Mimi ni mkristo mkatoliki nalijua kanisa langu kwa undani kabisa. Masimamo wa kuipinga tume ya WARIOBA ni shinikizo la KARDINALI Pengo kwa maslahi ya kanisa katoliki huko Zanzibar. Ni kweli matukio mabaya yamefanyika na serikali ya CCM kushindwa kuyashughulikia na hata kutoa majibu. Kumekuwa na juhudi ZA kuidhibiti zaidi Zanzibar. Tukumbuke JK alishawambia CCM wajiandae kisaikolojia kupokea serikali 3 na kusaini rasimu zote. Mnajiuliza maswali nini kimetokea na Watu kubadilika ghafla hata wale waliokuja pamoja mfano wajumbe wenye nguvu wa Zanzibar ? Nawapa jibu hapo. Binafsi nimewaelimisha viongozi wangu wa dini falsafa ya ukristu ya kwenda pole pole kama alivyoshauri Gamaliel kwenye kitabu cha matendo ya mitume. Kuikandamiza Zanzibar sio kuimarisha ukristu . Kama alivyolia LYatonga MRema 2005 kwa KIlaini na Mimi nalia Leo kwa Askofu wangu KARDINALI Pengo. Umeiharibu Tanzania. Amani kwanza serikali baadae.