CCM wapiga marufuku mijadala ya katiba mpya

CCM wapiga marufuku mijadala ya katiba mpya

Sawa hili ni zoezi zuri tupate katiba yetu nzuri ukawa wasituharibie nchi.
Mkuu usilewe madaraka na chenji maiti unazopata kutoka kwa hao waadhalimu waliotunyonya zaidi ya miaka hamsini sasa.Wengine tunachangia hapa tukiwa sio wanachama wa chama chochote cha siasa.
Lakini uhuni na upumbavu ambao serikali inataka kutuletea kwenye mustakabali wa maisha yetu na ya vizazi vijavyo hautavumilika kamwe.
Ieleweke nchi hii ni ya wananchi wote na si ya CCM wala vyombo vya dola pekee.Kuwanyima wananchi uhuru wa kudiscuss na kufwatilia mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia chombo cha Umma kama TBC ni kinyume na haki za binadamu,na Tanzania ndio itakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo duniani kote.
Amka ewe Mtanzania Mwenzangu.
 
Sawa hili ni zoezi zuri tupate katiba yetu nzuri ukawa wasituharibie nchi.

kwani umeambiwa CCM hawana katiba nzuri hadi watake kubadilisha katiba ya wananchi kuwa ya CCM? acheni kujitoa akili, mkuu.
 
Wana wazimu!! Tutakula nao sahani moja kwani wengi wao tuna account zao za social media, namba za simu nk nk, labda waende kuzimu tu; tunao sambamba. tutatumia BBC na sauti ya ujerumani na VOA, magazeti ya ndani na nje ya nchi, makanisa na mpaka vikao vya harusi na mazishi kutoa maoni yetu na watayasikia hata wakiyapuuza ujumbe utakuwa umefika na hilo ndilo tunalotafuta na kwa kitendo cha kutaka kufanya black out ni kwa sababu ujumbe umefika na wanaugwaya!
BMK ni batili no matter the outcome; katiba ya CCM haitakuwa endelevu na haina uhalali katika jamii nzima ya Kitanzania, wakishamaliza kazi tutaanza upya kudai Katiba mpya na bora mpaka kieleweke; Aluta continua

Komandoo Salimin Amour aliwahi kuyafungia magazeti fulani ya huku bara; alipoambiwa yanasomeka online je atafanyaje kuhusu Inernet! akajibu; Hapo chacha!! hiyo itakuwa ngumu.
CCM hii ni karne ya 21, ya sayansi na tekelinalokujia, Serikali 3 hazikwepeki mnazichelewesha tu na ujumbe huo wataendelea kuupata.

bora mtu -------- anayejitambua kwamba hajui kuliko mtu mjinga asiyejua kwamba hajui!
 
Back
Top Bottom