CCM Yamchagua Sitta kuwa mgombea pekee

Geeky

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
307
179
Tuesday, March 4, 2014.
HabariLeo
IMG_6430.JPG
Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempitisha Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwa kauli moja kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, linaripoti gazeti la HabariLeo.

Pia kamati hiyo imempitisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.

Taarifa kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo ya uongozi ya CCM iliyoketi jana, zimebainisha kuwa Andrew Chenge aliyekuwa akitajwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti, amejitoa katika kinyang'anyiro hicho kwa hiari yake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kanuni za Bunge kupitishwa, utaratibu wa kuchukua fomu utatangazwa ambapo Sitta atakwenda kuchukua na atakuwa mgombea pekee kutoka CCM.

Kitakachosubiriwa ni kuona wagombea kutoka makundi mengine kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo na kundi linalotarajiwa ni kutoka vyama vya siasa vya upinzani.

Sifa ya kwanza imetajwa kuwa ni utayari wake katika kuliongoza Bunge hilo.
"Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa Mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,"
alinukuliwa Sitta akizungumzia nia yake.

Kisheria, sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni pamoja na kuwa na
Shahada ya Sheria kutoka katika chuo kinachotambulika, pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.

Sitta anatajwa kuwa na sifa za kushika nafasi hiyo, ikiwemo uzoefu wa miaka mitano wakati alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Inaelezwa kuwa katika Bunge hilo la Tisa wakati akiwa Spika, mijadala mizito ilijadiliwa lakini hakutetereka hata kidogo.

Waziri huyo pia amekuwa akitajwa na wapambe wake kuwa anafaa kuwania nafasi ya uenyekiti kwa sababu uadilifu wake hauna shaka.

Mbali na uadilifu na uzoefu wake katika uongozi wa Bunge aliloliita la kasi na viwango, inadaiwa hata makundi mengine, wakiwemo wabunge wa upinzani na asasi za kiraia, wanamkubali.

Mwenyewe Sitta aliwahi kunukuliwa akieleza sababu ya kukubaliwa na wabunge wa upinzani kuwa wanaamini akikalia kiti hicho, ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi na haki.

Sifa ya nyingine anazotajwa nazo, ni uwezo wa kutumia busara kukabiliana na makundi yenye maslahi mbalimbali na kuwaleta pamoja.

Baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo tayari wanamuona Sitta kuwa mjumbe pekee mwenye uwezo huo, kutokana na uzoefu mdogo uliopatikana katika wiki mbili za Bunge hilo Dodoma.


Source: Tuesday, March 4, 2014.
Habari Leo.
Via : wavuti: CCM yamteua Sita kugombea Uenyekiti wa Bunge la Katiba
 
Nyie mchagueni tu,hata mumweke nani kama katiba haitakuwa ya wananchi bado tunanafasi ya kuikuta kwenye sanduku la kura
 
Hivi kumbe bunge la katiba linaendeshwa kivyama?
Sasa hii ndio fursa ya mwisho kwa Sitta kuonyesha yuko na wananchi au yuko "nao"?...
 
Huku kuingia bunge maalum na sura ya vyama ndo kunanipa wasiwasi kama katiba hii itawalenga na kuwawakilisha watanzania!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Hili jambo la kuingiza maslahi ya vyama ndo linaloleta matatizo kwenye bunge la katiba! Tumeona jana wabunge wa chama tawala wakilazimisha mambo kwa kuwaburuza wachache, binafsi namuunga mkono sitta lakini hayo masuala ya vyama ndo yanaleta matatizo baadae!
 
Sita kama hajui ni kuwa ametegwa ajimalize, ama ndani ya chama au kwa wananchi.

akitenda matakwa ya wananchi atakosa "indozmenti" ya chama muda muhimu ukifika, akikibeba chama atakosa "kredibilite" machoni pa wananchi jambo linaloweza kusababisha "kura zisitoshe" ikalazimisha mitulinga kujaribu (sijui kama itafaulu) kuokoa jahazi.

ccm wanazidi kujibana kwenye kona, wamebakisha mipasho tu, hoja kwishnehi.
 
