tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,518
- 21,544
Waziri Mkuu Mstaafu, Dr Edward Ngoyai Mollel Saitoti Ole Lowassa, ndiye alyekuwa kinara na muasisi wa shule za Kata. Pia alikuwa amekusudia baadaye kuanzisha Zahanati za Kata, kwamba kila Kata katika nchi hii iwe na Zahanati yake kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote.
Baada ya kugundua kwamba mikakati hii ingempaisha Dr Ngoyai kisiasa, CCM wakaamua kumuundia zengwe na hatimaye kumuangusha kutoka nafasi yake ya Uwaziri Mkuu kwa skandali feki ya Richmod. Hapa ndipo wakapata mwanya wa kuhujumu mikakati aliyokuwa ameiandaa Dr Lowassa kwa maslahi ya umma. Shule za kata alizozianzisha Dr Ngoyai zikatelekezwa na kuachwa solemba.
Badala ya kuboresha shule hizi, CCM wakaanza kuchakachua mfumo wa utahini kutoka madaraja ya awali na kuanzisha mfumo kanyaboya wa GPA. Lengo lilikuwa ni kuharibu kabisa mfumo wa elimu ili shule za Lowassa za Kata zionekane si lolote wala chochote, na hakika wamefanikiwa kuvuruga mfumo wa elimu yetu kwa hasara ya wananchi. Hapa ndipo serikali ya CCM ilipolifikisha taifa hili. Tazama jinsi wanafunzi wa shule za Kata walivyofeli mitihani yao ya mwaka 2015! Zaidi ya 98% ya wanafunzi wa shule hizi wamepata madaraja ya IV na 0!
Haya ni matunda ya CCM na serikali yao. Walilenga kumdhoofisha Lowassa kisiasa lakini wanaoumia ni watoto wa walalahoi wasiokuwa na uwezo wa kusoma kwenye shule za Akademi huku watoto wao wakisoma Ulaya na Marekani. Ipo siku kitakuja kunuka katika nchi hii, na hapo ndipo tutakapokuja kuheshimiana. Kumbuka kwamba chokochoko humchokoa pweza. Hizi chokochoko za CCM iko siku zitakuja kuwachokoa wananchi wenye hasira na kusababisha taharuki isiyokuwa ya lazima katika nchi hii ya Tanganyika.