CCM waumbuka Mwanza

CCM waumbuka Mwanza

Hongereni sana, habari njema hiyo.. Wafanyeni kitu mbaya October
 
Leo tarehe 30/06/2015 katika mahakama ya Wilaya kulikuwa na hukumu ya kesi zilizofunguliwa mahakamani na CCM za kupinga matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika 14 Disemba 2015 ambapo CCM waliangukia pua,leo WAMEUMBUKA ile mbaya baada ya mahakama KUTUPILIA mbali kesi hizo na kuwafanya wenyeviti wa CHADEMA kutangazwa kuwa washindi halali.

Mbaya zaidi ni pale ambapo hata ile mitaa ambayo wao (CCM) walishinda KIBABE nayo matokeo yake yametenguliwa!

Pole sana ambao hamjajitambua na kutambua kuwa CCM mwisho wao umefika! Muda huu sisi tuliojitambua kwa kuchagua CHADEMA katika mtaa wetu wa KILELENI kata ya KITANGIRI tupo tunagonga moja baridi,moja moto na nyama choma tukisherehekea ushindi!

Katika mkoa wa Kagera hasa Wilaya za Karagwe na Kyerwa Mahakama imegeuka mwiba mchungu kwa CCM.Kesi zilizofunguliwa na WANA UKAWA wakiongozwa na CHADEMA kupinga matokeo na mapingamizi zimetenguliwa na sehemu kubwa ya uongozi wa Serikali za mitaa zipo wazi.Jambo ili litakuwa na athari kubwa kwenye maendeleo ukizingatia kuwa hawa viongozi nido muhimili wa maendeleo katika ngazi za mitaa.CCM ubishi wao na kuwatumia Wakurugenzi mitaa haitawaliki sasa.
 
Hahaaaa haki hucheleweshwagwa tu. Ccm tuachieni nchi yetuuu
 
Back
Top Bottom