CCM watishia Kuuwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM watishia Kuuwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masanilo, Sep 12, 2010.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Atishiwa kuuawa kwa kutoinadi CCM Moshi Mjini

  Mgombea aliyeshinda kura za maoni katika jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kisha kuenguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya chama hicho, ametishiwa kuuawa. Athuman Ramole (pichani) maarufu kama Buni, ametishiwa kifo pamoja na kuhujumiwa katika biashara zake na watu wasiofahamika. Taarifa zinadai kuwa vitisho hivyo vinatolewa kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kutoshiriki mikutano ya kampeni ya kumnadi mgombea aliyepitishwa na Nec kuwania ubunge wa jimbo hilo, Justine Salakana.
  Akizungumzia vitisho hivyo jana, Ramole alisema kwa muda mrefu hakuwepo nchini kutokana na majukumu yake ya kibiashara na kwamba alirejea Septemba 9, mwaka huu. Alidai kuwa baada ya kurejea mjini hapa, watu walio karibu naye (hakuwataja majina) walimfikishia taarifa za kufanyika kwa kikao kilichomjadili na kufikia uamuzi wa kumuua na kuhujumu biashara zake. Kada huyo wa CCM ameshatoa taarifa Kituo cha Kati cha Polisi mjini Moshi na kufungua jalada lenye namba MOSH/RB/12212/2010 la Septemba 10, mwaka huu.
  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lucas Ng’hoboko, alithibitisha kupokea taarifa ya kufunguliwa kwa jalada hilo na kusema polisi inaendelea na uchunguzi.
  “Tumepokea taarifa za kutishiwa kuuawa ambazo anadai kaelezwa na wasiri wake, tunazifanyia kazi kwa umakini mkubwa, maana kipindi hiki cha kampeni ni kigumu,” alisema.
  Ng’hoboko alisema baadhi ya tuhuma zinazotolewa kipindi hiki zinaweza kuwa na ukweli ama mbinu za kisiasa.
  “Tunachunguza kwa makini, polisi tunalaumiwa kuwa tunatumiwa na wanasiasa, ila wajibu wa polisi ni kupeleleza taarifa zozote tunazoletewa,”alisema.
  Ramole alisema anawashangaa watu wanaokutana kwenye kikao na kupanga njama hizo kwa madai kuwa hamuungi mkono Salakana.
  Alisema dhamira yake ni kuona CCM inashindwa kiti cha ubunge Moshi Mjini kama na kwamba alishayakubali na kuyatambua maamuzi ya Nec.
  Lakini alidai kwamba kuna baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya mkoa na wilaya, waliomtumia taarifa za kumlazimisha apande jukwaani na kumnadi Salakana.
  “Nawaomba waache vitisho juu yangu, nimeshaenguliwa na nimeridhika, kwa sasa ni mwanachama wa kawaida, wasiniite kwa vitisho kwenye vikao vyao vya ushindi jimbo la Moshi Mjini,” alisema.
  Alisema ingawa ana nia ya kushiriki kampeni hizo, lakini hayupo tayari kujihusisha na masuala ya ndani kwa kuhofia kupakwa matope ikiwa siri za mikakati ya CCM zitavuja.
  Ramole alisema kuna kikundi cha majungu katika jimbo hilo,ambacho kimekuwa kikipeleka maneno kwenye Kamati Kuu ya CCM kwa lengo la kuwachafua wanachama wengine. NIPASHE iliwasiliana na Katibu wa CCM mkoani hapa, Steven Kazidi, ambaye alisema hajapata taarifa hizo. Kazidi ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi ndani ya CCM mkoani hapa, alisema suala la Ramole kutopanda jukwaani kumnadi Salakana, hana uhakika nalo kwa kuwa hajashiriki kwenye mikutano yote ya kampeniya CCM jimbo la Moshi Mjini. Katika kura za maoni zilizofanyika katika jimbo hilo, Ramole aliibukana ushindi wa kura 1,554, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Kilimanjaro,Thomas Ngawaiya (1,539) na Salakana (1,152).
  Jimbo hilo limekuwa gumzo ndani ya CCM kuanzia ngazi yaTaifa, mkoa na wilaya kutokana na kushikiliwa na upinzani kwa vipindi vitatu, ambapo kwa sasa CCM imeweka nguvu kubwa kupata ushindi.

  NB

  Ramole karibu upinzani, utapatiwa ulinzi na kwenye demokrasia ya ukweli. CCM ni Magaidi
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Siasa za kibabe hizi! kwanini wafanye haya sisi watanzania tuwaelewe vipi?
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,066
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  Ndesapesa amesema Chadema watashinda 6 kati ya Majimbo 9 yaliyomo Kilimanjaro so hata waue haitasaidia wananchi ndo waamuzi wa mwisho na hawadanganyiki!!!!
   
 4. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,550
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Naamu wameshashindwa katika jimbo la Moshi sasa wanatafuta mchawi
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hahaaaaaaa chichi emu bana
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  CCM wananuka damu,

  CCM ni chama cha damu
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hebu fikiria Tanzania bila raisi mwenye Kifafa na wabunge wa CCM
   
 8. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu kweli mavi yanagonga vyupi....
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Wataua kweli oooh, si mafisadi hawa?
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280

  Sisiemu ina wenyewe. Ramole waachie wenye nayo.
   
Loading...