CCM yafuata nyayo za CHADEMA, CUF

CCM yafuata nyayo za CHADEMA, CUF

Keben

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
725
Reaction score
177
Siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuutangaza mwaka 2013 kama mwaka wa kazi kupitia falsafa ya nguvu ya umma na Movement For Change (M4C), Chama Cha Mapinduzi CCM nacho kimeibuka na kuutangaza mwaka huo kwamba utakuwa wa kazi kwao huku kikisema chenyewe kitatumia falsafa ya "Nguvu ya Mungu".

CCM kimetangaza kuzunguka nchi nzima kuanzia mwakani na kuhusisha viongozi wao kuanzia ngazi ya shina hadi ngazi ya Taifa na
kusema kwamba wameshindwa kufanya kazi hiyo mwaka huu kutokana na kuwepo uchaguzi ndani ya chama hicho. Chadema imekuwa kikitumia kauli mbiu ya "Nguvu ya Umma" kupitia Movement For Change (M4C) huku Chama cha Wananchi (CUF) nacho
kikizunguka mikoani kikitumia falsafa ya "Vugu vugu la Mabadiliko maarufu kama Vission For Change (V4C) kwa ajili ya kujijenga kwa wanachama wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dra es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba, alisema kazi ya kuzunguka mikoani kuanzia mwaka 2013, itafanywa na Sekretarieti ya CCM. "Chadema wao wanasema wanatumia nguvu ya umma, lakini sisi CCM tunasema tutaweza kufanikisha kazi ya kuzunguka mikoani kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kutumia nguvu ya Mungu," alisema.

Nchemba alisema kila kiongozi wa CCM katika eneo lake atatakiwa kukagaua miradi iliyotokana na Ilani yao ya mwaka 2010 na kutoa taarifa katika ngazi ya juu huku Sekretarieti iifazunguka mikoani kwa makundi kuangalia utekelezaji wake. Hata hivyo, Nchemba alikiri kwamba baadhi ya ahadi zilizotolewa na CCM, ikiwamo kununua Meli katika baadhi ya maziwa makubwa pamoja na kujenga majengo ya kusaidia wafanyabaishara ndogo ndogo (Wamachinga), bado zimeendelea kuwa kitendawili.

"Ahadi hizi kubwa inabidi tuwaulize watu wa serikalini ili watuambie imefikia wapi, lakini bado haijatekelezwa mpaka sasa ingawa ahadi hizo zilitolewa na mgombea wetu," alisema Nchemba. Wakati CCM kikitangaza mikakati kwa mwaka 2013, mwaka huu pia kilitangaza mpango kama huo na viongozi wake walifanya ziara mbalimbali zilizolenga kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM wakiwa wameambatana na Mawaziri kwamba hazikuwa na tija wala maana yoyote.

Chanzo: Nipashe leo
 
mhh Kwa nguvu ya Mungu?
hii kali mtuhadae halafu mseme Ni nguvu Ya Mungu?
wacha utani Mwigulu, na hapo kwenye ahadi vipi ziwe kitendawili na mlisema kabla JK hajaondoka mgogoni mtatekeleza ahadi zote ?
 
mhh Kwa nguvu ya Mungu?
hii kali mtuhadae halafu mseme Ni nguvu Ya Mungu?
wacha utani Mwigulu, na hapo kwenye ahadi vipi ziwe kitendawili na mlisema kabla JK hajaondoka mgogoni mtatekeleza ahadi zote ?

Si nguvu ya Mungu bali wanamaanisha nguvu ya mungu.

NB. kunatofauti kati ya Mungu yenye herufi kubwa, na mungu yenye herufi ndogo. God & gods.

Nawaonea huruma albino.
 
