CCM waongeze polisi haraka sana

Acha Uvivu

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
525
131
Hali inayoendelea hivi sasa katika nchi hii siyo ya kawaida. Mwenye akili tu ndiye anaweza kuona mbali lakini sio sisi ccm tunaojitahidi tu kulinda maslahi yetu bila kuwajali wananchi.

Pamoja na mambo mengi ambayo wakati wowote yataamsha hasira za wananchi-hali ngumu ya maisha, kusua sua kwa mchakato wa katiba mpya-hamna jinsi kukwepa kwamba jeshi la polisi tulionao ambao pia wanalia hali ngumu ya maisha hawawezi kudhibiti hasira za wananchi. Ushahidi upo kwamba maandamano yanapokuwa Arusha polisi huletwa toka maeneo ya jirani: Manyara, Kilimanjaro n.k

Sasa iwapo Manyara, Kilimanjaro na kwengineko utawaka moto, wapi watatoka polisi wa kuongeza nguvu? Kuwafunza wengine zaidi, bajeti ya mishahara mipya kwao hamna. Nchi inafilisika na watoa misaada Europe wameshachoka tayari.

CCM tutashindwa kupeleka vibakuli. CCM tufanyeje ili kukwepa hili tishio, ushoga tumeukataa hatuwezi kuhongwa na vitambi vyetu na vyeti feki tulivonavyo vinategemea siasa tu na hatuwezi kuomba kazi za kitaaluma.
 
kuna article fulani iliwekwa mara tatu jana na kila ikiwekwa mods walikua wanaiondoa.
 
Wao wanafikiri vuguvugu la mageuzi na kudai haki linaweza kuzimwa kwa kuwambambikizia kesi na kuwafunga kina Lema, never. Mfungeni Lema, Dr. Slaa, Mbowe, Lissu, Ndesamboro na wengineo.

Lakini vuguvugu la mapinduzi ndio kwanza limepamba moto na limeshaingia masikioni mwa wananchi, in short wameshaichoka CCM, watu wanataka mabadiliko mtake msitake.
 
wao wanafikiri vuguvugu la mageuzi na kudai haki linaweza kuzimwa kwa kuwambambikizia kesi na kuwafunga kina Lema, never. Mfungeni Lema, Dr. Slaa, Mbowe, Lissu, Ndesamboro na wengineo; lakini vuguvugu la mapinduzi ndio kwanza limepamba moto na limeshaingia masikioni mwa wananchi, in short wameshaichoka CCM, watu wanataka mabadiliko mtake msitake.

Hapo umenena. CCM wanadhani adui yao mkubwa ni Upinzani (CHADEMA). Watambue kuwa mtu akishajua ukweli hawaze kusukumwa apinge utawala uliopo, mtu anaamua mwenyewe kuandamana. Hivi sasa asilimia kubwa ya wananchi wanajua kuwa kuna wanaonyonya nguvu zao. Hata kiongozi akitokea kusema nchi maskini hawatomuelewa maana wanajua kuwa viongozi wanakula na kutapika.
 
Wao wasubiri tu siku zao maana si wanajifanya wenye nchio wakatyi wao ni wapita nia wssijua muelekeo wanapoelekea

kitaeleweka tu. keep up tanzania!!!!
 
Aliyeleta Thread hii hapa JF anawatafutia kazi Greengard katika jeshi la polisi, kwani nasikia mashariti ya kujiunga na CCP Moshi moja ya sharti lazima uweumepitia greengard, kazi kwelikweli.
 
Back
Top Bottom