Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,189
- 5,821
Jana CCM wamefanya mkutano wao wakati huo huo tume ya uchaguzi imeweka wazi ratiba rasmi ya uchaguzi mkuu.
Hii inatoa taswira kuwa CCM hawajali lolote lile, kumekuwepo mambo mbalimbali yanao endelea kutoka kwa wananchi na vyama pinzani kutaka mabadiliko ya tume kabla ya uchaguzi. Lakini kwa matukio hayo mawili hapo jana kunaonyesha kuwa hakuna cha mabadiliko yoyote yale na uchaguzi upo pale pale.
Pamoja na asilimia kubwa ya wananchi na wadau kuto ielewa serikali iliyopo madarakani na kupigwa wazi wazi hilo wao hawajali kabisa na sio shida zao.
Wananchi na wadau mnapaswa kuelewa kuwa serikali ya CCM iko madarakani zaidi ya miaka 60 hivyo kama ni utamu wa madaraka wanaelewa vizuri uko vipi na ni ngumu sana kuachia. Kwa miaka zaidi ya 60 CCM vitengo muhimu viko chini yao kuanzia Jeshi, Bunge, Mahakama na serikali kuu. Ni ngumu sana kuitoa hapo ilipo kwa mtindo unaofanywa.
Ndio maana wanafanya vile watakavyo maana wanajua kabisa hakuna chochote mtafanya zaidi ya kulia mtandaoni tu.