CCM Wameishika CHADEMA PABAYA...

"The only time a politician tells the truth is when they call another one a liar."
 
it is clear that biashara ya watu kukabidhiwa kadi za CCM huwa ni mamluki yaana wenyewe kwa wenyewe na huwa local CCM leaders wanawadanganya viongozi wao wa kitaifa....hii imetokea sehemu nyingi tu.
 
Na Ghati Msamba, Bunda
Gazeti la Uhuru

Hili si tulisha li RIP? limefufuka?😛ound:

Halafu hii sekretarieti ya CCM vipi? Shurti wajumbe wakajitambulishe kwao? Chiligati alikuwa Singida huyu nae Mara? Mcheza kwao nini? Walahi wangeanzia kusikokuwa kwao wangeambulia miangwi!!
 
hawa ccm humu kwenye jf wanafanya nini mi naona wanaleta kichefuchefu tu. akina nape, mwakyembe, sita wote wamedhihirika ni wasaliti kwa ccm, mafisadi mmewashindwa kuwaondoa, magamba yamewazidi halafu eti mnafiki anasema cdm imeshikwa pabaya. hivi hata uwezo wa kujipambanua hamna nyie ccm .......anguko lenu lipo karibu sana
 
Imekuwaje tena?? Nafikiri Nape alisema wanampango wa kuacha wanachama wa papo kwa papo? sasa hawa 239 wamepata mafunzo wapi? isije ikawa ni mamluki kama alivo waita? Kweli sasa hivi CCM wamebanwa pabaya sana. CDM kaza buti CCM wamechanganyikiwa.
 
siku nyingine ambatanisha na picha ili kuthibitisha uliyoyaandika.
 
Mwili mkubwa akili kidogo. Nilidhani dr. Slaa. Kashikwa na mabilioni ya EPA. Kumbe umbeya!! Kazi kweli kweli!!
 
Niliposoma chanzo tu kuwa ni gazeti la uhuru sijaendelea zaidi maana ndani kilichoandikwa nnajua ni prop....,,
 
Nimekuwa nifukifuatuatilia hoja zinazotolewa na wapenzi wa Chama cha Magamba juu ya ufisadi wa Dr Slaa,Mbowe na Ndesa pesa nikagundua kuwa kweli mtu anapoishiwa hoja ni sawa na gari bovu linapokosa break linakwenda popote. Kwani hata kutunga uwongo unaofanana na ukweli ni tatizo kwa sababu breki hamna. Fikiria Ndesamburo jinsi anavyojitoa kuwasaidia watu wa jimbo lake na jinsi alivyosaidia CHADEMA kwa hali na mali tena kwa uwazi na biashara zake ni za uwazi, Angalia Mbowe jinsi anavyojitoa kwa hali na mali kukisaidia chama chake na wananchi kwa ujumla na biashara zake zote ni za uwazi tofauti na wafanyabiashara wa chama cha magamba wanaotoa michango kwa kificho na hata hiyo wanayosema ameuzia chama magari yaliotumika ni kitu kimejadiliwa kwenye vikao na kuwekwa wazi. Tazama mtu kama Dr Slaa alivyojitoa kwa hali na mali kuwapa watanzania elimu ya uraiya na hata kuahatarisha maisha yake, mtazame Zitto kazi aliyoifanya juzi juzi hapa eti hawa ni mafisadi kama ndiyo hivyo basi mimi natangaza ufisadi wa CHADEMA tunauhitaji kabisa na waendelee kuwa na ufisadi huo.

Watanzania sii wapumbavu kiasi hicho cha watu kufikiri kuwa uanaweza kuwadanganya kama kuwa hawaoni wala hawatambui kinachofanyika. Ni dhambi kubwa chama CCM kinafanya kuwaona wa TZ hawawezi kutambua ni nani fisadi na nani mzalendo. Hivi ninyi ndugu zangu hamumuogopi hata Mungu kwa uovu mnaowafanyia wa TZ waliopewa nchi yenye utajiri mkubwa kiasi hicho mkawafanya masikini kiasi hicho. Jamani maisha yetu ya kuishi hapa Dunia ni mafupi ni miaka sabini ukiwa na nguvu miaka 80 sasa yanini kuhangaikia mambo ya rushwa, wizi na kupenda madaraka nasema malipo ya mwovu huanzia hapa hapa Duniani na wengine wenu mmeshaanza kulipwa. Hivi kunaraha gani ya wewe kusomesha nje mtoto wako kwa fedha za rushwa ili hali kuna mtoto wa masikini licha ya kwenda shule hana uhakiaka wa kula.Mshahara wa Dhambi ni mauti wanyonge wanalia na Kitabu cha Mungu kinasema kilio cha mnyonge kinamfikia Mungu moja kwa moja na washauri mbadilike na kuacha uongozi wa nchi hii kwa wengine bila hivyo huko tuendako mtakuja ona hasira ya Mungu.
 


Source gazeti la uhuru.Mnatoa nakala ngapi kwa siku?coverage yenu ya mauzo ikoje?

Tumeshawazoea wasanii, ninyi any way watu wa leo hawaambiwi tazama.
 
umeongea vizuri, lakini title yako inamislead!
 
Niliposoma Title nilipata picha tofauti na kille kilchoma. Hebu rekebisha Mkuu
 
mkuu nilianza kutishika na tittle yako,kumbe tupo pamoja sana. usijali,kuna watu huwa wanatoa comments zao bila kusoma ujumbe so kuna uwezekano ukakutana na makombora. mana hawa wandugu si mafisadi kivile,title umeikosea.
 
Mtaongea mengi ila nawaambieni ccm imekufa siku nyingi ila inasindikizwa na nguvu za dola tu hamna kipya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…