CCM wanalilia Zimbabwe iondolewe vikwazo wakati wao wanawekea upinzani vikwazo ndani ya nchi yao. Huu si zaidi ya unafiki wa Kifarisayo?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
KATIBU MKUU WA CCM TAIFA

Hivi karibuni Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimetoa kauli yakuiomba Umoja wa Mataifa na Jumuia za Ulaya kuiondolea vikwazo vyakiuchumi nchi ya ZIMBABWE
Na mimi sinaubishi juu ya hilo nakubaliana nalo na ninaungana na chama changu cha CCM

Ndugu katibu mkuu YESU alitufundisha kuwa

MSIWE KAMA MAFARISAYO WANAFIKI KWAMAANA WAO HUPENDA KUOSHA VIKOMBE VYAO KWA NJE ILI VIONEKANE NA WATU LAKINI NDANI NIVICHAFU

Hivyobasi sitamani CCM ifanane na MAFARISAYO kwakuosha vikombe vyao kwanje lakini ndani nivichafu

CCM tutakuwa ni wanafiki kama tunaona uchungu ZIMBABWE kuwekewa vikwazo vyakiuchumi wakati ndani ya nchi yetuya TANZANIA hatuposawa kisiasa na Kidemokrasia

CCM kama kweli tunahitaji haki itendeke ZIMBABWE kwakuondolewa vikwazo vyakiuchumi, nilazima na sisi CCM tuonyeshe mfano na uchungu wa Demokrasia

KWAKURUHUSU VYAMA VYAUPINZANI NAVYENYEWE VIRUHUSIWE KUFANYA MIKUTANO YAO YAKISIASA

Kwakufanya hivyo tutakuwa tumeitendea HAKI demokrasia lakini pia hata sauti zetu tunazopaza UMOJA WA MATAIFA ZITAKUWA NA MSHIKO TIJA KWA TAIFA LETU

Katibu wangu wa CCM Taifa
Nijambo lisiloingia akilini hata kwa mtoto aliyezaliwa jana

HIVI INAWEZEKANA VIPI UKAAMULIE UGOMVI WA JIRANI YAKO WAKATI KWAKO WATOTO WAKO WANAGOMBANA KWA WAKATI HUOHUO?

Huu NIUNAFIKI usiokuwa na tija nisawa na MTU ALIYESHIKA GITAA NAKUMPIGIA MBUZI ILI ACHEZE
Acheni kucheza na akili za Watanzania iposiku mtayatolea hesabu mambo yenu maovu mnayoyafanya

Mwalimu NYERERE alisema kuwa KUWA UPINZANI SIYO DHAMBI isipokuwa Dhambi inakuja pale mtu mmoja anapohamasisha vurugu na uvunjifu wa Amani ya Taifa letu

Nakwakuonyesha msimamo wa kauli yake hakuweza KUMTENGA WALA KUMBAGUA MWANAYE WAKUMZAA (MAKONGORO NYERERE) ALIPOIHAMA CCM NAKUJIUNGA NA CHAMA CHA UPINZANI CHA (NCCR MAGEUZI)
Nahiyo ndiyo demokrasia yakweli

Nchi haiwezi kuongozwa kwakuwafunga watu makufuri mdomoni ili wasiseme wala kutoa hisia zao katika mambo ambayo yanagusa masrah ya Nchi

Ninaamini ujumbe umefika nimatarajio yangu kuwa tutakuwa tumewatendea haki wana ZIMBABWE na WATANZANIA kwaujumla kama tutajisafisha sisi wenyewe ktk nchi yetu nakuruhudu Demokrasia itawale kwamanufaa ya nchi

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Ishu ya CCM na upinzani ni tofauti na ishu za Zimbabwe kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi.

Moja, CCM kuwaekea Wapinzani vikwazo wanaoathirika ni wapinzani. Wakati vikwazo vya Zimbabwe vinaathiri shughuli zote za nchi nzima na wanachi wake.

Pili, wapinzani hawajanyimwa haki zingine za kitaifa. Wanafanya mambo yao mengine yote isipokuwa uduchu wa kufanya shughuli za kisiasa. Wakati Zimbabwe imefungiwa milango yote katika shughuli za ushirikiano wa Kimataifa.

Tatu, wapinzani wamenyimwa kufanya shughuli za kiasa katika maeneo yasiyo yao. Maeneo yao wanapiga siasa. Wakati Zimbabwe imeachwa ijitesekee kabisa bila msaada wowote.

NB: Siafikiani kabisa na wapinzani kunyimwa kufanya shughuli za kiasa. Lakini kufananisha vikwazo vya Zimbabwe na swala la upinzani Tanzania ni kutoijua athari za Vikwazo vilivyowekewa.
 
Viongozi wa Zimbabwe wafanyie kazi kile western countries wanakilalamikia kuhusu human rights etc etc waondolewe hivyo vikwazo sio kuleta porojo tu
 
Yaani ni kwa namna gani ccm yuko radhi kuuwa kisa madaraka. Ccm na makaburu kuna tofauti gani?
 
