Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Ninashangazwa sana kuona jinsi CCM imeteka nyara sikukuu nyeti ya wafanyakazi na kugeuzwa ni mradi kamambe wa kumnadi mgombea wao wa URAISI 2020.
Matatizo ya wafanyakazi yalipaswa yaongelewe na viongozi wa kitaifa wa wafanyakazi lakini Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kalipa mamlaka ya kumpigia debe la nguvu mgombea Urais wa CCM 2020 huku wenye sherehe yao kupitia wawakilishi wao kuishia kupewa dakika tano zikiwa ni hata pungufu za muda ambao wasanii mbali mbali walizopewa kutumbuiza!
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro katumia zaidi ya nusu saa kuzungumzia mafanikio na matatizo ya mkoa wake huku akimpigia debe bosi wake ili asimtumbue.
Maswali ya kujiuliza hii sherehe ni kusherehekea CCM au MEI MOSI?
Hivi Mkuu wa Mkoa ambaye anadaiwa siyo mtumishi wa umma ana uhalali gani wa kuwa msemaji mkuu wa wafanyakazi na wala siyo mtumishi bali mwanasiasa.
Vyama vya wafanyakazi kweli vinaongozwa na wachovu na hata wanachama wao wachovu wanaporuhusu kero zao kuwekwa pembezoni na CCM kutumia nafasi yao kukemea mikutano na maandamano ya kudai haki.
Hata Mgeni rasmi siyo lazima awe Rais kama anajipa nafasi ya kuteka nyara ajenda za wafanyakazi.
Hata huyo, Mcee Muungano wa vyama vya wafanyakazi ujipime kama wameamua kuwa mawakala wa CCM wajue mgongano huo wa masilahi unatosha kuwatumbua.
MEI MOSI NI SIKU YA KUTAFAKARI KERO ZA WAFANYAKAZI SIYO MWANYA WA KUMPIGIA DEBE MGOMBEA URAIS WA CCM WA 2020.