Lupyeee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 2,683
- 2,820
Kwa jinsi mikito ya kisiasa inavyoenda sasa hivi, mtu yoyote makini anaweza kutabiri upepo wa kisiasa utakavyokuwa kwenye uchaguzi kwa ngazi zote mwaka 2020.
Kwa sasa ccm wanajitahidi kadiri ya uwezo wao kupambana na rushwa,ufisadi na madawa ya kulevya kwa nguvu zao zote.
Elimu bure, serikali kuhamia dodoma na kufufuka kwa Atcl pamoja na kuboreka kwa bei ya mazao ya biashara kwa wakulima kama vile pamba na korosho ni baadhi ya mambo yanayotoa mwanga kwa ccm kuendelea kutamba na kuaminiwa na wananchi zaidi mwaka 2020.
Kwa upande mwingine Chadema wanajaribu kuwinda na kuvutia wanachama wapya kwa kutetea wakwepa kodi, wala rushwa, mafisadi na wauza madawa ya kulevya.
Chadema wanajaribu kujibanza nyuma ya wafanyabiashara, kwamba ikishinda chadema, biashara zao zitaboreka ,pia licha ya kwamba chama hakina hata ofisi, chadema wameahidi wanafunzi watasoma bure mpaka chuo kikuu.
Kwa hali hiyo chadema pia inatoa mwanga wa kutamba mwaka 2020 kupitia uungwaji mkono wa makundi yanayoshugulikiwa vizuri na utawala wa awamu ya tano.
Makundi kama ya wauza madawa ya kulevya, mafisadi, wala rushwa, wazembe kazini, wakwepa kodi, kwa sasa hawana nafasi ccm, hivyo watakimbilia chadema na kuipa matumaini ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2020.!!!
Wewe kwa maoni yako nani atatamba 2020??