Elections 2010 CCM wanaswa wakinunua shahada

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
*Polisi yakiri kuwashikilia viongozi

Wakati jihudi za kuliokoa Jimbp la Bukombe liko katika hatihati za za kunyakuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zikipamba moto, viongozi wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa wakinunua shahada kutoka kwa wapiga kura.

Habari kutoka Bukombe ambazo zimethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Seleman Nyakipande, zinasema viongozi hao ni Juma Mhoja na Shadrack Paul, ambao ni makatibu wa Tawiu la Ushirombo na Msonga.

Alisema viongozi hao walikamatwa katika Kijiji cha Msonga, Kata ya Runzewe wakiwa tayari wamenunua shahada 185 za kupiga kura kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wanarubuniwa na baadhi ya makada wa CCM ambao wako katika mkakakati wa kuliokoa jimbo hilo.

Viongozi hao walikuwa wakinunua shahada hizi kwa bei ya kati ya Sh 2,000 na 5,000 huku lengo likionekana kuwalenga zaidi wafuasi wa Chadema ili kudhoofisha nguvu iliyopo.

Kamanda Nyakipande alisema polisi inaendelea kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa hao kwa kushirikiana na TAKUKURU kwa madai kuwa tukio hilo linaingiliana na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Hali ya siasa katika jimbo hilo iko tete kutokana na upinzani mkali uliopo kati ya CCM na Chadema, sababu kubwa ni kutokana na kuwapo makundi katika CCM baada ya kura za maoni zilizoibua malalamiko mengi.

Chanzo: Tanzania Daima
 
CCM wanaswa wakinunua shahada

Chanzo: T. Daima

Hivi Yusuf Makamba bado hajampigia simu Kamanda huyo wa polisi ahakikishe kama kweli ni wa CCM na kumuagiza kuwa iwapo ni wa CCM awaachie mara moja kama anataka kuendelea na kibarua chake?

Ni kweli mwaka huu CCM maji shingoni!!!
Nadhani hata polisi nao wamechoka sasa!!
 
Kawaida yao!halafu wanasema baada ya kupiga kura tuondoke vituoni eti sisi ni washabiki!hawajui kuwa kura ni mali zetu muhimu kuzilinda!
 
hao wananunua shahada za wana sisiem wenzao..! sioni sababu za mwana chadema kuuza shahada..!

tuone kama watafungwa..!!
 
Hawa jamaa wamezoea kushinda kwa wizi tu,hawana lolote,wizi mtupu!!!!
 
Kadi si ina picha ya mwenye kadi hivyo haiwezi kutumiwa na mtu mwingine au wananunua ili iweje?
 
ngoja amri kutoka makao makuu ije, usishangae ukiambiwa ni UZUSHI, ili kuua soo. Mwaka huu mafisadi tunao!
 
hao CCM ni noma watatumia mbinu zote na lazima waondoke madarakani kwa hali inavyoenda.

PEEEEEPPPPPPLLLLLEEEEEEESSSSS PPPPPPOOOOOOWWWWWEEEEERRR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
She she em fungu la kukosa, makamba na wifi yako kikwete habari ndo iyo!!!!!!!!!!
 
Jamani, hiyo ni rasha rasha tu kibunga kinakuja october 31 watu wengi naimani hawatapiga kura kwa kukosa majina yao vituoni. subirini mtaona jamani!!! tena bahati mbaya zaidi hautakuwepo muda mwingine wa kupiga mpaka 2015.

Watu wahimizwe kuangalia majina yao ikiwezekana mawakala wapewe majina ya vituo mapema.
 
Kadi si ina picha ya mwenye kadi hivyo haiwezi kutumiwa na mtu mwingine au wananunua ili iweje?

Wananunua kadi ili yule mwenye kadi (ambaye aghalabu huwa anafahamika kuwa ni wa upinzani) asiweze kupiga kura siku husika ikifika. Wanafanya hivi ili kupunguza kura za wapinzani. Ni umafia flani hivi.
 
Tumuombe Mungu atusaidie uchaguzi salama kwani mwaka huu tutaona na kusikia mengi. Kwa wazalendo tunaopenda nchi yetu tutumie haki yetu ya kupiga kura ipasavyo kwani huu ni wakati wa mabadiliko na sio kufanya mambo kwa kurithi au mazoea.
 
Back
Top Bottom