CCM wana jazba na yamewashinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wana jazba na yamewashinda

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkimbizi, Sep 13, 2010.

 1. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jana nilikuwa napata kilaji mahala fulani, akapita omba omba fulani. Alivyokuja kwangu nikamwambia mimi hela hata nikikupa haitasaidia, cha maana October 31 usiipigie kura CCM. Nikamwambia akiipigia CCM ataomba omba maisha yake yote na vizazi vyake kwa maana gap kati ya mwenye nacho na asiyenacho ni kubwa na hakuna anayewajali. Akaondoka. Baada ya muda akapita dada anauza soksi etc, akaja kwangu, nikamwambia soksi zako kwa mazingira haya siwezi kununua. Yote hii ni sababu kuna mfumo duni na usiofaa kwa wachuuzi wadogo wadogo matokeo yake hamfanikiwi. Nikamuuliza umejiandikisha kupiga kura? akajibu hapana. Nikamwambia basi waambie rafiki zako na ndugu zako wasiipigie kura CCM maana utaishia kuuza soksi maisha yako yote wakati watu wanaishi maisha ya peponi.

  Kumbe pembeni kulikuwa na kada wa CCM, akaanza kuongea kwa jazba(baada ya kuona reaction ya yule omba omba na dada muuza soksi)". ''wewe unaongea nini, sio kila mahala mtu anafurahia unachosema!!!''. Nikamuuliza kwani shida iko wapi mbona jazba..? Wewe hunijui mimi, mimi nakujua sana wewe unakuja sana hapa... Nikamwambia kwahiyo?? Nikaongelee ******? Yani upuzi wote miaka 49 toka tupate uhuru nikae kimya?? Mbona unatumia nguvu nyingi kuongea?? Mapovu, unatetemeka vipi bwana nchi huru hii kusema.. Au mmezoea kuendeshwa tu kama mapunda?? Jamaa akaondoka akabamiza meza na kunitisha..!

  Sasa najiuliza, jazba jazba jazba.. Yule mwingine alitishia kumshtak mtu kwenye mdahalo TBC. Sasa tunajua na dawa yenu ni october 31 tu!!!
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Utapigwa mawe ndugu lazima uwe makini na uwe na busara unapofanya haya......................hata nyerere kuna kipindi alifikia akasema "kuzungumzia azimio la arusha kwa sasa ni lazima uwe mwendawazimu"...kwani kuna watu walikuwa hawako tayari kusikia habari za azimio japo moyoni mwake aliendelea kuwa na msimamo nalo na aliamini hiyo ndiyo ingekuwa misingi ya kulikomboa taifa hili...........kwa hiyo kusema km wewe tena mbele ya hadhara inatakiwa uwe na moyo wa umwenda wazimu...
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Pole ndugu yangu. CCM hupenda sana kutawala makondoo. Katika hotuba yake kule Jangwani, Dr Slaa aliwapa CCM laivu, kwamba wamaemua kuwafanya vijana wa nchi hii kuwa wamachinga milelele na milele na kwamba CCM inajigamba bure kwamba imetoa ajira 1.3 milioni katika miaka mitano ya JK. Akahoji: Kuna vijana wenye digrii wanatembea nazo mifukoni hawana kazi, jee hizo ajira 1.3 milioni ambazo serikali ya JK illizitoa, ilizitoa kwa akina nani?
   
Loading...