CCM Yakubali yaishe, Bunge Maalum la Katiba kuahirishwa

Akiongea kwa njia ya simu kutoka dodoma, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Ndg. Nape Nnauye amesema CC imeridhishwa na hoja za kukosekana kwa akidi ya 2/3 hivyo kwa kuzingatia maslahi mapana ta taifa wameona ni busara kuachana na vikao vya Bmk kuanzia kesho Alhamis tar 21 aug 2014.
Source: Radio Uhuru mchana huu.
ahaa, Vipi kuhusu pesa walizotumia kwa kuendelea na mchakato ambao hata watoto wa chekechea walijua akidi haitatatimia,watazirudisha? na hakuna namna yoyote ile ya kuwatafuta wanasheria kufungua kesi ya ufujaji wa mali ya umma? na je kabla ya kuanza tena BMK hawakuliona hilo au walifanya makusudi wakijua hakuna mtu wa kuwauliza, kwa maana wao ndio watawala?.
 
Kama huu sio uzushi sisi CHADEMA kwa akili zetu timamu tunapinga maamuzi haya kwa vile hawakutuhusisha na ni ya pupa mno tutazunguka nchi nzima na chopa kushawishi maandamano.
 
Kumekuwepo na vichwa mbalimbali vya habari kwenye magazeti juu ya kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vichwa hivyo vya habari ambavyo ni CCM YAJIPA MTIHANI-NIPASHE, UAMUZI MGUMU CCM-Mwananchi na vingine vingi ambavyo vinatoa habari ya kudhani ya kwamba Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi inakutana ili kutoa uamuzi wa kusitisha mchakato wa Katiba Mpya na kwamba Kamati kuu hiyo inategemewa kuazimia kulivunja/ kulisimamisha Bunge Maalum la Katiba linaloendelea hivi sasa Dodoma.

Kwanza kabisa, ningependa watanzania wafahamu kuwa CCM NI IMARA, Chama ambacho hakijawahi kuyumbishwa kwa namna yeyote na Upinzani ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Bado Chama Cha Mapinduzi ni Chama Imara sana kinachopendwa na kuaminiwa na Watanzania walio wengi. Na hatusemi hivyo kwa kubahatisha, kuropoka au kujipa matumaini/kujifariji kama wafanya wengine, bali tunasema kwa uhakika na kujiamini. Matokeo ya Uchaguzi, katika chaguzi ndogo mbalimbali zilizojitokeza hapa nchini zinatoa tafsiri halisia juu ya maneno yangu kuwa CCM ni IMARA.

Hivyo watanzania hawapaswi kuaminishwa hata mara moja na maneno ya dhahania ya magazetini ambayo yana mlengo wa Upinzani kuwa CCM itachukua uamuzi wa kuvunja Bunge la Katiba, si tu kuwa haikutani kujadili hilo bali hata kufikiria haijawahi kufikiria, kwani haiwezekani kwa Chama Makini cha siasa tena chenye dhamana ya kuendesha na kusimamia Dola kikawa mstari wa mbele kuvunja utaratibu wa kisheria na kikanuni wa kuvunja Bunge Maalum la Katiba na ni vizuri watanzania wakatambua kuwa si tu kuwa CCM haiwezi kufanya hivyo bali hata Bunge lenyewe la Katiba halina mamlaka ya kujivunja.
Historia inatuambia kuwa kabla ya TUME ya warioba, hapo nyuma kulikuwa na tume mbalimbali zilizoundwa kwa masuala kadha wa kadha, nitatolea mfano wa tume mbili nazo ni; Tume ya Nyalali iliyoundwa na Mhe Rais wa awamu ya Pili Ndugu Ali Hassan Mwinyi, ilikabidhi ripoti ya tume yake ambayo yalisema kuwa asilimia 80% ya watanzania hawataki vyama vingi, lakini KWA UTASHI wa Rais maamuzi hayakufuata mapendekezo ya TUME hiyo na kwa kuheshimu Sheria na Mamlaka ya aliyemteua Jaji Fransis Nyalali hatukumsikia kwenye televisheni, vipindi vya redio wala kwenye makongamano.

