CCM wasitegemee sana kura za vijijini uchaguzi wa keshokutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wasitegemee sana kura za vijijini uchaguzi wa keshokutwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by p53, Oct 29, 2010.

 1. p

  p53 JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ebwana uchaguzi wa mwaka huu ni noma.Siamini mazee.nimetoka kuongea na mjomba angu sasa hivi shamba.Huyu mzee ni ccm damu miaka yote.Pamoja na mambo mengine,nilimuuliza kesho kutwa kura yake ya urais atampa nani?Mzee akasema yeye na shangazi yangu(mkewe) na binamu zangu(watoto zake) kura zao ni kwa Slaa.Sikuamini.Akasema mbunge atampa wa ccm,manake walikuwa wanamtaka siku nyingi na walikuwa wanampitisha kwenye kura za maoni lakini jina lilikuwa halirudi,badala yake walikuwa wanaletewa jina lilelile la mgombea wasiyemtaka,lakini mwaka huu huyu mgombea kapigwa chini,wameletewa wanayemtaka.
  Nikamuuliza kwanini hatamchagua JK ambaye alimkubali sana mwaka 2005?Jibu alilonipa siwezi kuliweka hapa.Nikajaribu kumshawishi nione msimamo wake kama hatayumba,akanikatisha tamaa tu kwamba nisiendelee kumshawishi manake nitapoteza bure tu muda wangu.
  Wakuu,mimi nawaombea uchaguzi mwema huko nyumbani.Eee Mungu waongoze wenye mamlaka ya kutenda haki waifanye haki manake kama wapiga kura wenyewe tegemeo la ccm ndiyo wanafikiria hivi,basi mwaka huu kunaweza kuchimbika huko Tanzania.
   
Loading...