CCM wamefikia kujimilikisha fedha walipa kodi na kutangaza kuwa wao ndio wanazitoa kwa wananchi

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Ukiona mwanamke unampa pesa za matumizi ya watoto na ndugu zako halafu anaenda kwa watoto anawambia yeye ndio anaye wapenda sana na ndiye anayetoa pesa za matumizi, mkeo huyo mkimbie na tena kimbia bila kugeuka nyuma utakuja kunishukuru siku moja.

Mke wa namna hiyo ujue anakuona wewe unayetoa hela ni zuzu na anataka kujionesha yeye ndie kila kitu kwa watoto ili apate Upendo usiostahili kwakuwa hajiamini kutokana na matendo yake kama watoto wanaweza mpenda bila kutumia njia ya hila ya uongo.

CCM ndio wamefikia hatua hiyo kwa Sasa. Baada ya kuona hawapendwi na wananchi wameamua kujimilikisha pesa za walipa kodi na kujitangaza kuwa eti wao ndio wanazitoa kwa wananchi.

Rais ana pesa gani maskini tuu hawa wameomba kazi mpaka kupiga mapushapu hadharani ili wapate kazi halafu eti mjinga mmoja anakwambia Rais katoa hela kufanya mradi Fulani na Fulani.

Pesa ya Serikali inatumika kwa bajeti iliyopitishwa na Bunge Sasa Rais anatoa hela wapi?

Majitu haya yenye uchu wa Madaraka na yanayong'ang'ania Ikulu kwa gharama zozote mpaka kuwapakazia wenzao Ugaidi hewa ndio wawe matajiri wa kutupatia sisi fedha?

Hebu acheni ushamba ninyi mkome kutueleza upupu wenu oooh Rais katoa pesa sijui. Sisi sio mazuzu tunajua pesa ni zetu Rais analipwa mshahara kwa Kodi za wananchi kuanzia mavazi, usafiri, chakula na maladhi halafu ndio mtuambie anazo hela za kutupa wananchi?
 
Back
Top Bottom