CCM: Wana-MTWARA watafutiwe adhabu

CCM: Wana-MTWARA watafutiwe adhabu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Hapa Lumumba,ofisi ndogo za CCM Dar, sasa ni vikao mfululizo. Kamati mbalimbali zinaundwa na kupewa majukumu mbalimbali lakini yenye lengo moja:kuiadhibu Mtwara. Kwanini waandamane kupinga kuisafirisha gesi toka huko Mtwara hadi Dar es Salaam? Kwanini wamsaliti Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa nchi? Wapo Wajumbe wenzangu wanawaita Mtwara wahaini na wasaliti.

CCM imeapa kuidhibu Mtwara. Wanakamati tumepewa kazi ya kutafuta adhabu mujarabu na kuishauri Serikali. Nitakuja kuwaambia adhabu husika baada ya Kikao cha Jumatatu. Hali ni tete hapa Lumumba.Tutaonana siku hiyo.Jadilini lakini mjue hivyo

Wenu,

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa
 
Mungu awajaalie mufanikishe miwazo yenu mufilisi. Ila kumbukeni malipo ni hapa hapa duniani tena zaidi siku hizi kila mnachofanya huwaga kinabuma mapema basi ndio kabisaaa.
 
duu kweli ccm ni kama wachawi wameshindwa kutafuta njia ya kuwapa maendeleo wanamtwara ili waache kuandamana, wanajadili kuwaadhibu, mi naona adhabu yao tumieni policeccm kuwaua wote watakapoandamana tena ili muridhishe roho zenu.
 
Hapa Lumumba,ofisi ndogo za CCM Dar, sasa ni vikao mfululizo. Kamati mbalimbali zinaundwa na kupewa majukumu mbalimbali lakini yenye lengo moja:kuiadhibu Mtwara. Kwanini waandamane kupinga kuisafirisha gesi toka huko Mtwara hadi Dar es Salaam? Kwanini wamsaliti Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa nchi? Wapo Wajumbe wenzangu wanawaita Mtwara wahaini na wasaliti.

CCM imeapa kuidhibu Mtwara. Wanakamati tumepewa kazi ya kutafuta adhabu mujarabu na kuishauri Serikali. Nitakuja kuwaambia adhabu husika baada ya Kikao cha Jumatatu. Hali ni tete hapa Lumumba.Tutaonana siku hiyo.Jadilini lakini mjue hivyo

Wenu,

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa

aidha Watanzania hatujui siasa, ama tuliowapa dhamana za uongozi wa siasa hawajui wajibu wao. Maana hizi vuta-nikuvute zimekuwa mara zinatutupa huku, mara zinatutupa kule kiasi kwamba Watanzania tumesahau kupambana na maadui wa maendeleo yetu.

Ona kwa mfano hii taarifa ya VUTA NIKUVUTE aka Mzee Tupatupa inaonesha Chama kinachoongoza serikali hakina mpango wa kuhakikisha Wanasayansi wa Tanzania wanaenda Mwezini achilia mbali kuhakikisha neno "umasikini" linakuwa historia, kwa mujibu wa taarifa hii CCM inajiwinda kuwaadhibu wananchi masikini wanaohoji namna watakavyo faidika na rasilimali zao za asili, sio tu ni aibu wanaMtwara kuogelea kwenye lindi la umasikini kwenye serikali inayojigamba kuongoza kwa ufanisi, bali ni kinyaa kwa serikali inayojiita makini kuwatishia wananchi wake yenyewe. Haya mambo yanaashiria udhaifu mahali fulani, kama sio kwa wananchi, basi kwa serikali ama kwa chama kinachoongoza serikali
.
 
Inamaana wale wazee wa Mtwara walioitwa Ikulu kwa kikao cha dharura na JK hawajasaidia lolote. Huo mchezo mnaofanya hapo Lumumba ni kama mnajichimbia wenyewe. Mtawaadhibu watu 50, ila mtaangushwa na malaki ya watu. Nawashauri mfanye mikakati ya kurudisha pence zetu za tembo Uchina, ama pesa zetu kule Uswiss ili tupunguze deni la Taifa hapo tutawaona wa maana.
 
ukweli ni kwamba watz na CCM is a perfect marriage of cycle of stupidity, gullibility and poverty. Fireworks/
 
aidha Watanzania hatujui siasa, ama tuliowapa dhamana za uongozi wa siasa hawajui wajibu wao. Maana hizi vuta-nikuvute zimekuwa mara zinatutupa huku, mara zinatutupa kule kiasi kwamba Watanzania tumesahau kupambana na maadui wa maendeleo yetu.

Ona kwa mfano hii taarifa ya VUTA NIKUVUTE aka Mzee Tupatupa inaonesha Chama kinachoongoza serikali hakina mpango wa kuhakikisha Wanasayansi wa Tanzania wanaenda Mwezini achilia mbali kuhakikisha neno "umasikini" linakuwa historia, kwa mujibu wa taarifa hii CCM inajiwinda kuwaadhibu wananchi masikini wanaohoji namna watakavyo faidika na rasilimali zao za asili, sio tu ni aibu wanaMtwara kuogelea kwenye lindi la umasikini kwenye serikali inayojigamba kuongoza kwa ufanisi, bali ni kinyaa kwa serikali inayojiita makini kuwatishia wananchi wake yenyewe. Haya mambo yanaashiria udhaifu mahali fulani, kama sio kwa wananchi, basi kwa serikali ama kwa chama kinachoongoza serikali
.

Umenena mkuu!
Hii serikali imeshasahau ya kwamba cheo ni dhamana!
Wamejisahau ya kuwa wapo madarakani kutokana na kura za hao hao wanaotaka kuwaadibisha.
Watanzania amkeni, ccm haiko kwa ajili yenu.
Ondoeni uozo huu muone angalau harufu ya mabadiliko.
Mpira uko kwetu wana Mtwara na watanzania wote!
Haitakuwa rahisi lakini hatuna budi kuanza.
Hata TANU ilipoleta uhuru kuna waliotia mashaka kama ingewezekana, lakini sauti ya yule, mimi na wewe ikamtoa mkoloni.

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
 
Mi na familia yangu tushaamka zamani...hatutambui CCM
 
Ninapoona habari kama hii naona mabadiliko makubwa ya kisiasa yakiinyemelea Tanzania.Naona wanachi wakiamua kusimamia ukweli na vitendo.Nawaona wakijibu mapigo kupitia sanduku la kupigia kura 2015. Enyi CCM,ikumbatieni Mtwara.Mnayo Mtwara,Lindi,Tanga,Ruvuma na Pwani kama mikoa mnayotamba kadiri mtakavyo.Mkiiudhi hii,hali yenu itakuwa tete hapo 2015. Iweni na busara...saidieni badala ya kukomoa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom