CCM wakumbuke Ghalib Bilali alitangaza kugombea urais ndani ya CCM dhidi ya aliyeko madarakani

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
555
915
Mwaka 2000 jina la Ghalib Hilal liliongoza katika kura za maoni ya CCM kumpata mgombea urais wa Zanzibar.

Lakini NEC ya CCM ilipokaa iliondoa jina la Ghalib Bilal na kumweka Amani Karuma, tena naiskia aliyekuwa wa tatu.

Kitendo hicho kikaunda kundi na kundi la Bilal liliendelea kuwa na nguvu.

Karuma akatawala kwa miaka mitano na ilipofika mwaka 2005, wengi wakajua kuwa ataendela kwa kipindi cha pili kama kawaida ya CCM.

Kumbe, Ghalib Bilal alikuwa anaendelea na mipakakati yake kugombea urais wa Zanzibar kupitia CCM bila kujali mazoea ya CCM ya kumwacha aliyeko madarakani amalizie miaka mitano inayofuata.

Watu wakadhani utani, hatimaye pamoja na Amani Karume kuchukau fomu za kumalizia kipindi chake, GHalib BIlali naye akachukua fomu ili wakakutane kule Dodoma. Wakati huo mwenyekiti wa chama ni Benjamin Mkapa.

Sik ya siku ikafika, hadi watu wamekusanyika pale Dodoma, Kikwete hajachaguliwa kuwa mgombea wa CCM na jina la Rais wa Zanznibar haijajulikana atakuwa Bilali au Karume.

VYombo vya habari vilimshambulia sana Bilal kwa swali kwamba "kwa nini ameamua kugombea urais wakati bado aliyeko madarakani atagomea". Jibu la Bilali lilikuwa ni fupi na hakuna mwana CCM mwandishi wa habari aliyeweza kupnagua hoja yake.

Hoja au jibu la GHalib BIlali lilikua hivi, "Kama kugombea kungekuwa na tatizo basi kanuni zingesema". Hakuna tena ndani ya CCM hadi leo mwenye akili ya kupnagua jibu hili, maana ni ukweli.

Sasa, baadaye imebakai kama siku moja kule Dodoma, ndipo GHalib BIiali akaondoa jina. Je, aliondoaje"?

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais Mkapa kule Zanzibar anasema "KWa heshima na ttadhima nilimwomba BIlali aondoe jina lake".

Hivyo, BIlali akawa ameweka precedence kwamba, hakuna kanuni inayomkataza mwana CCM kugombea urais na aliyeko madarakani. Sanasana kama watu hawapendi, basi hawana kifungu cha kumfukuza au kumzuia kama akiamua kugombea.

Na zaidi ukitaka aache msitumia mashinikizo badala yake kumwomba kama MKapa alivyomwomba Bilali kwa heshima na taadhima.

Na kuona kilichotokea baadaye ni kwamba Bilali huyohuyo akaja kupewa umakamu wa Raia wa Muungano mwaka 2010.

Kimsingi ni kwamba kuna kitu ndani ya CCM kinaendelea na haijulikani kwamba sasa wakati umefika wa kukifumua au bado. Hiki kitu ni kwamba kw amiaka mingi baada ya Nyerere CCM wamekuwa wakitafuta namna ya kufanya ikibidi Rais atawale kipindi kimoja tu. Taabu ni jinsi wao wenyewe walivyompa madaraka makubwa mno Rais maana ukijaribu tu japo siyo kosa basi utashughulikiwa na wapambe hata kama Rais mwenyewe hatashughulika yeye mwenyewe.

Hivy, kinachoendelea sasa utasikia majina Membe, Diallo na mengine mengi lakini ukweli ni huu nilioueleza.

Tatizo la hawa hawajitokezi hadharani kama Ghalib Bilali. Wajitokeze na wawe na jibu lilelile la Bilali maana huwa halijibiki kwa hoja.
 
Pale ccm akiondolewa mangula na mkapa ccm kwisha kabisa na huyu mh nimjuavyo mmmm...
Ngoja niishie hapo.
 
Kwenye hili nadhani hata mimi niliandika though sikutumia case study hiyo ya Dr. Bilali mtaalamu na nguli wa Physics hasa upande wa nuclear; ukweli hakuna kosa lolote alilolifanya au analolifanya ndugu Membe, kwangu mimi hiyo ndio demokrasia. Hasira hizi kwa Membe binafsi nazitafsiri tu kwa mhe amekua ni mtu asiyependa upinzani hata kidogo, tabia na mwenendo wake ni kama anapenda zile KURA za NDIO zirudi kuliko kushindanishwa na mtu mwingine ambaye anadhani atamzidi KIHOJA nk, refer historia yake tokea ameanza mambo haya ya siasa na hasa kuanzia jimboni kwake mwaka 1990 hadi uchaguzi wa mwisho aliogombea kama mbunge, ni mtu anae amini katika ONE MAN SHOW na sio kushindana kwa HOJA ili watu wachague wanacho kipenda! Membe hana KOSA, Dr. BAshiru anajua, Polepole anajua na wana ccm wote wanajua but mtu mwenye mamlaka ndio shida
 
Kumbuka kuna kanuni (sheria) zilizoandikwa na zile zisizoandikwa. vyote huwa sehemu ya utamaduni uliozoeleka.
 
Hata hivyo inabidi tuache ulimbukeni wa kujifanya kwamba hatujui kanuni za chama, tuache kujipendekeza kuzuia mambo ambayo yameruhusiwa na Katiba zetu.

Najua 2020 watachukuwa fumo lkn mwisho wa siku vikao vitaamua (KwamabJPM akishinda wale wenzake wakubali kupanda jukwaa kumwombea kura - kazi ya viongozi wa juu kurudisha watu pamoja). Mfano ni kwamba Jimbo la Buyungu, Kigoma baada ya Kasuku Bilago kufariki dunia walichukuwa fomu Makada 20 ambao ni Mhe. Eng Chiza, Msakila Kabende, Aloyce Kamamba, Gwegenyeza, Mawazo, Gwamagobe na wengine wengi tu. Baada ya kura za maoni zilizompa Eng Chiza ushindi CCM ilikaa na wagombea wote na kuwapa mwongozo ili kupata ushindi. Jukwaani walipanda na ushindi umepatikana.

Si Buyungu pekee, lkn hata Korogwe kwa Maji Marefu walichukuwa fomu Makada takriban 40 lkn mwisho wa siku wote walivunja makundi na kumnadi mgombea mmoja aliyeteuliwa.

HIVYO, hata kama kuna makada watajitokeza kutafuta urais kupitia CCM mwisho wa siku lzm viongozi wajikite kwenye kuunganisha watu hao ili kutengeneza kundi moja la ushindi bila kusahau kuwa ikitokea Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akaanguka haimanishi kuwa CCM na watanzania hawatatambuwa mchango wake (Nidahmu kwa umma, Matumizi ya fedha za umma, miradi ya maendeleo, vita dhidi ya ufisadi, madini nk) ni kati ya mambo ambayo hayawezi kusahaulika kwa wananchi wote.

CCM ni imara sana na si rahisi kuyumba
 
Back
Top Bottom