CCM walitaka kumtumia Msigwa kwa namna tatu

CCM walitaka kumtumia Msigwa kwa namna tatu

jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,756
Reaction score
4,849
Wanabodi Salaam.

Nimeona muda mfupi taarifa kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali Katibu Uenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole akiambatana na ujumbe wa viongozi wa CCM wamekwenda gereza la Segerea alipokuwa akishikiliwa Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mchungaji Peter Msigwa, kutokana na kutokamilisha taratibu za kimahakama juu ya malipo ya faini kutokana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Kisutu.

Hivyo, kumekuwa na juhudi mbalimbali zinazofanywa na chama chake (CDM) kwa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani (hasa NCCR Mageuzi na ACT Wazalendo) bado sijaona juhudi toka vyama vingine (samahani kama navyo vitakuwa vimetoa tamko lolote kuhusiana na kushikiliwa kwa viongozi hao wa Chadema binafsi sijaona). Juhudi hizo ni kukusanya michango ya fedha kutoka kwa watu mbalimbali ili kuwatoa/kuwalipia faini viongozi wanaoshikiliwa waweze kuachiwa huru, wapo ambao wameshaanza kuachiwa baada ya kulipiwa faini zao.

Suala la kusema ndugu wa Msigwa walijichanga milioni mbili wakashindwa kumalizia zilizobaki wakati wakijua kuna juhudi za chama chake kuwachangia viongozi wote linaacha ukakasi. Wangetakiwa kuwasiliana na viongozi wa Chadema kwanza kabla ya kwenda kwa Mh. Rais.

Ghafla jioni ya leo, sote tumeona taarifa za Katibu Mwenezi wa CCM Ndg. Polepole, ikielezwa alikwenda kumlipia Msigwa faini yake atoke gerezani, swali ninalojiuliza haraka ni kwa nini iwe Msigwa?
Hapa Msigwa angetumika kama chambo tu.

Wazungu wanamsemo wao wanasema; "there is no free lunch" hivyo kwa akili ya kawaida ndugu msomaji utagundua CCM walitaka kumtumia Msigwa kwa mambo matatu.

Mosi: ku- disturb nguvu ya umma iliyoonekana baada ya viongozi hao kushikiliwa; hili halikutegemewa na wengi kwamba watanzania kwa umoja wao bila kujali itikadi, rangi, dini, wala kabila, kujitoa kwa hali na mali licha ya hali ngumu waliyonayo, kuwachangia viongozi wa CDM waweze kutoka gerezani. CCM hawakulitegemea hili, walijua hao viongozi wangeachwa wapambane kivyao kujinasua na mtego wa kifungo cha miezi mitano uliokuwa unawakabili kama wasingelipa hiyo faini.

Hivyo kutokana na nguvu ya umma iliyooneshwa, CCM wakaamua kuvuruga huo mpango ili ionekane na wao pia walichangia viongozi wa CDM, wakiamini kufanya hivyo kungewakatisha tamaa baadhi ya wachangiaji.
Kwa hili wamefeli.

Pili: Kurudisha imani ya wapiga kura; huu ukiwa ni mwaka wa uchaguzi, CCM inajua fika hali yale ni mbaya huku ikiwa inajitahidi kununua wabunge na madiwani wa upinzani kila kona ya nchi. Hivyo, waliamua kumchangia Msigwa ili ionekane CCM ni chama kinachojali utu wa mtanzania, bila kujali itikadi yake kisiasa, kwamba hata akiwa mpinzani wao wapo tayari kumchangia aweze kutoka gerezani.
Kwa hili pia wamefeli.

Tatu: Msukumo kutoka jumuia ya kimataifa; kama inavyojulikana, CCM ndio chama kinachounda serikali, na kinawajibika kwa namna moja au nyingine kuilinda serikali yake. Sote tu mashuhuda, hukumu waliyopewa viongozi wa Chadema imeishtua jumuia ya kimataifa hasa Marekani ambapo siku za karibuni tumeshuhudia matamko mbalimbali kutoka idara yake ya mambo ya nje inayoshughulikia masuala ya Afrika. Ni wazi kutokana na hili, CCM iliamua kumlipia Msigwa ili ijaribu kuisafisha taswira ya Tanzania kwenye jumuia ya kimataifa kutokana na hukumu ile.

Asanteni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa ni mchezo wa mahesabu ccm hawajui hesabu wanajua kutumia Vyombo Vya dola kujinufaisha. Hesabu walizo Nazi ni kununua viongozi badala ya wananchi. Hongera chadema kwa kujua jinsi gani ya kuucheza mchezo
Na hawana mtu smart wa kupanga mipango,wao ni kukurupuka tuwisho wa siku wanapata aibu
 
CCM wamejipiga bao wenyewe!Timu ya propaganda imefeli big time!
 
Nchi huru uhuru wa maoni!

Nadhani sasa umeamini ccm chini ya jiwe haiwezi tena siasa za hoja wala ushawishi, ndio maana imeamua kutumia dola bila aibu. Hivi vituko wanavyofanya ccm leo ndio hiyo inatumika nguvu kubwa kutuaminisha kuwa ccm sasa hivi ni imara!

Huu utoto wa leo wa ccm toka kwa viongozi wa ccm, ndio huo tunaaminishwa kuwa ccm imeua upinzani! Je una shaka tena kuwa viongozi wa upinzani huwa wananunuliwa kwa ushauri wa mwenyekiti na genge lake? Ccm hii uliyoiona ikifanya utoto hapo gerezani, ndio hiyo iliyoendesha kikao cha maadili ya Makada wake wiki zilizopita.
 
Hivi undugu wa Msigwa na Kayafa unageukaje kuwa jambo la ki-ikulu na kichama??
Nahisi pale #ikulu na #ccm kwa sasa hakuna watu smart...
Na hata dola nayo ishaanza kuwashtukia...!!
Wala!! CCM wamechanganyikiwa. Walitaka kuua nge wakapiga kichwa wakasahau mkia. Matokea yake ukawadanga sumu. Sasa hapo walipo wanaugulia maumivu na paracetamol walitupa wakidhani wamepona.
 
Hivi undugu wa Msigwa na Kayafa unageukaje kuwa jambo la ki-ikulu na kichama??
Nahisi pale #ikulu na #ccm kwa sasa hakuna watu smart...
Na hata dola nayo ishaanza kuwashtukia...!!

Kweli kabisa, wale viongozi wa vyombo vya dola ambao huwa wanapewa maagizo na viongozi wa ccm kwa kisingizio kuwa ndio kimeshika dola, wajue kuwa wanaaigizwa kutii amri za watu wenye upeo gani. Ni vyema vyombo vya dola kuanzia sasa vikasimamia weledi na sio maagizo ya hao wahuni.
 
Back
Top Bottom