Huku kuingia bunge maalum na sura ya vyama ndo kunanipa wasiwasi kama katiba hii itawalenga na kuwawakilisha watanzania!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
genekai
Siku zote tunasema Chadema ni wapiga deal hamna jipya; wao waliwaza posho zaidi; katiba tulipaswa kuipigia kura moja kwa moja; watanzania tunafahamu tunahitaji kitu gani; upinzani mlishindwa kushinikiza hilo kwa njaa zenu sasa unalaumu nini?
 
Last edited by a moderator:
Nyie mchagueni tu,hata mumweke nani kama katiba haitakuwa ya wananchi bado tunanafasi ya kuikuta kwenye sanduku la kura

Ndugu? % kubwa ya wapiga Kura ni hao wanaovikwa Kapelo na kulishwa uBWABWA wenye uelewa wa mambo walio wengi wanakaa hom kutokwa POVU wanajiita wadadis wa mambo SHAME,,! 2kubali kuwa mchakato umekosewa tangu mwanzo so hadi hapa 2subiri Huruma ya CCM tu,,! hutaki unaacha!
 
genekai
Siku zote tunasema Chadema ni wapiga deal hamna jipya; wao waliwaza posho zaidi; katiba tulipaswa kuipigia kura moja kwa moja; watanzania tunafahamu tunahitaji kitu gani; upinzani mlishindwa kushinikiza hilo kwa njaa zenu sasa unalaumu nini?
Kwa maneno hayo c ndo unaungana na Wanaoiponda CCM kuwa ipo kwaajili ya Wanufaika wachache2! Ikiwa CDM walifikiria posho kwa nini ccm hawakuwa na hilo kwa Maslah mapana ya TAIFA?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu? % kubwa ya wapiga Kura ni hao wanaovikwa Kapelo na kulishwa uBWABWA wenye uelewa wa mambo walio wengi wanakaa hom kutokwa POVU wanajiita wadadis wa mambo SHAME,,! 2kubali kuwa mchakato umekosewa tangu

mwanzo so hadi hapa 2subiri Huru

ma ya CCM tu,,! hutaki unaacha!


Sisi tunasubiri huruma ya MUNGU kwa watu wake. ccm wana huruma gani!????
 
genekai
Siku zote tunasema Chadema ni wapiga deal hamna jipya; wao waliwaza posho zaidi; katiba tulipaswa kuipigia kura moja kwa moja; watanzania tunafahamu tunahitaji kitu gani; upinzani mlishindwa kushinikiza hilo kwa njaa zenu sasa unalaumu nini?

kwa hiyo kumbe na wewe ni mmoja wetu tunayeamini kuwa wapinzani wapo sahihi??? tunaoamini kuwa ccm hawana nia ya kuleta katiba ya watz wote??? unapolaumu wapinzani huku ukisapoti ccm una maana ipi??? ni unafiki au???? wewe binafsi umeshiriki vp kuhakikisha tunapata katiba bora????? ulitaka nani akupiganie huku wewe ukiendekeza ushabiki wa kijinga kwa magamba???? nani ana wajibu wa kukupigania wewe badalla ya kujipigania????? Amka iunge mkono cdm ili kwa pamoja tupiganie maslahi mapana ya taifa letu!!!!
 
Last edited by a moderator:
genekai
Siku zote tunasema Chadema ni wapiga deal hamna jipya; wao waliwaza posho zaidi; katiba tulipaswa kuipigia kura moja kwa moja; watanzania tunafahamu tunahitaji kitu gani; upinzani mlishindwa kushinikiza hilo kwa njaa zenu sasa unalaumu nini?
Kwa maneno hayo c ndo unaungana na Wanaoiponda CCM kuwa ipo kwaajili ya Wanufaika wachache! Ikiwa CDM walifikiria posho2! kwa nini ccm hawakuwa na hilo Wazo Ulilopendekeza? kwa Maslah mapana ya TAIFA?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom