https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/471062-magaidi-hawa-hapa.html
Haya jamani sasa, baadhi ya picha ambazo nilizipata kwa siri sana ni pamoja na hizi hapa chini, japo hazionekani vizuri lakini sitawasaidia wale akina Tomaso wenye mashaka, hilo ni gari alilojia huyo Padri, na hapo ndo wanaondoka, huyo kijana alievaa kofia na tshirt ya kijani ni mojawapo ya makamanda hao.
Mchezo ulianza hivi, tukiwa nyumbani ibada ilifanyika kwa amani kabisa huku makamanda hao wakiwa wamelizunguka jeneza la marehemu, baada ya ibada tukaanza safari ya kuelekea makaburini, na hawa jamaa wa CCM ndo waliobeba sanduku lenye mwili wa marehemu, tulipofika Padre akaendelea na ibada ile ya mwisho sasa na mwili ukashushwa kaburini, kaburi ambalo halikuchimbwa na makamanda hawa, baada ya hapo, Padre kama kawaida ya ibada za Kikristo, ni lazima waitwe ndugu jamaa na marafiki kwa ajili ya kuweka udongo kama ishara ya kumuaga marehemu then kinachofuatia ni udongo kuwekwa ili kuchimbia jeneza.
Wale vijana wa pale mtaani na ambao ndio waliochimba kaburi wakachukua machepe/sepeto ili kufukia mwili ule kumbe kwa kanuni za makamanda hawa mwili wa kamanda unafukiwa kwa mikono na sio kwa kitu kingine chochote, hapa ndipo vuta nikuvute ilipoanza.
hata hivyo, padri alikasirika na kuondoka sehemu ya tukio lakini baada ya muda kupita na busara za wazee kutumika, alikubali kurudi na kutoa hotuba fupi kama karipio kwa makamanda wale, huku akiuliza kuwa, KAMA KURA ZA MAONI WANAFANYA VURUGU VP WATAKAPOCHUKUA NCHI? swali ambalo lilizua tena utata na kumfanya padri aweke msalaba kwene kaburi na kusema AMEN kisha kuondoka.
Hawa ndio CCM makamanda
nipo makaburini hapa mabibo_ makaburi kwenye mazishi ya mmoja wa makamanda wa ccm, ktk hali isiyo ya kawaida vijana hawa wanaonekana wavuta bangi wamemzuia pasta asiendelee na ibada wakidai watamalizia wenyewe, pasta nae amesusa ndo ameondoka sasa ivi, picha ninazo kwene simu nitatuma baada ya kuweka kwene computer, nitaleta na matukio mengine ila hawajafanikiwa kufanya vurugu hizo
Kumzuia Pastor kumaliza ibada ni vurugu tosha,tunasubiri picha kwa hamu.nipo makaburini hapa mabibo_ makaburi kwenye mazishi ya mmoja wa makamanda wa ccm, ktk hali isiyo ya kawaida vijana hawa wanaonekana wavuta bangi wamemzuia pasta asiendelee na ibada wakidai watamalizia wenyewe, pasta nae amesusa ndo ameondoka sasa ivi, picha ninazo kwene simu nitatuma baada ya kuweka kwene computer, nitaleta na matukio mengine ila hawajafanikiwa kufanya vurugu hizo
Hizo si ndio vurugu zenyewe mkuu?
Mi nikiichek hiyo avatar yako tu nakumbuka sana kombe ladunia.
Mi nikiichek hiyo avatar yako tu nakumbuka sana kombe ladunia.Hizo si ndio vurugu zenyewe mkuu?
Mkuu hizi ni vurugu za kisiasa au ni za kijamii. Sielewi kwanini unasema "CCM wafanya fujo makaburini", this is too sweeping, ungekuwa specific kidogo kama vurugu hizo zinahusiana na chama kizima, au marehemu au uchaguzi, etc.Mi nikiichek hiyo avatar yako tu nakumbuka sana kombe ladunia.
why ccm anyway? kwanini wasiwe vijana tu wavuta bangi waliohudhuria msiba ? kwanini wamebeba jina la chama...je kuhudhuria msiba wa kamanda wa ccm inatosha kuitwa mwanaccm? au kuvaa nguo za kijani msibani inatosha? je walijitambulisha kuwa ni wanaccm kabla ya vurugu?
mix with yours
acheni kuchonganisha jamani-utaprove vipi kuwa hao ni CCM? Tuwe na topic za kujenga tusipotoshe jamii
Ni makamanda wa CCM waliowekwa kambini huko Kigamboni.... wamekuja wamevaa uniform za CCM sio kuwa jina la CCM nimewapachika mkuu, siwezi kuwasingizia CCM wakati sio CCM nina report kitu live
Ni makamanda wa CCM waliowekwa kambini huko Kigamboni.... wamekuja wamevaa uniform za CCM sio kuwa jina la CCM nimewapachika mkuu, siwezi kuwasingizia CCM wakati sio CCM nina report kitu live
msimshambulie nusunusu au mumuombe radhi akileta picha. Unajua mwanao akifanya jambo baya watamtaja kuwa ni wa ukoo wako, dawa si kukanusha kila kitu kama walivyozoea sisiemu, jirekebisheni (ushauri wa bure). Mbona hata wagombea wenu walipigana jukwaani? sio ajabu hata kidogo.
Mkawakanye vijana wenu