Lakini mfano wa pili ni wa Tume ya Jaji Kisanga ambapo ingawa watanzania walio wengi wa bara na visiwani walipendekeza mfumo wa Serikali Mbili (2) Jaji Kisanga na tume yake alipendekeza huwepo wa Serikali tatu (3) lakini Rais wa Awamu ya tatu Mhe Benjamin Mkapa alimjibu kuwa hilo halipo kwenye hadidu za rejea alizopewa. Jaji Kisanga si yeye wala si wajumbe wa tume yake hawakwenda katika studio za televisheni au redio kutetea busara zao na wala hawakushiriki katika midahalo au makongamano. JAJI KISANGA ALIHESHIMU NA KUTII MAMLAKA. Jaji alikuwa muungwana na mstaarabu.

Ni vizuri kufahamu kuwa Tume ya Jaji Warioba imeishavunjwa na Rais Kikwete kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3 ambayo inampa Rais Mamlaka ya kuivunja pindi inapowasilisha Rasimu ya Katiba. Kazi ya tume kisheria hazipo tena kama ilivyo kwa tume za Nyalali na Tume ya Jaji Kisanga.

Ni vizuri pia kufahamu kuwa, maridhiano ya kuandika katiba mpya yatafanyika ndani ya bunge kama sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za uendeshaji wa Bunge Maalum zinavyoelekeza na siyo barabarani. Mchakato wa Katiba umefikia hatua ya tatu ambapo wajumbe wa Bunge Maalum kwa sasa ndiyo wenye Mamlaka kisheria ya kuamua nini kiwepo kwenye Katiba mpya kabla ya kupigiwa Kura ya Maoni na wananchi.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina viongozi makini, wenye weledi, wazoefu na waadilifu ambao kamwe hawako tayari kuliona Taifa likiangamia kwa hulka, visasi na tamaa ya madaraka ya baadhi ya makundi. Tumeahidi na kuapa ndani ya Chama kuwa tutailinda na kuitetea nchi hii, katiba yake na wananchi wake.

mimi sina upeo kubwa sana kufikiri ila Naona Wewe umekariri, husomi alama za nyakati na kubwa zaidi unashindwa hata kutambu aliyekuwa na Miaka 15, 2010 sasa anaweza kupiga kura.. Mabadiliko ni magumu ila yakupasa ukubaliane nayo.
 
kama huu sio uzushi sisi chadema kwa akili zetu timamu tunapinga maamuzi haya kwa vile hawakutuhusisha na ni ya pupa mno tutazunguka nchi nzima na chopa kushawishi maandamano.

nguli acha utani na ushabiki wa mambo nyet kama haya,huu ndo uchochez,unastahili kukamatwa
 
nguli acha utani na ushabiki wa mambo nyet kama haya,huu ndo uchochez,unastahili kukamatwa

Mkuu usi panic huu uzi wenyewe ni uzushi. Ila Kama umekasirika sana njoo nikamate haraka iwezekanavyo ukishindwa naanzisha maandamo
 
kama huu sio uzushi sisi chadema kwa akili zetu timamu tunapinga maamuzi haya kwa vile hawakutuhusisha na ni ya pupa mno tutazunguka nchi nzima na chopa kushawishi maandamano.

ukawa hooyeeeeeeeeeeeeeeee!!!!
 
mbona hii habari ishakanushwa na katibu mwenezi

Mimi nawashangaa moderators wa jf. Mara tu baada ya kusikia maamuzi ya kikao kilichomalizika jana na katibu mwenezi wa chama kuweka wazi maamuzi yao ya kuendelea kwa bunge maalum la katiba uzi huu ungeshatolewa.
 
Yaani kama sisiem wangekuwa na uhakika wa 2/3, tungekoma ubishi, suala la maridhiano wasingelitamka hatakidogo. joha ingebaki oooooh nini nini na nini kwa mujibu wa sheria! Hasa Wasira na Lukuvi. Hawa wabinafsi saaana.
 
Ngoja nizitafute zile threads za Nguruvi3 nizisome kwa makini...

Nahisi kama kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria hapa, iweje CCM ndio awe muamuzi wa ama kuendelea au kuhairishwa kwa bunge?
Na wala klatiba haikuwahi kuwa katika ilani yao ya uchaguzi au sera zao.

Unaona jinsi wanavyohangaika. Hata hivyo nguvu ya umma siku zote inashinda. Na inaelekea huko sasa.
 
Na wala klatiba haikuwahi kuwa katika ilani yao ya uchaguzi au sera zao.

Unaona jinsi wanavyohangaika. Hata hivyo nguvu ya umma siku zote inashinda. Na inaelekea huko sasa.

Nape amegoma. Uchakachuaji utaendelea na katiba ya CCM lazima ipatikane.
 
Back
Top Bottom