Kufuatia kupanda kwa joto la kumsaka mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia CCM na songombingo la Zanzibar, Kamati Kuu ya CCM (CC) imeitishwa kwa dharura. Nyaraka za kikao hicho zinaonesha kuwa CC itajadili songombingo la Zanzibar na kuanza kupanga nondo za kuchambua na kuchuja watiania wa CCM. Kikao hicho cha dharura kinatazamiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na kitafanyika Dodoma.
Kulingana na taarifa nilizonazo,kikao kitafanyika kesho.CC inagusia pia malalamiko ya rushwa toka kwa watiania waliorejesha fomu. Yametolewa malalamiko lukuki yachomayo kama mkuki hasa juu ya wakati wa kusaka wadhamini mikoani. Ni kutoka kwa watia nia wenyewe. Wapo waliowasilisha nyaraka na shahidi nyinginezo kushuhudia rafu za baadhi ya watiania.JF will be the first to know kitakachojiri kikaoni!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam