CCM wafanya fujo makaburini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wafanya fujo makaburini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, Aug 4, 2010.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  nipo makaburini hapa mabibo_ makaburi kwenye mazishi ya mmoja wa makamanda wa ccm, ktk hali isiyo ya kawaida vijana hawa wanaonekana wavuta bangi wamemzuia Pastor asiendelee na ibada wakidai watamalizia wenyewe, Pastor nae amesusa ameondoka sasa hivi.
  Picha ninazo kwene simu nitatuma baada ya kuweka kwenye computer, nitaleta na matukio mengine ila hawajafanikiwa kufanya vurugu hizo

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/471062-magaidi-hawa-hapa.html
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hizo si ndio vurugu zenyewe mkuu?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Labda hajaelewa kati ya fujo na vugurugu
   
 4. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kumzuia Pastor kumaliza ibada ni vurugu tosha,tunasubiri picha kwa hamu.
   
 5. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hao vijana ni wana CCM ?
   
 6. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  why ccm anyway? kwanini wasiwe vijana tu wavuta bangi waliohudhuria msiba ? kwanini wamebeba jina la chama...je kuhudhuria msiba wa kamanda wa ccm inatosha kuitwa mwanaccm? au kuvaa nguo za kijani msibani inatosha? je walijitambulisha kuwa ni wanaccm kabla ya vurugu?
  mix with yours
   
 7. T

  Tiger JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mi nikiichek hiyo avatar yako tu nakumbuka sana kombe la dunia.
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu hizi ni vurugu za kisiasa au ni za kijamii. Sielewi kwanini unasema "CCM wafanya fujo makaburini", this is too sweeping, ungekuwa specific kidogo kama vurugu hizo zinahusiana na chama kizima, au marehemu au uchaguzi, etc.
   
 9. A

  Audax JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  acheni kuchonganisha jamani-utaprove vipi kuwa hao ni CCM? Tuwe na topic za kujenga tusipotoshe jamii
   
 10. T

  Tiger JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145

  :noidea: Hili swali la kwangu kweli?
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Ni makamanda wa CCM waliowekwa kambini huko Kigamboni.... wamekuja wamevaa uniform za CCM sio kuwa jina la CCM nimewapachika mkuu, siwezi kuwasingizia CCM wakati sio CCM nina report kitu live
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Wakuu wenzangu, kilichinipelekea kuwaita ni CCM ni kwa sababu walijitambulisha hivyo , huku wakiwa wamevalia sare za CCM na nina mfahamu marehemu kuwa ni mwana CCM na hata ugonjwa ulimzidia akiwa Kambini, na kama huna habari ujue ndo hivyo CCM wana kambi za vijana...wanachofundishwa hakijulikani, na kubwa zaidi ndo waliobeba jeneza/ sanduku la marehemu hadi makaburini...he hehe heee, sidhani kama kuna sababu ya msingi ya kuwaita jina lingine wakati wameshajitambulisha hivyo,,,,sina ugomvi na CCM na wala wanaCCM nina ripoti tu kilichotokea
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280

  Heheeee, nashukuru MUNGU sijawahi kuchonganisha na sitakaa nichonganishe, hivi mtu akija kwenye shughuli yako tena na magari mawili yamewabeba wanaCCM hao, wakajitambulisha kwa nguo na kwa maneno na matendo, uthibitisho zaidi ya huo ni upi?? Labda ulitaka watoe kadi waonyeshe kuwa sisi ni CCM. I think and believe kuwa hata huo ni utambulisho tosha.....Hapo je?
   
 14. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mwanzoni hukusema kama wana mavazi ya CCM ila ulisema ni wavuta bangi.
   
 15. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mkuu hizo kambi zao kikubwa ni jinsi ya kufanya rigging kwenye uchaguzi. Uchaguzi nao unahitaji watu kuwekwa kambini?
   
 16. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kama unao ushahidi tuma hizo picha maana unatuchanganya.
   
 17. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  Haya jamani sasa, baadhi ya picha ambazo nilizipata kwa siri sana ni pamoja na hizi hapa chini, japo hazionekani vizuri lakini sitawasaidia wale akina Tomaso wenye mashaka, hilo ni gari alilojia huyo Padri, na hapo ndo wanaondoka, huyo kijana alievaa kofia na tshirt ya kijani ni mojawapo ya makamanda hao.

  Mchezo ulianza hivi, tukiwa nyumbani ibada ilifanyika kwa amani kabisa huku makamanda hao wakiwa wamelizunguka jeneza la marehemu, baada ya ibada tukaanza safari ya kuelekea makaburini, na hawa jamaa wa CCM ndo waliobeba sanduku lenye mwili wa marehemu, tulipofika Padre akaendelea na ibada ile ya mwisho sasa na mwili ukashushwa kaburini, kaburi ambalo halikuchimbwa na makamanda hawa, baada ya hapo, Padre kama kawaida ya ibada za Kikristo, ni lazima waitwe ndugu jamaa na marafiki kwa ajili ya kuweka udongo kama ishara ya kumuaga marehemu then kinachofuatia ni udongo kuwekwa ili kuchimbia jeneza.

  Wale vijana wa pale mtaani na ambao ndio waliochimba kaburi wakachukua machepe/sepeto ili kufukia mwili ule kumbe kwa kanuni za makamanda hawa mwili wa kamanda unafukiwa kwa mikono na sio kwa kitu kingine chochote, hapa ndipo vuta nikuvute ilipoanza.

  hata hivyo, padri alikasirika na kuondoka sehemu ya tukio lakini baada ya muda kupita na busara za wazee kutumika, alikubali kurudi na kutoa hotuba fupi kama karipio kwa makamanda wale, huku akiuliza kuwa, KAMA KURA ZA MAONI WANAFANYA VURUGU VP WATAKAPOCHUKUA NCHI? swali ambalo lilizua tena utata na kumfanya padri aweke msalaba kwene kaburi na kusema AMEN kisha kuondoka.

  Hawa ndio CCM makamanda
   
 18. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  msimshambulie nusunusu au mumuombe radhi akileta picha. Unajua mwanao akifanya jambo baya watamtaja kuwa ni wa ukoo wako, dawa si kukanusha kila kitu kama walivyozoea sisiemu, jirekebisheni (ushauri wa bure). Mbona hata wagombea wenu walipigana jukwaani? sio ajabu hata kidogo.
  Mkawakanye vijana wenu
   
 19. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Asante mpwa, hope nimesomeka sasa, sorry kama jina la wavuta bangi limekusumbua kidogo ila ndo hivyo.... thanks
   
 20. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Hivi kumbe ni wale wale wa THITHIEMU eehh, asante kwa kuniambia
   
Loading...