@Sidhani kama wameamua kudharau wito wa maombolezo, Nafikiri wahusika kwenye ofisi za CCM watakuwa wamejisahau tu, maana wengi wako busy sana na shughuli zao binafsi. @Lakini wapo wengine wanapeperusha bendera ya CCM kwenye mazingira yao kama utamaduni, au kuficha biashara haramu zinazofanywa kwenye mazingira yao, au kukwepa usumbufu wa polisi na maafisa wa kodi. Kwa ujumla wengi wao sio wanaCCM halisia hivyo hawana muda na mchango wowote kwa chama chao, kwa hivyo suala la kupeperusha bendera nusu mlingoti ni msamiati na zoezi gumu sana kwao.