CCM wajifunze kutoka Uganda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wajifunze kutoka Uganda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Sep 12, 2009.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati marais waliomtangulia waliamua kuondoa utawala wa Buganda kama njia ya kuondoa ukabila na kuunganisha nchi ya Uganda, Mseveni aliamua kurudisha utawala huo wa jadi wa Buganda kama njia ya mtaji wake wa kisiasa na kutafuta kuungwa mkono.

  Sasa mambo yamegeuka, Mseveni anamwaga damu kutumia jeshi lake na polisi kudhibiti maandamano baada ya Mtawala wa jadi wa Buganda kukataliwa kutembela Kampala. Vurugu hizi ziwe fundisho kwa CCM ambao waliamua kutumia ahadi ya Mahakama ya kadhi katika ilani ya CCM ua uchaguzi kama mtaji wa kisiasa wa kupata kura za Waaslamu. Marais watangulizi, Nyerere, Mwinyi, Mkapa wote waliendeleza umoja huo bila kuchanganya dini na siasa kama katiba inavyosema. Sasa angalia, waislamu wanadai ahadi ya mahakama ya kadhi na hawaishii hapo wanasema mwaka 2010 watapigia kura waislamu wenzao, hii ni hatari katika umoja wa taifa letu. Vilevile nimeshtushwa na kauli za makamanda wa wa vita dhidi ya ufisadi huko Nzega. Kauli ya kuwa Selelii ni mnyamwezi mwenzao ni kauli ambazo hazifai kutumika katika majukwaa ya kisiasa. Mtu hachaguliwi kwa kabila lake wala dini bali kwa uadilifu wake na moyo wa kusaidia watanzania. Tabia hii ya kutumia udini na ukabila inaonekana kuota sana mizizi katika chama cha CCM.

  Kwanza mtandao wa Kikwete walianza kumbagua Salim Ahmed Salim kuwa ni mwarabu kwa hivi hakusitahili kuwa rais. Chenge pia alikimbilia kwao kwa kutumia kabila lake kama njia ya kuungwa mkono. Pia Lowasa, akakimbilia umasaini ili kupata kuungwa mkono baada ya kujiuzuru uwaziri mkuu. Muelekeo huu wa CCM wa kutumia ukabila na udini kwa manufaa yao ya siasa utaifanya Tanzania iwe kama Kenya na Uganda. CCM sasa wajifunze kwa wanayotokea uganda ili wasiharibu nchi yetu, Ni bora wawaachie CHADEMA au chama kingine cha siasa kuliko kuiangamiza nchi yetu kwa manufaa binasi ya kisiasa.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  <Ni bora wawaachie CHADEMA

  Ndugu, naona umezungumzia mambo yenye ukweli mwanzo wa barua yako, lakini mwisho wa barua yako naona umemwaga ma.. jamvini!
  Chadema!!!! Sio bora hao CCM!!! Au unataka tutawaliwe tena???
   
 3. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa CCM wamebolonga kama Mseveni, twahitaji mbadala, wawarudisha walewale. Kazi ipo.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Ndo maana ile issue ya IOC na kadhi wanashauriwa iwe nje ya utaratibu wa kuendesha nchi. Haya mambo huwa tu nayaona madogo ila yanatugharimu sana waafrika
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hili tumeisha lisemea sana kwamba kadhi iundwe nje ya mfumo wa serikali wa mahakama na waiendeshe wenyewe waislamu na siyo kodizetu zitumike nadhani watafanya hivyo.

  ingawa kwa mawazo yangu napinga kuwepo kwa mahakama ya kadhi kwa sababu ktk nchi ambako inatumika waislamu wengi hawaitumii kwa sababu ya kughubikwa na rushwa, na wengi wana kata rufaa ambazo tena ni usumbufu kwa mahakama za serikali.
   
Loading...