CCM wapiga marufuku mijadala ya katiba mpya

CCM wapiga marufuku mijadala ya katiba mpya

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,995
Reaction score
25,392
Kuna taarifa za chini chini kwamba serikali ya CCM imeuagiza uongozi wa TBC kusitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni Dodoma ili kuwanyima fursa wananchi kufuatilia mjadala wa utunzi wa katiba utakaoanza ngwe ya pili kesho Jumanne. Lengo kubwa ni kuwafanya wananchi wasijue kinachoendelea ndani ya ukumbi wa bunge. Imeazimiwa kwamba TBC Taifa (RTD) warekodi kipindi hicho na kukihariri kwa kadri watakavyoona inafaa na kisha kukirusha kupitia redioni saa 4 usiku.

Aidha wamekipiga marufuku kituo cha Star TV kurusha mjadala huo moja kwa moja kama walivyokuwa wakifanya katika ngwe ya kwanza. Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi Rehema Nchimbi na wakuu wengine wa mikoa wameagizwa kuwazuia watu kujadili katiba hiyo katika mji wa Dodoma na mikoa mingine kwa kisingizio cha ‘kuwavuruga' wajumbe watakaoukuwa wakijadiliana bungeni. Baadhi ya vyombo vya habari, hasa vya binafsi, vimepigwa marufuku kusogelea ukumbi wa bunge wakati mijadala itakapokuwa ikiendelea. Wameelekezwa wasubiri mjadala ukiisha watakuwa wanapewa taarifa na katibu wa bunge mara moja kwa kila siku.

Ndugu zangu, huu ni udikteta. Naona sasa CCM inakaribia kabisa kuiingiza nchi hii katika machafuko. TBC inaendeshwa kwa kodi za umma. Sasa iweje wananchi wazuiwe kupata habari na kufuatilia michango ya utunzi wa katiba mpya? Hili jambo halikubaliki hata kidogo. Kama CCM wameamua kuwanyanyasa wananchi namna hii, nchi hii sasa itakuwa imegeuza kuwa ya kidikteta.

:israel:
 
Unategemea nini kutoka Serikali dhalimu iliyojaa wahuni ? wamejiona hawana hoja sasa ni kauli za kibabe tu huku wakiwa wamejificha mgongoni mwa vyombo vya dola. Hii ni katiba ya Watanzania kwanini wanachojadili kifanywe siri? Wanajua watafanya madudu ambayo Watanzania tukiyaona live kamwe hatuwezi kukubali uhuni na uharamia wao. Sasa ndio wameamua kufanya kila kitu nyuma ya pazia huku wakilipana mabiioni ya posho kutoka kwenye pesa za walipa kodi. Wafanye tu walitakalo lakini pesa za walipa kodi wasiziguse. Kuendelea kulipana shilingi laki tatu kwa siku huku wakijua fika kwamba wanachokifanya hakitakubalika na Watanzania walio wengi ni ufisadi na wizi wa mchana kweupe.
 
Mkuu tpaul,

Kwangu mimi,nadhani huu ni ukweli kabisa,ni suala la muda tu,maana mambo yanayofanywa na CCM kwa sasa ni kama wamechanganyikiwa, au sijui laana ya yule kiongozi wa dhehebu fulani la dini nchini imewafikia?..

La pili,ilikuweka rekodi sawia,Mkuu wa mkoa wa Dodoma ni Dr.Rehema Nchimbi,huyo bi Mwasha ni wa Tabora

Asante.
 
Asante kwa kunikumbusha mkuu Masakata . Naona sasa CCM wameamua kujikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Dhambi ya unafiki na dharau kwa wananchi inawaandama na dhambi hii haitawaacha salama 2015.
 
Last edited by a moderator:
Information is Power! When you have information, you have everythng! Sasa kama wanatumia tena mbinu hiyo, tunakoelekea siko sasa!!
 
kwahiyo wanafanya hayo yote wakitegemea jeshi la polisi sio,tusubili tuone hii nchi ya ccm au yawatanganyika.
 
Kuna taarifa za chini chini kwamba serikali ya CCM imeuagiza uongozi wa TBC kusitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni Dodoma ili kuwanyima fursa wananchi kufuatilia mjadala wa utunzi wa katiba utakaoanza ngwe ya pili kesho Jumanne. Lengo kubwa ni kuwafanya wananchi wasijue kinachoendelea ndani ya ukumbi wa bunge. Imeazimiwa kwamba TBC Taifa (RTD) warekodi kipindi hicho na kukihariri kwa kadri watakavyoona inafaa na kisha kukirusha kupitia redioni saa 4 usiku.

