Ccm wanachakachua maoni ya katiba mpya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm wanachakachua maoni ya katiba mpya.

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by mizambwa, Jul 30, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Kuna taarifa nimezipata muda huu kwa njia ya simu, kuwa CCM wameamua kuchakachua maoni ya Katiba Mpya kwa kusambaza Fomu kwa Wanachama ambao wanajua wataficha siri hasa viongozi katika matawi ya CCM, ili wazijaze na kisha kurudisha ofisini kwa ajili ya kukusanywa.

  Kwa mujibu wa taarifa niliyoipata nikwamba katika ile fomu kuna mambo ambayo wanayahitaji yawepo, mfano Suala la Muungano, na madaraka ya Rais ikiwemo ya kuwa awe ndiye amiri jeshi mkuu.

  Ukipewa hiyo fomu unatakiwa kutoa photocopy zisizopungua tano kisha unajaza na kuandika majina tofauti katika kila fomu na kurudisha ofisi ya chama.

  Nimemuomba aliyenipa taarifa kuwa aniletee hiyo fomu aliyonayo kisha nitawawekea hapa. Ni mtu wa uhakika aliyenipa taarifa hii, ambaye pia ni kiongozi wa UWT katika tawi fulani.

  Naomba kama kuna mwenye taarifa kuhusu suala hili na hiyo fomu kama ipo naomba atuwekee lakini na mimi nikiipata tu itakuwa hewani hapa.

  MYTAKE: kama taarifa ikiwa ni hii, je, Tanzania tutapata Katiba Mpya kweli au itabadilishwa jina tu na kuwa ni ileile???????
  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 2. r

  rwazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tusiogope ccm niwachache sana ktk nchi hii.Tukiwa na dhamila ya dhati tutashinda uovu huwo.
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Katiba mpya hatutaipata tunapoteza tu mda na pesa, bora tungejenga hospitali na madarasa. CCM from the word go haina nia ya kutuandikia katiba mpya.

  M'kiti wa tume Jaji Warioba ni MUUMINI wa SERIKALI 2 ndiyo muundo wa Muungano utakaopendekezwa.
  Makamu M/kiti Jaji Augistino Ramadhani ni MPINGAJI wa mgombea binafsi. Mgombea binafsi litakuwa sio pendekezo la tume.
  Sasa imeingia hii ya CCM kuchachua maoni na hasa kipengele cha madaraka ya RAIS.

  I'm telling you mambo haya matatu tu yataifanya katiba mpya ipigwe chini kwenye kura ya maoni. Unless NEC wachakachue matokeo
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa ni kwamba kila anayepewa hiyo fomu (Hao wanaCCM) anatakiwa kutoa photocopy zisizopungua tano na kuzijaza kwa jinsi wanavyotaka. Hivyo idadi itakuwa kubwa ya hayo maoni yatakayojazwa na kufanya upande wa CCM kuwa wengi.


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJWA!!!
   
 5. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  CCM wanataka Vita hakika hakuna katiba nzuri itakayopatika bila kuchinjana hilo sasa ndio linatakwa na ccm
   
Loading...