Tetesi: CCM waitisha kikao cha dharura Agosti 26, 2026

Tetesi: CCM waitisha kikao cha dharura Agosti 26, 2026

CCM wameitisha NEC ya dharura keshokutwa (Jumatano), Dodoma.

Huenda kukawa mambo mapya yataibuka?
Ni nani hao kwenye NEC; siyo hao hao wanaosababisha maumivu haya?

Kuna jipya lipi watakaloweza kulizungumzia?

Nchimbi kawatisha? Kuna nani huko NEC anayeweza kumwokoa Nchimbi?

Sana sana kikao hicho, ajenda pekee ni huyo huyo Nchimbi kama kakomaza shingo.
 
Lakuzingatia neno Dharula
"Dharura"?
Hawasomi nchi inavyokwenda sasa?
Hata swala la Nchimbi siyo dharura, kwa sababu wanamtengenezea agenda wao wenyewe wanaamua lini wamfikishe wanapotaka kumfikisha.

Kama ni dharula kweli, basi kutakuwepo na watu wenye akili kidogo iliyobaki vichwani mwao kujuwa kwamba waTanzania wamechafukwa roho. Hiyo kwa hakika itakuwa ni dharula ambayo sioni kuwa wanao uwezo wa kubadilisha chochote katika kikao hicho.
 
CCM wameitisha NEC ya dharura keshokutwa (Jumatano), Dodoma.

Huenda kukawa mambo mapya yataibuka?
Hawa akina NEC; ni nani hasa jina kwa jina la kila mmoja wao.
Hawa watu inafaa tuwajue; kwa sababu wanatuamlia mambo mazito sana ndani ya nchi hii.

Mwenye orodha kamili ya wajumbe wa NEC, tafadhali iweke humu nasi sote tuwajue.

Haya mambo ya kusema NEC, huku watu wenyewe hatuwajui inapunguza uzito wa kikao cha watu hao.
 
Dah!
Aliyeasisi dharau hii ya kisheria mbele ya mahakama ni nani na hatima yake huwaje?

Halafu aliyeipakua video hii, mbona hukuifikisha mwisho ili tusikilize maelezo muhimu ya wakili?

Kulikuwa na haraka gani ya kuikatisha kwenye 'maudhui'?

Kukosa kusikiliza hadi mwisho point za wakili, nimejisikia maumivu kama yale yatokanayo na kufumaniwa ukiwa katika kilele cha tendo, au kukutwa na mama mkwe ukijisaidia haja ndogo!
 
Bahati mbaya sana hakuna yeyeto mwenye uthubutu wa kuongea au kutoa mawazo yake kwa sasa.

Wajumbe wataenda pale watalipwa posho zao, watamsikiliza mwenyekiti ajenda ya kwanza, wataunga mkono, ajenda ya pili wataunga mpaka ajenda ya mwisho zote wataunga mkono. Kikao kitafungwa, picha zitazambazwa mtandaoni.

Hakuna mwenye uthubutu wa kuongea au kutoa mawazo mbadala. Hapo ndo CCM ilipofika.
📌
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom