaidi ni na nani hapo???

  Maadam Mzee Makamba kaonelea vema kumwaga japo hata maji ya kunawa tu, sasa ugali na kitoweo vyote chini tu!!!!
   
 7. a

  alles JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  CCM wamechelewa sana na watakapofunguka macho makamba ameshawaharibia mengi. Pale kwa makamba zimejaa blabla, lakini ile kitu haki, busara na hekima anahitaji kujifunza kwa vijana sasa kwani haziwezi kuota na kumwagiliwa kwa sasa wakati ni jioni kwake.

  Alichokiongea Mheshimiwa Lowasa kuna dalili ya mtu mwenye mtazamo wenye kuwa na uchungu na mji wake, na hata dalili za busara zinaonyesha kuliko katibu mkuu makamba haoni nini cha muhimu kwa nchi ila mradi sisiemu wako madarakani. Inachekesha sana.

  Kwa vile kwa sisiem ni mwaka wa wanawake afadhali waziri wa ardhi wampe wadhifa wa Katibu mkuu wa sisiemu akinusuru chama.
  :embarrassed:
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Makamba hana tofauti na Hamis Mgeja, ni kweli CCM watashtuka wakati chama kimekufa.Shinyanga mgeja kaimaliza CCM
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  haya mambo ya kusema kuwa kuna mahali maalumu pa kukikosowa chama yamepitwa na wakati,kwani huko mlipo ni wajumbe tu ndio wanaoruhusiwa kuingia na hata yanayojadiliwa huwa ni siri,nadhani lowasa kafanya vizuri kuweka wazi nini kinatakiwa kufanya,makamba mambo ya kusemea ktk chama yamepitwa na wakati tunahitaji wanachama wetu wajue nini kinaendelea kwani chama si cha makamba na viongozi wake

  lowasa usitishe na makamba,fanya kile uonacho kinaweza leta amani ktk jamii

  mapinduziiii daimaaaaa
   
 11. m

  mpingomkavu Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Mkamba anamatatizo sana kwani anaonekana kuwa hakuna anchokifikiria zaidi CCM yake ambayo tayari imeshawafia yeye na MKWERE wake,anaonyesha utahira na umbumbumbu wake akafie mbali, kwani hata FISADI EL amekuwa more rational kwenye baadhi ya mambo
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Du! kweli dunia kigeugeu. Leo Lowassa anaonekana shujaa na kupongezwa hapa jamvini! Ama kweli!
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Chadema haiwezi kupata umaarufu kupitia Arusha!
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huko ni kuichokoza dola wazi wazi, watatuvunja miguu bure halafu familia yangu iteseke, utanisaidia wewe ????. Nenda peke yako
   
 15. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hao ndio GREAT THINKERS BANA !
   
 16. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako wewe akili yako ni sawa na ya Makamba!!!
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Duh, kweli kumbe wewe ndio umekufa. Chama kimeshinda Urais, Kina wabunge 76%, kina madiwani 83% bado wasema kimekufa. Hivi nawe kweli ni GREAT THINKER? Jitoe tu humu jamvini
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Ndiye Makamba mwenyewe ati.....
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mtachonga sana... Ila tu chadema haiwezi kuitumia Arusha kutafuta umaarufu! Mbaya zaidi kupitia huyo mhuni Lema!
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  hii ilivyotulia lazima iwe CHILLI SOURCETomato makamba asingejibu
   
Loading...