CCM ya sasa ni alama ya Uovu

Wanafanya ushetani wote. Fikiria mtu anatengeneza kundi la utekaji, limteke na kumpiga mgombea wa upinzani, anatangazwa amepita bila kupingwa, halafu bila aibu anaenda kanisani au msikitini, analazimisha apate nafasi ya kusimama madhabahuni, na kujifanya anahubiri upendo.

Uovu aliomtendea mgombea mwenzake anaona hautoshi, anathubutu kwenda kuinajisi madhabahu ya Mungu!! Hawa wanaenda kuchota laana yao na vizazi vyao. Mbaya zaidi hawa ndio wanaotuongoza, halafu tunatarajia nchi ipate maendeleo!!

Tanzania hatua ya kwanza ya maendeleo itapatikana siku CCM itakapokuwa imeondolewa, na watu wakajitenga na uovu wa CCM.
 
ukitazama upinzani katika ujumala wake,
unaona sura za chuki, tamaa ya mali, vyeo na madaraka, ubinafsi ulopindukia, uchu usiomithilika, uadui wa waziwazi, kutokuaminiana na kuogopana kuliko dhahiri kabisa na kwakweli mpasuko na mgawanyiko mithili ya ghaza na ukingo wa magharibi,
ambao huoni wala hakuna matumaini siku moja wanaweza kua na mtazama moja angalau, jamii ya wengi Tanzania ikawa na tumaini jipya.

kilicho dhahiri, ni kwamba upinzani unajitahidi kwa bidii sana kujigawanya na kutengeneza nafasi na uhakika usio na shaka kwa ccm kushinda na kutawala milele.....
 
Mimi nilishachora mstari nikiona unashabikia ccm nakaa na wewe kwa machale sana.
 
Chama Cha Mapinduzi
 
Hii haitoshi mkuu, toa mifano halisi ya viongozi wa upinzani ambao wamejaa chuki , ubinafsi na tamaa ya madaraka. Otherwise, hii naichukulia kama juhudi za kukatisha tamaa. Kuna Wewe unaaamini ccm itatawala milele. W. Well, trust me, hakuna chama Cha siasa kilichodumu milele katika historia ya Dunia mpaka Sasa. Kwa tamaa ya madaraka, wizi na ufisadi ulioko ndani ya ccm, mwisho wake uko humohumo.. Yaani ndani ya wizi na ufisadi na tamaa ya Mali na madaraka ndimo lilimo anguko la ccm. CCM is engineering its own downfall.
 
Mc
Umetuacha solemba ,stori zawale watu wanaopewa majina ya vitongoji au mitaa zimeishia wapi mkuu
dah nitarudi mzee ngoja kwanza ni solve hii financial crisis... Sema mods kwa kubadilisha title za threads wanazingua
 
yaani umekaa mahala na matumaini kabisa mtu mzima mwenye akili timamu kwamba Lipumba atakaa meza moja na Mbowe, wakubaliane na zito kabwe, Joseph Selasini aseme ndio Mzee, kisha Hashimu Rungwe Sipunda aunge mkono halafu, John Momose Cheyo akubali, huku John Shibuda sauti ya wakulima afurahie Dr slaa, mwambukusi lazma watasema wapuuzi nyie vibaraka wa CCM msinitumbue......

baadae cck, Umoja Party, DP, DA, SAU na kile cha dovutwa na vingine vingi ambavyo havipendi maigizo na mazingeumbwe, vitajikalia zao kando...

na halafu taratibu bila maringo wala tashwishwi yeyote vinajipanga nyuma ya CCM pasina shaka.........
 
Unalinganisha na nini?
 
Sina matumaini hayo, Wala siamini kama wapinzani wakiungana ndipo wataing'oa CCM... Kuna chama kimoja kitaiondoa ccm madarakani, iwe 2025 au miakaa mingi ijayo. It will happen. Kuamini ccm itakaa madarakani milele ni kujilisha upepo TU.
 
Sina matumaini hayo, Wala siamini kama wapinzani wakiungana ndipo wataing'oa CCM... Kuna chama kimoja kitaiondoa ccm madarakani, iwe 2025 au miakaa mingi ijayo. It will happen. Kuamini ccm itakaa madarakani milele ni kujilisha upepo TU.
kwa mgawanyiko uliopo upinzani?
Thubutu, hawa CCM hata wavurunde namna gani hakuna kachama eti kamoja kaling'oe hilo jabali la chama Tanzania.

Nnnnnneverrr nakwambia nnnnnneverrr........
 
Naam naam
Chama kiovu kinacholindwa na serikali dhaifu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…