CCM ya Dr. Mwl. Nyerere sio ccm ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ya Dr. Mwl. Nyerere sio ccm ya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Sep 1, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Katika harakati zangu za kuwahamasisha watu kuchagua kwa busara katika uchaguzi ujao, nilikuwa naongea na mkazi mmoja wa Dar kuhusu suala hilo. Nilimueleza umuhimu wa kutochagua chama kinachoongozwa na mafisadi wa nchi yetu. Aliniambia kuwa, pamoja na ufisadi huo, chama hicho kina asili ya Nyerere kwa hiyo kina mvuto kwake. Ilibidi nitumie kama nusu saa hivi kumuelimisha kuwa CCM ya Nyerere sio ccm ya leo. Mwalimu alikuwa anapigania maendeleo ya Watanzania wote, wakati ccm ya sasa inakumbatia ufisadi na kulimbikiza mali kwa njia ya wizi kwa watu wachache.

  Ni muhimu watu watambue kuwa itikadi ya Nyerere imefutwa katika chama hicho, bali wanatumia jina lake tu kujitajirisha kupitia migongo ya Watanzania. Mwalimu angefufuka leo na kuona mambo yanavyoendelea, nina hakika angefoka sana na kuwatia jela wote wanaohusika na kuchafua jina lake.
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Dingswayo,
  Nakuunga mkono kwa asilimia mia kwa maneno yako. Juzi nilishuhudia mjadala mkali kwenye daladala ambapo kijana mmoja alianza kwa kusema kwamba Nyerere ndiye aliyeleta shida zote hizi. Walizuka watu wa makamo na kijana mmoja waliokuwa wanaijua vilivyo historia ya TANU na ujio wa CCM ya Nyerere wakatetea kwa nguvu zao zote kwamba kinachotokea hivi sasa wala hakihusiani kabisa na msimamo wa Nyerere alipounganisha ASP na TANU na kuzaliwa CCM. Kinachoendelea sasa hivi kwenye CCM ni uhuni, usanii na ukiukwaji mkubwa wa misingi mizuri iliyokuwepo huko nyuma wakati wa Mwalimu iliyosimamia haki za wanachama wote bila kujali uwezo wa kifedha wa mtu na haki za wananchi wote kwa ujumla ambao waliweza kwenda kupiga kura kwa uhuru bila vishawishi vyovyote vya kupewa pesa ama vitu.

  Nakubaliana nawe kabisa kwamba Mwalimu angelifufuka leo sijui hawa viongozi wangelimwambia nini kuhusu kukiharibu kabisa Chama kilichokuwa safi na ambacho hakikuwahi hata mara moja kutumia pesa kwa ajili ya kununua kura za wananchi.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Tatizo lingine la watanzania ni Kuukumbuka wosia wa Mwalimu.
  Nanukuu
  Watanznia wamekariri hawjui kuwa CCM alikyokuwa anaizungumzia mwalimu sio CCM hii ya leo.
   
 4. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Nina uhakika kama leo mwalimu angekuwepo ( Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) nina imani angempigia Dr. Slaa kampeni. Kuna muda nakumbuka aliwahi hata kusema "CCM si baba yangu wala siyo mama yangu" kuna mambo walimuudhi na walishaanza kumuudhi hata kipindi hicho cha uhai wake. ndiyo hawa hawa ccm ambao wanadhani watabakia madarakani milele kwani wana haki miliki ya nchi hii na vilivyomo ndani yake.

  Siyo CCM aliyoienzi baba wa taifa tarehe 5/2/1977, hii ccm imebaki ya wafanyabiashara na wababaishaji wengi tu, mtu akikwambia utaje watu 10 tu ndani ya CCM ambao ni wasafi na wanafuata miiko yote ya uongozi na ile ya uanachama wa ccm, sidhani kama utawapa kwa urahisi. sana sana wapo 4 tu naojua mimi.

  Ni kweli baadhi ya ndugu zetu wanaona kuitosa ccm ni sawa na kumsaliti muasisi wake, lakini pole pole tunawaeleza watatuelewa tu kabla ya 31st of October. mungu anasikiliza vilio hivi vya watanzania wengi kun akitu lazima kinatokea this year na kitashangaza tulio wengi.
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwanza nimependa hicho kichwa cha habari: CCM ya Dr. Mwl. Nyerere sio ccm ya Kikwete

  Kabisa huwa hata mie naomba kama MUNGU anaweza fufua watu basi amfufue Mwl. Nyerere japo kwa miezi kadhaa asafishe huo utumbo uliokuwapo katita CCM ya DR.KIKWETE!! :mad2::mad2: maana yale maadili ya chama yaliokuwapo enzi zile sasa hayapo tena ukifikiria kwa kina unaweza tokwa na machozi. Huwa najiuliza ingekuwa Mwl.Nyerere ni mbinafsi kama hawa wanaccm waliopo hii nchi ingekuwa wapi but Mwl. alikuwa mpenda maendeleo alitaka watu wote wafanane wenye nacho na wasio nacho na hata kama unacho lazima uchunguzwe je! hivyo ulivyonavyo ni vya halali ama mazinga ombwe.
  Muhujumu uchumi alikuwa anashughulikiwa kisawasawa bila kujali sura wala rangi lakini sasa hivi wahujumu uchumi (mafisadi) wanashungulikiwa kimazingaombwe. Nakumbuka hata kile kipindi cha RTD - MIKINGAMO (MIKINGAMO TUAMBIE NANI YUKO WAPI NA ANAFANYA NINI......nakingora kinalia kweli hakuna kulala hadi kieleweke
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Ndio maana anapenda aitwe jk wakati yeye anatakiwa aitwe jm kwani hawezi hata kujaribu kuvaa viatu vya yule mheshimiwa ambaye hakutaka aitwe mheshimiwa bali alitaka aitwe mwalimu...................mshauri kikwete aitwe mwalimu..weeeee thubutu kanavyopenda sifa....
  Hakika tuna rais dhaifu lakini aliye nadhifu wa sura...
   
 7. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Hakika CCM ya Mwalimu siyo ccm ya jk. Nakumbuka miiko ya viongozi, Azimio la Arusha, Mwongozo wa TANU, ambavyo vilianzishwa na TANU na kurithiwa baada ya CCM kuzaliwa. Tujiulize vyote hivyo viko wapi leo hii. Tulikuwa hatuingii darasani asubuhi bila kurecite ahadi za TANU. Kati ya ahadi hizo zilikuwepo "rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa." "Cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu." Hizi ahadi zilikuwa zinatupa mwelekeo wa Tanzania tuliyodhamiria kuijenga. Mwalimu ameondoka ametuacha wakiwa, na wajanja wakayapindua mazuri yote hayo. Mwalimu tunakukumbuka, Mungu Akulaze mahali pema. Ulitujali watanzania. Ni wajibu wetu kuyarudisha yote mazuri uliyotuanzishia Mwalimu. Tuirudishe Tanzania mikononi mwa watanzania wenyewe, wanaojali vizazi vijavyo. Kwa kuwa ccm imeshindwa ni wakati wa kutafuta chama kitakachoweza kuyafanya hayo kituongoze.

  Mungu Ibariki Tanzania!!!
   
Loading...