Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 104,104
- 183,897
Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi siku chache zilizopita imetoka na maazimio kadha wa kadha yenye lengo la kujenga Demokrasia na kuimarisha Utawala wa Sheria Nchini Tanzania .
Maazimio ya kamati kuu hiyo ambayo kiuhalisia ni KAMA DIRA YA TAIFA yalisubiriwa kwa hamu kubwa karibu Dunia nzima , na sasa maazimio hayo yamewekwa hadharani kupitia Mkutano wa Waandishi wa Habari na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Salum Mwalimu .
Baadhi ya maazimio ambayo kimsingi yanagusa moja kwa moja Uhai wa Mazungumzo ya Maridhiano ni pamoja na Sharti la kuondolewa kwa Wabunge wanaoitwa COVID 19 , Wakiongozwa na Halima Mdee , hawa waliingizwa bungeni kinyume cha sheria kwa lengo la KUWADANGANYA WAFADHILI ILI WAONE KWAMBA TANZANIA KUNA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI ILI SERIKALI IPEWE MISAADA , Chadema inataka maridhiano yaendelee baada mamluki hawa kuondolewa bungeni maana walishavuliwa uanachama wa Chadema .
Azimio lingine kabambe kutoka Chadema linahusu KUONDOLEWA KWA ZUIO HARAMU LA MIKUTANO YA HADHARA , ikumbukwe kwamba mikutano ya hadhara na maandamano ni haki iliyo ndani ya Katiba ya Nchi .
MWL NYERERE aliwahi kunukuliwa huko nyuma akitamka kwamba CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI , hapa alimaanisha kwamba uhai wa chama chochote cha siasa uko kwenye maandamano na mikutano ya hadhara .
Sasa Swali letu ni hili , kwa Masharti haya ambayo ni kitanzi kwa ccm , Je Maridhiano yatadumu , au ccm itaweka mpira kwapani ?