Hayo machozi yakwapi..!!??
Samahani mkuu, mimi nimesoma tu heading nikakuja huku mbio....
 
Dahhh...
Nilijuwa huu uzi utakuwa umejaa green kwa machozi ya chama..teh
 
Ishu ya CCM na upinzani ni tofauti na ishu za Zimbabwe kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi.

Moja, CCM kuwaekea Wapinzani vikwazo wanaoathirika ni wapinzani. Wakati vikwazo vya Zimbabwe vinaathiri shughuli zote za nchi nzima na wanachi wake.

Pili, wapinzani hawajanyimwa haki zingine za kitaifa. Wanafanya mambo yao mengine yote isipokuwa uduchu wa kufanya shughuli za kisiasa. Wakati Zimbabwe imefungiwa milango yote katika shughuli za ushirikiano wa Kimataifa.

Tatu, wapinzani wamenyimwa kufanya shughuli za kiasa katika maeneo yasiyo yao. Maeneo yao wanapiga siasa. Wakati Zimbabwe imeachwa ijitesekee kabisa bila msaada wowote.

NB: Siafikiani kabisa na wapinzani kunyimwa kufanya shughuli za kiasa. Lakini kufananisha vikwazo vya Zimbabwe na swala la upinzani Tanzania ni kutoijua athari za Vikwazo vilivyowekewa.
Hayo ni kwa mujibu wa katiba au??
 
Maendeleo ya Tanzania pia yamedumaa tatizo mnashinda mitandaoni hamfahamu uhalisia
Ishu ya CCM na upinzani ni tofauti na ishu za Zimbabwe kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi.

Moja, CCM kuwaekea Wapinzani vikwazo wanaoathirika ni wapinzani. Wakati vikwazo vya Zimbabwe vinaathiri shughuli zote za nchi nzima na wanachi wake.

Pili, wapinzani hawajanyimwa haki zingine za kitaifa. Wanafanya mambo yao mengine yote isipokuwa uduchu wa kufanya shughuli za kisiasa. Wakati Zimbabwe imefungiwa milango yote katika shughuli za ushirikiano wa Kimataifa.

Tatu, wapinzani wamenyimwa kufanya shughuli za kiasa katika maeneo yasiyo yao. Maeneo yao wanapiga siasa. Wakati Zimbabwe imeachwa ijitesekee kabisa bila msaada wowote.

NB: Siafikiani kabisa na wapinzani kunyimwa kufanya shughuli za kiasa. Lakini kufananisha vikwazo vya Zimbabwe na swala la upinzani Tanzania ni kutoijua athari za Vikwazo vilivyowekewa.
 
Viongozi wa Zimbabwe wafanyie kazi kile western countries wanakilalamikia kuhusu human rights etc etc waondolewe hivyo vikwazo sio kuleta porojo tu
+1

Vikwazo vya zimbabwe vinajieleza kabisa kwa nini vipo pale , kikubwa ni human rights violations . Wakati comrade mugabe anatwaa ardhi na kuwafukuza wazungu , kulikuwa na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu ,

Kupiga kelele kuwa western counties waondoe vikwazo ilhali watawala wa Zimbabwe hawajakubali ku comply kwenye demands za haki za binadadamu ni kulazimisha mambo tu, na ni kama haitawezekana maana wenzetu wapo smart kichwani
 
Kama shughuli za wapinzani ni kuzushia watu vifo ni bora wazuiliwe tu.

Uzuri hata hao wazungu wanajua viongozi wa Tanzania ni wakatii hivyo hamna mtu atasikiliza viongozi wahuni. Kama ccm wanazuia wapinzani wasifanye siasa nchini bali kwenye maeneo yao tu, huko Zimbabwe kunatuhusu nini? Viongozi wa Tanzania hakuna mtu aliyewatuma kuhusu masuala ya Zimbabwe, bali wanafanya hivyo kimkakati ili kujilinda wao, pindi huu ukora wao ukichukuliwa hatua waseme ni kwasababu ya msimamo wa nchi yetu.
 
Viongozi wa Zimbabwe wafanyie kazi kile western countries wanakilalamikia kuhusu human rights etc etc waondolewe hivyo vikwazo sio kuleta porojo tu

Ndugu yangu mambo ya Zimbabwe yanahitaji umoja wa Waafrika hakuna sababu kuzungumzia mambo ya human right, kuna mambo makubwa mengi yanayowaumiza wananchi Wa Zimbabwe, mkakati wa Wa Wazungu ni rasilimali walizowekeza Zimbabwe, daima waliweka Zimbabwe kama mali yao, kitenda cha kudai haki ya ardhi kiligeuzwa na lugha ya human right, sina hakika kama haki ya kumiliki mali ni kwa watu weupe tu.
 
Na sisi Watanzania kuna nchi haturuhusiwi kuwekeza kwenye masoko yao ya hisa kwa sababu, tumewekwa kwenye kundi la nchi za kigaidi, sijasikia mtu hata mmoja akiongelea hilo, mojawapo ni Australia wametuweka kundi moja na nchi za kigaidi.
 
Back
Top Bottom