Mungu hasimamii wizi, mauaji na dhuluma kwa wananchi. Ni Mungu gani huyo wanayemtegemea kama wayafanyayo yanapingana na amri za Mungu? Waache kufuru, itawamaliza.
 
aisee CCM wanaongoza kwa kujitia aibu, hivi falsafa ya NGUVU YA UMMA huyu nchemba anaelewa maana yake kweli????
CCM ni sawa mwanafunzi anayeigilizia kwa mwenzake kwenye chumba cha mtihani ila kwa uoga anakosea anacopy jibu la swali la kwanza na kuliweka kwenye swali la pili.
 
mungu yupi? je wa mbinguni tunaemtegemea wote? ni mungu gani? wa kusaidia wezi, waongo,mafisadi, waficha mahela nje? madhulumati? oo mugulu pole. Mungu wa utukufu asitajwetajwe na wenye mawaa.
 
Nafurahi kuwa CHADEMA sisi tuna anzisha wao wana copy!CCM eti nguvu ya mungu mke wake cuf nae eti v4c!khaaah...
 
natamani 2013 ifike ili nione political drama za ccm zinavyochuana na democritazation drama za chadema.

chonde chonde mwenye zile ahadi za CCM za 2010 naomba aziweke hapa tuzitumie kupima miaka miwili ya utekelezaji wake.

welcome 2013 a year of evidences
 
Wapange nini kwa akili gani waliyokuwa nayo kwa maendeleo na masilahi ya mlala hoi? Mipango waliyonayousiku na mchana ni kuchafua watu, kuibia walalahoi, kusaliti walalahoi, kuua walalahoi, kuhadaa walalahoi kwa namna mbali mbali zikiwemo data feki za kupika (siku hizi watu binafsi, taasisi binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, wanatakwimu sahihi au zinazo karibiana na ukweli kuliko serikali). Wazo kuu kichwani mwao ni wizi na kuhadaa, basi! Ole wao walitajao jina la Bwana bure! Imeandikwa usilitaje bure jina la Bwana bure. Mungu hawatumi CCM kuiba na kuhadaa walalaho. Mungu alisaidia masikini (walalahoi) na hata kutoa mwanaye Yesu kama sadaka ili kuwakomboa, hii ni kinyume na matendo ya CCM hata mtoto wa darasa la tatu anaweza kuthibitisha hili pasi-na-shaka. Hakika haya ni maudhi kwa mungu na mungu hadhihakiwi! Ndiyo, Mungu halipi kisasi lakini ni vizuri CCM wakazingatia Angalizo la kutotaja jina la Mungu! Neno Nguvu ya Mungu ni maneno machache na mazito ambayo CCM sioni kama wanaweza kuyaishi achilia mbali hawakuweza tangia hapo hususani baada ya kifo cha Mwalimu! Magamba yamewagandia wamalize hilo kwanza??? Leo hii kuna kazi eti ya kusafisha chama kwa kuwachukulia hatua walioshinda kwa nguvu ya pesa nawaonea huruma Mzee Kinana na P. Mangula, angalia sana na mizizi ya rushwa mayotaka kuhadaa wadanganyika eti mnataka kuingoa. Utakata vipi mti uliokalia au uliopanda juu yake?. Mtahangaika sana ili kuhadaa, mpango haujaanza lakini mpaka sasa watu wameshafahamu mwisho wake. Mwenzenu kajaribu kutikisa kiberiti eti kuwavua gamba limemtoka yeye, wao al… kwa raha zao!. Cheza na akili za wadanganyika siyo Mungu, huyu siyo mwanamikakati mwenzenu!
 
Mfa maji haachi kutapatapa copy n paste
 
“Nguvu ya Mungu”

hahaaaaa eti falsafa ya nguvu ya mungu????????? sasa ni dhahiri ccm imejiandaa kikamilifu kuwa chama cha upinzani
 
Usilitaje bure jina la Mungu wako! Kwa wale waliopitia mafunzo ya kipa imara mwaweza kutusaidia ni amri ya ngapi hii?
Atom ni amri ya pili nayo yasema:-
Usilitaje bure jina la bwana Mungu wako maana Bwana atamhesabia kuwa anahatia mtu alitajae bure jina lake....
 
