CCM waanza kutumia silaha za moto Arusha [kampeni za udiwani]

Movement

Member
Mar 24, 2012
58
15
Wanabodi,

Katika kile kinachoendelea kuonyesha ni kushindwa vibaya kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani unaoendelea kwa sasa kwenye kata ya bangata arumeru magharibi, kampeni meneja wa ccm bwana bosco eduad saimoni ametoa silaha ya moto mean bastola na kumtishia kijana wa chadema aliyekuwa akitangaza matangazo ya mkutano wa hadhara, ndipo alipotokea bwana bosco na kuziba barabara kwa kutumia gari aina ya rav4.

Chakushangaza baada ya mtuhumiwa huyo kuwekwa chini ya ulinzi na vijana wa chadema kisha kamanda kilewo na makamanda wengine kama diwani gibson wa kachukua hatua ya kupiga simu polisi kwa ocd wa usa, baada ya hapo polisi waliwasili na kumchukua mtuhumiwa huyo na kuchukua bastola na kumpeleka kituo cha usa, ila baada ya masaatakribani manne tu, mtuhumiwa huyo aliachiwa huru jana siku ya jumapili.

Je sheria hapa inasemaje kwa mtuhumiwa kuachiwa huru bila uchunguzi wa kina kufanyika, wananchi wakimuona mitaani wakiamua kuchukua sheria mikononi nani wa kulaumiwa?

Ocd usa kiukweli anatumika na hawa magamba, cdm endeleezeni uimara wenu huwo huwo wakutoongopa vitisho vya jeshi la polisi kutumiwa na magamba.
 
Wanabodi.
Katika kile kinachoendelea kuonyesha ni kushindwa vibaya kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani unaoendelea kwa sasa kwenye kata ya bangata arumeru magharibi, kampeni meneja wa ccm bwana bosco eduad saimoni ametoa silaha ya moto mean bastola na kumtishia kijana wa chadema aliyekuwa akitangaza matangazo ya mkutano wa hadhara, ndipo alipotokea bwana bosco na kuziba barabara kwa kutumia gari aina ya rav4.

Chakushangaza baada ya mtuhumiwa huyo kuwekwa chini ya ulinzi na vijana wa chadema kisha kamanda kilewo na makamanda wengine kama diwani gibson wa kachukua hatua ya kupiga simu polisi kwa ocd wa usa, baada ya hapo polisi waliwasili na kumchukua mtuhumiwa huyo na kuchukua bastola na kumpeleka kituo cha usa, ila baada ya masaatakribani manne tu, mtuhumiwa huyo aliachiwa huru jana siku ya jmapili,je sheria hapa inasemaje kwa mtuhumiwa kuachiwa huru bila uchunguzi wa kina kufanyika, wananchi wakimuona mitaani wakiamua kuchukua sheria mikononi nani wa kulaumiwa? Ocd usa kiukweli anatumika na hawa magamba, cdm endeleezeni uimara wenu huwo huwo wakutoongopa vitisho vya jeshi la polisi kutumiwa na magamba.

Ngoja tumalize pilikapilika za mazishi ya Libe.
Naona ni muda muafaka kuhamia A town.
 
Poilisi wa Tanzania wanahitaji maombi ya Ukombozi! Wanatia huruma, hawajifunzi wanatumiwa kama makalai ya zege na CCM.
 
Nilishasema Kadi ya CCM ni kiharalisho cha maovu, hakuna sheria iliyotumia zaidi ya UKADA WA CCM.
 
Naamini kuna wakati wataona hata hizo silaha hazina kazi,Makamanda wa Arumeru Magharibi wasimame imara na wasikubali kutishwa na yeyote na hakuna Umma ulikowahi kushindwa.Haki haiwezi kushindwa na dhuluma hata siku moja.Watabebana lakini mwisho watarejea ulingoni na ukweli utathibitika vi SANDUKU LA KURA.
 
Waliwakodi CUF walizani wataichanganya CDM matokeo yake moto chini sasa wanatia aibu jeshi linazidi kuchafuka kwa matendo dharimu hawajifunzi kwa Mwangosi Iringa? Sikio la kufa, sasa nimekubali wakati wa Mungu umefika watu lazima wakombolewe, utukufu wa Mungu hakuna wa kuuzuia.
 
Poilisi wa Tanzania wanahitaji maombi ya Ukombozi! Wanatia huruma, hawajifunzi wanatumiwa kama makalai ya zege na CCM.

Kumbe raia nao waweza kuua POLICCM? PoliCCM wakiua msoma magazeti kama walivyofanya Moro, Wananchi wanaua RPC kama walivyomfanya Kamanda Libe. Baadae wataua Kamanda CHAGONJA, Na wataendelea ili kuona "nani zaidi"
 
Jamani kwani uchunguzi lazima ufanyike akiwa ndani?
Na inawezekana kabisa hao polisi wamefanya uchunguzi na kugundua kuwapo kwake nje (most probably kwa mdhamana) hakutaathiri usalama wake.
Ila wewe kama raia mwema unafahamu njama zozote za kumdhuru pindi atakapoonekana ni vyema ukawasilisha ripoti hizo kuto cha polisi kilicho karibu nawe ili uweze kunusuru uhai wa binadamu mwenzio.
Las ivyo, nadhani wewe ni mchochezi tu baina ya jamii na polisi.
Jamani, hali iliyopo tu haitoshi mpaka uharibu zaidi!??
 
Ukweli husemwa:

Kwanza rekebisha heading ya thread yako kwa sababu matendo ya mtu mmoja wa CCM hayawezi kukihukumu chama chote. heading yako imebeba mawazo kama ya wale jamaa mbagala walioamua kuwahukumu wakristo wote kwa matendo ya kijinga ya kijana mmoja.

angalau ungeandika '' kiongozi wa CCM atumia silaha ya moto Arusha'
 
Je kwenye kundi lile la vijana wa CDM kama kungekuwa na mwenye bastola naye aichomoe,Ingekuwaje hapo?
 
Back
Top Bottom