CCM: Wana-MTWARA watafutiwe adhabu

CCM: Wana-MTWARA watafutiwe adhabu

Ingawa siamini habari hii, lakini nashauri kwamba adhabu kali kwa wanamtwara ni kumwamisha mkuu wa mkoa na kufunga ofisi zote za ccm katika mkoa huo. Fanyani hivi enyi ccm, msichelewe hapo Dom
 
Narudia tena kauli yangu: wananchi wanapopaaza sauti ya "sasa basi" ujuwe kwamba panatakiwa diplomasia ya hali ya juu damu isimwagike. Ile dhana ya serikali inajuwa kila kitu na isipingwe imepitwa na wakati.
 
Kila mtu akitumia Ubabe tutafika 2015?

Kama ni kweli kuna hiyo mipango,hao CCM wasishangae mchezo ukiwageuka!!!!
 
adhabu gani wanayoweza kuwapa?ni lazima wananchi wa mtwara wanufaike na gesi na lazima serikali ihakikishe watu wa mtwara wanapata maendeleo.Mtwara mkirudi nyuma shauri yenu.
 
Sasa wewe mleta mada hiyo akili uliyotumia kuleta huu upuuzi jf.kwa nini usingewashauri wenzio kuwa wanamtwara maisha yenyewe walioishi kwa miaka hamsini ni adhabu tosha.. Hivyo sasa wanaitaji kusikilizwa na sio vitisho.!
 
Kila kitu kinatokana na mpango wa Mungu,,haya yote Mungu anampango nayo!!!
 
Hapa Lumumba,ofisi ndogo za CCM Dar, sasa ni vikao mfululizo. Kamati mbalimbali zinaundwa na kupewa majukumu mbalimbali lakini yenye lengo moja:kuiadhibu Mtwara. Kwanini waandamane kupinga kuisafirisha gesi toka huko Mtwara hadi Dar es Salaam? Kwanini wamsaliti Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa nchi? Wapo Wajumbe wenzangu wanawaita Mtwara wahaini na wasaliti.

CCM imeapa kuidhibu Mtwara. Wanakamati tumepewa kazi ya kutafuta adhabu mujarabu na kuishauri Serikali. Nitakuja kuwaambia adhabu husika baada ya Kikao cha Jumatatu. Hali ni tete hapa Lumumba.Tutaonana siku hiyo.Jadilini lakini mjue hivyo

Wenu,

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa

ccm bwana sasa mtwara adhabu walizopata toka uhuru haziwatoshi hadi muwatafutie zingine, hawa watu kama ni adhabu tayari walishazipata kusini kanda ni kanda pekee pamoja na kigoma ambako usafiri kwa miaka mingi umekuwa ni wa matatizo waaacheni wapumue sasa!
 
Hapa Lumumba,ofisi ndogo za CCM Dar, sasa ni vikao mfululizo. Kamati mbalimbali zinaundwa na kupewa majukumu mbalimbali lakini yenye lengo moja:kuiadhibu Mtwara. Kwanini waandamane kupinga kuisafirisha gesi toka huko Mtwara hadi Dar es Salaam? Kwanini wamsaliti Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa nchi? Wapo Wajumbe wenzangu wanawaita Mtwara wahaini na wasaliti.

CCM imeapa kuidhibu Mtwara. Wanakamati tumepewa kazi ya kutafuta adhabu mujarabu na kuishauri Serikali. Nitakuja kuwaambia adhabu husika baada ya Kikao cha Jumatatu. Hali ni tete hapa Lumumba.Tutaonana siku hiyo.Jadilini lakini mjue hivyo

Wenu,

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa

Mhh! Mbona wananchi wa Mtwara wameadhibiwa kwa miaka yote 51 ya uhuru? Sasa adhabu nyingine ipi ambayo hawajapata? Labda kifo!!
 
Siasa chafu za kifisadi ndo chanzo cha vurugu zote. Wananchi wa Mtwara wanajua kinachofanyika huko Mererani, Nyamongo, Kahama na kwingineko ambapo raslimali husika haiwasaidii wananchi. Viva wananchi wa Mtwara!!!!!
 
kwani watu wa mtwara hawakuwa na haki ya kutoa hisia zao, ccm wakifanya hivuo watakuwa waapuuzi na mwishi wa siku wao ndio watapata adhabu,waache mbwembwe
 
Sihamini kama CCM wanaweza kuwa akili ndogo kiasi hiki hata kama siwapendi
 
Watu wa Mtwara dawa yao ni kanga, chumvi na vitenge wakati wa uchaguzi!!! Wataichagua ccm tena 2015 hakuna tabu!!!!!
 
Mtu Mzima hatishiwi nyau atii! hizo hila tu mnataka watu waogope.Askari jasiri ni yule alie tayari kufia Vitani, tuko tayari ,liwalo na liwe, hatuogopi tunawasubiri kwa hamu mafisadi nyie ,ama zenu ama zetu hadi kieleweke!!!!

Kila la heri wanamtwara!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom