CCM yahoji Serikali ya Umoja Zanzibar

CCM yahoji Serikali ya Umoja Zanzibar

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
zenji.jpg

Wakazi wa Zanzibar wakiitikia salamu wakati Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia katika Viwanja vya Kibandamaiti.

Zanzibar. Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Salmin Awadh Salmin amesema wawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza hilo ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), au la.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja jana, Salmin alisema wajumbe hao wamefikia hatua hiyo kwa kuwa wanaona kwamba lengo na matumaini ya kuundwa kwake yamefutika na hayana dalili njema katika siku za usoni.

Alisema ni vyema wananchi wakaulizwa kama bado wana hamu na mfumo huo au ule wa zamani urejeshwe.

"Kitendo cha viongozi tuliounda nao umoja wa kitaifa kupinga Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar hakivumiliki, tunaona ipo haja kila upande ubaki na msimamo wake kuliko kujenga urafiki wa mashaka," alisema Salmin ambaye ni Mwakilishi wa Magomeni CCM.

Alimwomba Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa ili kutoa nafasi mpya ya kidemokrasia kwa wananchi wake kujua kama wanataka mfumo wa sasa au wa zamani.

Wazo hilo liliungwa mkono na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alisema ni jambo muhimu kuitishwa kura ya maoni ili wananchi wapate nafasi ya kuulizwa kama wanataka mfumo wa Serikali iliyopo au la kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu mwakani.

Kinana amshukia Maalim

Awali, Kinana alisema kwa miaka 20 tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad amekuwa akiwayumbisha Wazanzibari kutokana na tabia yake ya kubadilisha ajenda za kisiasa na kutikisa misingi ya umoja wa kitaifa nchini.

Alisema tabia ya kiongozi huyo imekuwa haifahamiki na haijulikani anatafuta jambo gani licha ya kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoundwa mwaka 2010 na CCM na CUF.

Alisema kwa msingi huo, tabia ya kiongozi huyo mbali na kuonekana kutaka kuzorotesha misingi ya umoja wa kitaifa pia imekuwa ikichafua siasa za Zanzibar na Muungano na kuwataka wananchi kuwa macho hasa katika mjadala wa Katiba unaoendelea nchini.

"Tabia ya Maalim Seif haifahamiki, ni bingwa wa kubadilisha ajenda za kisiasa mara kwa mara akiwayumbisha wananchi. Tokea kuanzisha vyama vingi, ameshabadili ajenda zaidi ya 20, amewaacha wananchi hawajui washike lipi na waamini jambo gani," alisema.

Alisema Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano lazima ipatikane kwa njia ya amani na isiwe kichocheo cha watu kung'oana macho au kutoana ngeu na kwamba mabadiliko ya katiba si mwarobaini wa maendeleo akisema mataifa mengi yamewahi kuandika katiba mpya na bado kuna kero za wananchi.

Aliwataka wabunge na wawakilishi wa CCM kukaa pamoja na kutafakari kwa kina jinsi ya kuondosha kero zinazolalamikiwa na wananchi wa Zanzibar na kuipa Zanzibar nafasi pana ili ijiimarishe kiuchumi.

Chanzo:Mwananchi
 
Hivi kuna kiongozi aliyepinga Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar? Kati ya CCM na CUF, ni chama gani kinachowayumbisha watanzania? Wanawasiwasi gani wa kusubiri kupiga kura ya maoni kwa katiba yao wanayoitengeneza sasa huko Dodoma, na wanataka kwanza wapige kura ya maoni ili kuvunja serikali ya moja wa kitaifa (SUK). Kama weli CCM wanataka serikali mbili, kwanini wasivunje katiba mpya ya Zanziba ambayo ndiyo kiini cha watu wa bara kudai Tanzanyika yao huru? Kama CCM walikuwa hawajui wazanzibari ndiyo wanaogeuka na siyo Maalim Seif, wajaribu kuchokonoa hayo waone jinsi CCM na CUF Zanzibar watakapoungana pamoja na kuwaumbua. Hayo mambo ya kuburuza watu watufanyie huku bara ambao hatujui hata Tanganyika ilipo na tupo kimya tu.
 
UKAWA= Umoja wa Kichaga na Wapemba! Toa hao kwenye serkal ya Mapinduzi waendelee na mipasho yao kibanda maiti.
 
CCM inawasomi waliomaliza madarasa lakini hawajaelimika!

Kura ya maoni ambayo ilitakiwa ifanywe kwa wakati tulionao ni ya kuwauliza wanannchi wanataka mfumo wa serikali ngapi.

