CCM wavuruga kampeni za CHADEMA !!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wavuruga kampeni za CHADEMA !!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by minda, Sep 28, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Monday, 27 September 2010 04:11
  Na Mohamed Hamad, Kiteto MANYARA.
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  MKUTANO wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Bwagamoyo Msikitini Wilaya ya Kiteto juzi uliingia dosari baada ya kuvamiwa na Wanachama wa CCM na kusabasha vurugu kubwa.

  Wakati mkutano wa CHADEMA wa kuwanadi wagombea wa ngazi ya Ubunge na Udiwani ukiendelea, ghafla waliibuka vijana wawili wakiwa wamevalia sare za CCM huku wakiendesha pikipiki kwa fujo, tendo ambalo lilisababisha kutosikilizana katika eneo hilo.

  Baada ya wanachama hao wa CCM waliotambulika kwa majina ya Juma Shabani, na Farida Omari ambao ni wakazi wa kata hiyo, kufanya fujo kwa muda, vijana wa CHADEMA waliokuwa katika eneo hilo waliwafuata na kuwataka kusitisha fujo zao, jambo ambalo lilizua mabishano na kuongeza ghasia.

  CHADEMA walipoona vijana hao hawataki kutoka kwa utaratibu wa kuambiwa kundi la vijana wao liliwafata wanachama hao wa CCM na kujaribu kuwatoa kwa nguvu huku wakiwatishia kuwapiga hali ambayo ilifanya askari wa usalama waliokuwa eneo hilo kuingilia kati.


  Wakiongea na Majira baadhi ya mashuhuda walisema Vijana hao wa CCM ambao walitaka kupigwa kabla ya kuokolewa na polisi, awali walionekana maeneo hayo ya mkutano wa CHAMDEMA wakiwa na sare za CCM wakiwa kama wasikilizaji tu, lakini baada ya muda mfupi walianzisha zogo kwa kupinga kauli za wagombea wakidai kuwa wanadanganya watu.


  Kutokana na hali hiyo mgombea udiwani wa CHADEMA kata ya Kibaya Bw. Ramadhani Mwamba alisimama na kuanza kuwasihi vijana hao kuondoka eneo hilo huku akikumbushia jinsi ambavyo vyama vilisaini makubaliano ya kutoingiliana katika kampeni na kuzingatia maadili.

  “Ndugu zangu wananchi, vyama vya siasa vilisaini kijitabu hiki cha maadili ili kusiwe na mwingiliano wa kisiasa katika kupiga kampeni zetu, sasa hapa kuna hawa wenzetu wamekuja wakiwa wamevalia sare zao, sheria inakataza lakini wamekaidi ni wazi wanataka kutuchokoza ili tuonekane chama kinachopenda fujo" alisema.

  Alisema CHADEMA si chama cha fujo lakini kamwe hakiwezi kukaa tu na kuvumilia fujo za namna hiyo, kwa kuwa matukio ya namna hiyo yakiachiwa yaendelee yanaweza kuleeta usumbufu wakati mwingine na pengine nchi nzima.

  Kauli ya diwani huyo ilisababisha vijana wa CHADEMA kuchukua jukumu la kujaribu kuwatoa wanachama hao kwa nguvu, na hatimaye kuibua fujo zaidi mpaka walipokuja polisi na kuwaokoa wanaCCM hao mikononi mwa wana CHADEMA wenye hasira.

  Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilayani Kiteto Bw. Athumani Kidawa alisema pamoja na kuchukizwa na vitendo vya CCM, lakini pia hawakuridhishwa na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wanachama hao kwa kuwa polisi waliwaachia wakaedna zao.

  “Ingekuwa ni kijana wa CHADEMA hapa angefunguliwa mashitaka kama ilivyotokea kule Kiperesa alikofunguliwa mashitaka kijana wa CUF Alli Juma Kibwana, kwa kudaiwa amefungulia redio na kusababisha usumbufu kwa mgombea wa CCM Habibu Kiberenge akinadi sera zake., natarajia kutoa malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi juu ya ulinzi hafifu tunaopatiwa" alisema.

  Mwisho.

  Source: Majira
   
 2. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa taarifa.
   
Loading...