CCM wamwandaa Magufuli kwa midahalo!

CCM wamwandaa Magufuli kwa midahalo!

Kwa jinsi ninavyomjua Magufuli, Lowassa atakua nawakati mgumu sana kushindana naye kwenye midahalo. Naamini UKAWA wanalijua hili na watafanya kila hila kulizuia kutokea.

Lowassa ni kamanda kwa jina lakinj hayupo fit mentally and physically.

Magufuli mwenyewe hana karama kihivyooo, labda kutiririka creaming na kujishusha na sasa wananchi tunataka mabadiliko sio risala na makaririsho. itabidi pia wote wawe tayari kujibu maswali watakayoulizwa kwa ufasaha. Waendesha midahalo wasipendeleee na pia wasitangulie kuwapa majawabu wadahiliwa, tutawapima kwa namna hiyo
 
Mh EL niliyemwona jana Mbeya akihutubia umati wa watu,siyo mahiri kuvutia hadhira kwa hotuba. Alikuwa anatetemeka,anarudia-rudia sentesi moja. Mafuriko ya jana ilikuwa maeneo yake angalau kujidai kwa muda,hata kama bado kampeni(Dr Slaa ndo sehemu zake). Sipati picha EL akikutana na Magufuli kwenye mdahalo.
 
Niliyoyaona leo jangwani,Magufuli ni namba nyingine. Mh Lowasa na UKAWA kwa ujumla bado wanazo kazi kubwa ya kufanya. Nausubiri mpambano wa wagombea urais,hasa UKAWA vs CCM,wakitetea sera zao,namna watakavyotatua matatizo ya kijamii. Wasiwasi wangu UKAWA watamzuia EL asishiriki.
 
CCM ni chama kubwa. Hawa jamaa wanafanya mambo yao kwa mikakati mikali. Kwa Lowasa niliyemwona leo kwenye mkutano wa bawacha,sidhani kama anaweza kumudu dak 90. CCM walimzuia Kikwete kupambana na Dr Slaa,wakijua Dr ni mashine kubwa. Sasa hivi wanashinikiza mpambano wa ana kwa ana kati ya Dr Pombe Vs Mh Lowasa
 
Mgombea wa CHADEMA hawezi kuthubutu kuingia kwenye mdahalo piga ua.
Umegonga penyewe. Lowasa niliyemwona jana hawezi kushindana na Magufuli,katapila la CCM.
 
UKAWA wamekula pori,wamehama njia kuu. Mdahalo uko hatihati,sijui kwa nini wanamficha jamaa wa Monduli. J. Pombe(Phd) yuko tayari hata kufanya madahalo na yeyote kwenye UKAWA anayejiamini kutetea ilani yao.
Ngosha kafunguka balaa. Kama Dr Slaa(Phd)atakubali kuwakilisha CDM kwenye mdahalo,itabidi afanye homework,lakini wengine mhh!,hâta akiamshwa usingizini. Kuna tetesi CDM watamleta Mbowe au Salum Mwl apambanishwe na Magufuli,kisa ugeni wa EL,na Slaa,Mnyika,wanadengua.Lisu naye maji yako shingoni jimboni kwake
 
Ni dhahiri CCM wameiva kwa mikakati. Hiki ni chama kongwe. Wamejiandaa kwa mdahalo muda mrefu,hasa mgombea wao wa urais,JP Magufuli. UKAWA, washindani hasa wa CCM katika mbio za urais,wanataka kutia mpira kwapani kabla ya dak 90. Mbatia,mwenyekiti mwenza wa UKAWA, anataka wenyeviti wa vyama washiriki midahalo hiyo.
 
Back
Top Bottom