Aidha wamekipiga marufuku kituo cha Stat TV kurusha mjadala huo moja kwa moja kama walivyokuwa wakifanya katika ngwe ya kwanza. Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi Rehema Nchimbi na wakuu wengine wa mikoa wameagizwa kuwazuia watu kujadili katiba hiyo katika mji wa Dodoma na mikoa mingine kwa kisingizio cha ‘kuwavuruga’ wajumbe watakaoukuwa wakijadiliana bungeni. Baadhi ya vyombo vya habari, hasa vya binafsi, vimepigwa marufuku kusogelea ukumbi wa bunge wakati mijadala itakapokuwa ikiendelea. Wameelekezwa wasubiri mjadala ukiisha watakuwa wanapewa taarifa na katibu wa bunge mara moja kwa kila siku.

Ndugu zangu, huu ni udikteta. Naona sasa CCM inakaribia kabisa kuiingiza nchi hii katika machafuko. TBC inaendeshwa kwa kodi za umma. Sasa iweje wananchi wazuiwe kupata habari na kufuatilia michango ya utunzi wa katiba mpya? Hili jambo halikubaliki hata kidogo. Kama kuna mtu mwenye taarifa kamili juu ya hujuma hizi naomba atujuze. Kama ni kweli CCM wameamua kuwanyanyasa wananchi namna hii, nchi hii sasa itakuwa imegeuza kuwa ya kidikteta.

:israel:

Taarifa haina chanzo watu wanaijadili kama ni kweli!!
 
Taarifa haina chanzo watu wanaijadili kama ni kweli!!

chanzo ni ITV na documents za siri zimesambazwa kwa wakuu wa mikoa zikiwataka kuwatumia polisi kutawanya watu watakaonekana wakiwa kwenye makundi wakiijadili katiba mpya!
 
Sawa hili ni zoezi zuri tupate katiba yetu nzuri ukawa wasituharibie nchi.
 
Mkuu tpaul,

Kwangu mimi,nadhani huu ni ukweli kabisa,ni suala la muda tu,maana mambo yanayofanywa na CCM kwa sasa ni kama wamechanganyikiwa, au sijui laana ya yule kiongozi wa dhehebu fulani la dini nchini imewafikia?..

La pili,ilikuweka rekodi sawia,Mkuu wa mkoa wa Dodoma ni Dr.Rehema Nchimbi,huyo bi Mwasha ni wa Tabora

Asante.

siyo kama wamechanfanyikiwa ni wamechanfanyikiwa...
 
Unategemea nini kutoka Serikali dhalimu iliyojaa wahuni ? wamejiona hawana hoja sasa ni kauli za kibabe tu huku wakiwa wamejificha mgongoni mwa vyombo vya dola. Hii ni katiba ya Watanzania kwanini wanachojadili kifanywe siri? Wanajua watafanya madudu ambayo Watanzania tukiyaona live kamwe hatuwezi kukubali uhuni na uharamia wao. Sasa ndio wameamua kufanya kila kitu nyuma ya pazia huku wakilipana mabiioni ya posho kutoka kwenye pesa za walipa kodi. Wafanye tu walitakalo lakini pesa za walipa kodi wasiziguse. Kuendelea kulipana shilingi laki tatu kwa siku huku wakijua fika kwamba wanachokifanya hakitakubalika na Watanzania walio wengi ni ufisadi na wizi wa mchana kweupe.

Wamelewa madaraka kila kukicha wanaibuka na vituko lukuki,kazi yao ni kuhakikisha wanaendelea kutawala huku wakiacha mambo ya msingi kama madawa ya kulevya vikishamili nchini.
 
Attachments

  • 1407209532726.jpg
    1407209532726.jpg
    79.1 KB · Views: 192
Sawa hili ni zoezi zuri tupate katiba yetu nzuri ukawa wasituharibie nchi.

Kweli? Una uhakika na ukisemacho au ni ushabiki usio na tija?

Information is power, katiba sio ya UKAWA wala TZ KWANZA, ni kwa ajili ya waTanzania, tunataka kujua na kufuatilia mchakato mzima, wewe unaleta habari za siasa? Aah!!
 
Nilishawai andika huko nyuma ccm wako tayari kuliongoza taifa ili kijeshi. wako tayari kupitisha katiba ovu...itakayolinda maslai yao kwa gharama zozote na wako tayari kufanya uchaguzi 2015 kibabe. Ni sisi kujipanga wasiyafanye wayapendayo wao.
 
Tbccm chombo cha propaganda chafu za ccm. Utatoaje taarifa ya Lukuvi kuwa ukawa hawana sababu za kutokuwa bmk?

By the way. ..JK yuko USA kwa siku 9, ya Tanzania amemwachia nani?
 
Kama nikweli, basi vita vitaanza mwaka huu huu na sio mwakani tena.
 
Taarifa haina chanzo watu wanaijadili kama ni kweli!!

Kauli ya Nyerere kwa sasa haina mashiko, kama great thinker you have to understand that "NO SITUATION IS PERMANENT" unless you are not one(great thinker).
 
Back
Top Bottom