SUK iwepo au isipokuwepo haiwezi kubadili msimamo wa viongozi wa upinzani Zanzibar na theluthi mbili ya kura bado itaendelea kuwa ndoto ya mchana kweupe!
 
Inanishangaza wakifanya CCM kile walichofanya Upinzani hakina nongwa,lakini wakifanya upinzani mh! Majina hayo,mengi.
 
Kura ya maoni inayotakiwa ni: JE, MUUNGANO UEMDELEE? Hii ni kutokana na ukweli kuwa Zanzibar haijawahi kuridhia makubaliano ya muunagano. Baada ya hapo ndo ujadiliwe mfumo wa serikali uweje
 
Hawa wanatafuta kigezo cha kuwasingizia wananchi ili waonekane kuwa wananchi ndio walioamuwa wakati hakuna hata mwananchi aliyelalamikia muafaka uliopo.
 
Mbona iko wazi hata juzi tu Mzee Mtei alikiri kuwa muungano hauna tija? UKAWA nia yao kuu ni kuufuta MUUNGANO. Lisu alishasema muungano si halali sasa tunamuuliza nani tena kama ukawa hawataki muungano ama la?

Maalim Seif yupo kwenye serikali hiyohiyo alafu anahamasisha wananchi wadai katiba ya the soo called "katiba ya wananchi" ilihali yupo madarakani akitumwa kwenda kusimamisha maandano atakua tayari? Tuache unafiki kwenye siasa zetu. Tuwe realistic, tunataka muungano au hatuutaki tuitishe kura ya maoni wenye nchi yao waamue. Aina ya muungano pia wenye nchi yao waamue si kikundi tu kwaajili ya madara wawaamulie watanzania. Mbona jana Juma Duni Haji alilisemea vyema hili ingawa kifalsafa?
 
Hiyo serikali unayojaribukuitetea ndiyo yenyewezo wa kitisha kura ya maoni ili ananchi waamue ni mundo upi wa serikali wanaouaka. Sasa jiuze kwa nini hawanyi hivyo na badala yake wanawatuma akina Nape na Kinana kushindana na UKAWA majukwaani!!?? Kwa ujumla JK na CCM yake walshalioroga sasa tuwaachie walinywe wenyewe.
 
chama tajiri hiki, yaani kabla ya mkutano kofia na Tshirts zinagawiwa kama njugu, hawa wamasai wa zenji watakuwa wamechelewa mgawo!!

zenji.jpg
 
Siku zote Zanzibar wamekuwa wakisema kuwa chanzo cha migogoro ya kisiasa Visiwani humo ni CCM-Tanganyika.

Sasa kama hili la kuhoji serikali ya umoja wa kitaifa ni la kweli basi hoja ya wanzanzibari inasimama.
 
UKAWA= Umoja wa Kichaga na Wapemba! Toa hao kwenye serkal ya Mapinduzi waendelee na mipasho yao kibanda maiti.
kweli mmeshikwa pabaya, mtaita majina yote - hata maji mtayaita mma!! na bado mziki haujaanza rasmi, ni rasha rasha tu hizo wana Lumumba za masika mbona bado!!
 
Siku zote Zanzibar wamekuwa wakisema kuwa chanzo cha migogoro ya kisiasa Visiwani humo ni CCM-Tanganyika.

Sasa kama hili la kuhoji serikali ya umoja wa kitaifa ni la kweli basi hoja ya wanzanzibari inasimama.

Kw hilo CCM Tanganyika itashindwa. Pamoja na Yusuf Makamba kuhujumu mazungumzo ya maridhiano, Karume na Seif kwa juhudu zao wenyewe wameleta maridhiano Zanzibar. Nadiriki kusema hivi kwa juhudi za Wanzanzibari wazalendo S3 itapatikana CCM itake isitake.
 
kama walishindwa kuzuiya 2010 wataweza sasa MSETO (GNU) ipo kikatiba,tunawajua kwa majina wanao tugombanisha WAZANZIBAR lakini tunawambia maweee hahahahahahh.Na wanakotoka tunakujua....................... THE GOVERNMENT OF NATIONAL UNIT(GNU) IS HERE TO STAY......wanajitia aibu bure baadhi ya wahafidhina,wakuja wazanzibara hebu msituchafue msituchafulie maji.