Walishajua kuwa wananchi hawana imani tena na CCM na si rahisi kuwarubuni tena. Hivyo nafasi pekee iliyobaki ni kumgeukia Mungu pengine atende maajabu. Lakini kwa sisi wakristu, Mungu hadhihakiwi kamwe. Kila mtenda mema hulipwa mema bali mtenda maovu hulipwa kwa uovu wake. Mamlaka yenye kumcha Mungu na kufuata misingi ya uumba hutenda mema yanayompendeza Mungu ili kujiwekea akiba ktk utukufu wa milele.
 
Nape ni NANGA lakini Mwigulu ni NANGA ya tope zito .Hakika hawa watu 2 ndani ya CCM pomoja na Wassira mh .Achilia mbali wengine walio choka .
 
Siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuutangaza mwaka 2013 kama mwaka wa kazi kupitia falsafa ya nguvu ya umma na Movement For Change (M4C), Chama Cha Mapinduzi CCM nacho kimeibuka na kuutangaza mwaka huo kwamba utakuwa wa kazi kwao huku kikisema chenyewe kitatumia falsafa ya “Nguvu ya Mungu”.

CCM kimetangaza kuzunguka nchi nzima kuanzia mwakani na kuhusisha viongozi wao kuanzia ngazi ya shina hadi ngazi ya Taifa na
kusema kwamba wameshindwa kufanya kazi hiyo mwaka huu kutokana na kuwepo uchaguzi ndani ya chama hicho. Chadema imekuwa kikitumia kauli mbiu ya “Nguvu ya Umma” kupitia Movement For Change (M4C) huku Chama cha Wananchi (CUF) nacho
kikizunguka mikoani kikitumia falsafa ya “Vugu vugu la Mabadiliko maarufu kama Vission For Change (V4C) kwa ajili ya kujijenga kwa wanachama wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dra es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba, alisema kazi ya kuzunguka mikoani kuanzia mwaka 2013, itafanywa na Sekretarieti ya CCM. “Chadema wao wanasema wanatumia nguvu ya umma, lakini sisi CCM tunasema tutaweza kufanikisha kazi ya kuzunguka mikoani kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kutumia nguvu ya Mungu,” alisema.

Nchemba alisema kila kiongozi wa CCM katika eneo lake atatakiwa kukagaua miradi iliyotokana na Ilani yao ya mwaka 2010 na kutoa taarifa katika ngazi ya juu huku Sekretarieti iifazunguka mikoani kwa makundi kuangalia utekelezaji wake. Hata hivyo, Nchemba alikiri kwamba baadhi ya ahadi zilizotolewa na CCM, ikiwamo kununua Meli katika baadhi ya maziwa makubwa pamoja na kujenga majengo ya kusaidia wafanyabaishara ndogo ndogo (Wamachinga), bado zimeendelea kuwa kitendawili.

“Ahadi hizi kubwa inabidi tuwaulize watu wa serikalini ili watuambie imefikia wapi, lakini bado haijatekelezwa mpaka sasa ingawa ahadi hizo zilitolewa na mgombea wetu,” alisema Nchemba. Wakati CCM kikitangaza mikakati kwa mwaka 2013, mwaka huu pia kilitangaza mpango kama huo na viongozi wake walifanya ziara mbalimbali zilizolenga kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM wakiwa wameambatana na Mawaziri kwamba hazikuwa na tija wala maana yoyote.

Chanzo: Nipashe leo

alieleta hii habari ameichakachua mno.gazeti ht mi nnalo halijaandika ivo.
 
CCM wavivu wa kufikiri mpaka lini copy n paste? Nguvu ya umma vs Nguvu ya Mungu
 
natamani 2013 ifike ili nione political drama za ccm zinavyochuana na democritazation drama za chadema.

chonde chonde mwenye zile ahadi za CCM za 2010 naomba aziweke hapa tuzitumie kupima miaka miwili ya utekelezaji wake.

welcome 2013 a year of evidences

hapa kwetu walituahidi maji na makompyuta kwenye kura za maoni bila shaka huu ni mwk wa nne hamna lolote. halafu wanasema wtatumia nguvu ya mungu huo ni uongo waseme watatumia nguvu ya mabilioni ya Uswis pumbv.....
 
Back
Top Bottom