kisoge 1.jpg
wanafikiri tumesahau wakati walipopinga maelewano znz...walichokuwa wakikihofia ni wazanzibar kushikana wakakomboa nchi yao. BASI NA WATULIEEE MUDA NI HUU.
''SIKU 31/7/2010 WAZANZIBAR WALIPOUNGANA 66% KWENYE KURA YA MAAONI ndio siku hiyo zanzibar ilirudi kuwa nchi AND FROM THAT DAY ZANZIBAR WILL NEVER BE THE SOME AGAIN''
b.JPG
sasa basi wahafidhina kama hawajui wapi tunaelekea SASA NI BORA WANYAMAZE TU WASITUKASIRISHE BUREEEEView attachment 155912 flana-220x126.jpg ''ACTION AND REACTION ARE ALWAYS EQUAL AND OPPOSITE''
mbele daima kurudi nyuma mwiko``

''JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR JUU YA MEZA KWANZA muungano baadaeee''
 
Kama CCM wameichoka Amani Zanzibar, wapeleke hiyo hoja haraka! Kuna watu ndani ya CCM ambao hawamtakii mema Kikwete, mpasuko sasa unazidi kuchukua sura mpya kila kukicha!!!!
 
Sikuwahi kujuwa kuwa Zanzibar ina raia wa Kimasai!

Mkuu ni sera ile ile ya kusafirisha watu toka sehemu moja kwenda nyingine ili ionekane mikutano yao imejaa usishangae wamasai hao wa chalinze ukawaona tena kwenye mkutano wao Mtwara hizo ndizo siasa muflisi mmasai afanye nini zanzibar:shetani: ccm
 
zenji.jpg

Wakazi wa Zanzibar wakiitikia salamu wakati Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia katika Viwanja vya Kibandamaiti.

Zanzibar. Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Salmin Awadh Salmin amesema wawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza hilo ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), au la.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja jana, Salmin alisema wajumbe hao wamefikia hatua hiyo kwa kuwa wanaona kwamba lengo na matumaini ya kuundwa kwake yamefutika na hayana dalili njema katika siku za usoni.

Alisema ni vyema wananchi wakaulizwa kama bado wana hamu na mfumo huo au ule wa zamani urejeshwe.

"Kitendo cha viongozi tuliounda nao umoja wa kitaifa kupinga Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar hakivumiliki, tunaona ipo haja kila upande ubaki na msimamo wake kuliko kujenga urafiki wa mashaka," alisema Salmin ambaye ni Mwakilishi wa Magomeni CCM.

Alimwomba Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa ili kutoa nafasi mpya ya kidemokrasia kwa wananchi wake kujua kama wanataka mfumo wa sasa au wa zamani.

Wazo hilo liliungwa mkono na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alisema ni jambo muhimu kuitishwa kura ya maoni ili wananchi wapate nafasi ya kuulizwa kama wanataka mfumo wa Serikali iliyopo au la kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu mwakani.

Kinana amshukia Maalim

Awali, Kinana alisema kwa miaka 20 tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad amekuwa akiwayumbisha Wazanzibari kutokana na tabia yake ya kubadilisha ajenda za kisiasa na kutikisa misingi ya umoja wa kitaifa nchini.

Alisema tabia ya kiongozi huyo imekuwa haifahamiki na haijulikani anatafuta jambo gani licha ya kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoundwa mwaka 2010 na CCM na CUF.

Alisema kwa msingi huo, tabia ya kiongozi huyo mbali na kuonekana kutaka kuzorotesha misingi ya umoja wa kitaifa pia imekuwa ikichafua siasa za Zanzibar na Muungano na kuwataka wananchi kuwa macho hasa katika mjadala wa Katiba unaoendelea nchini.

"Tabia ya Maalim Seif haifahamiki, ni bingwa wa kubadilisha ajenda za kisiasa mara kwa mara akiwayumbisha wananchi. Tokea kuanzisha vyama vingi, ameshabadili ajenda zaidi ya 20, amewaacha wananchi hawajui washike lipi na waamini jambo gani," alisema.

Alisema Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano lazima ipatikane kwa njia ya amani na isiwe kichocheo cha watu kung'oana macho au kutoana ngeu na kwamba mabadiliko ya katiba si mwarobaini wa maendeleo akisema mataifa mengi yamewahi kuandika katiba mpya na bado kuna kero za wananchi.

Aliwataka wabunge na wawakilishi wa CCM kukaa pamoja na kutafakari kwa kina jinsi ya kuondosha kero zinazolalamikiwa na wananchi wa Zanzibar na kuipa Zanzibar nafasi pana ili ijiimarishe kiuchumi.

Chanzo:Mwananchi

Zanzibar imetulia sasa wazanzibar hawapigani tena, sasa huyu jamaa anataka zanzibar irudi kule kule ilipotoka,kweli CCM hawaitakii mema zanzonar
 
Back
Top Bottom