CCM vs CHADEMA:Kipi ni chama cha mafisadi?

Mbona mnawaonea sana ccm wamewakosea nn.. kwa sababu watu waliopo ccm ndo wapo mtaani tunaishi nao
 
Niseme CCM ni chama nambari wani duniani kwa kufuga watu waovu na wasiofaa katika ujenzi wa taifa letu Tanzania

CCM wamepoteza dira kabisa na hawana hoja za kujitetea pale mbunge/mwanachama wao anapojiondoa na kusema madhaifu yote ya chama

CCM imekua na utaratibu wa kuibua kashfa za ufisadi,wizi wa Mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka kwa mbunge/mwanachama wake anayekipa kisogo chama hicho

Lowassa alipohama CCM na kujiunga na upinzani wakamshambulia kwa vijembe na maneno ya kwenye khanga,eti chama hakiwezi kumpitisha fisadi kuongoza nchi,cha ajabu mwenyewe kawaambia hao CCM kama MNA ushahidi nipelekeni mahakamani ,hawajafanya hivyo hadi Leo

Juzi juzi kaondoka Lazaro Nyalandu ambaye alikua mbunge na mwanachama hai wa CCM wameanza kutoa povu Mara jamaa kaondoka kisa kanyimwa uwaziri,mara arudishe twiga wetu yani mambo mengi nonsense ambayo Nyalandu hakuyafanya kwa matakwa yake bali maagizo ya viongozi wake ndani ya chama juu ya hao twiga na dhuluma nyingine

CCM kumejaa wajinga ndo mana hata kujibu hoja za Nyalandu wameshindwa ,walichobaki ni kuongea porojo na maneno ya kwenye khanga na kushindwa kabisa kujitetea dhidi ya hoja madhubuti za Nyalandu

CCM kuna wala rushwa wengi na hakuna mwenye nia ya kuondoa rushwa kwa sababu viongozi wenyewe wakuu ni wala rushwa,mafisadi na wabadhirifu wa Mali za umma

Kwa mtindo huu wa CCM kumshambulia mtu anayehama chama kwa kutaja madhambi yake basi inaonesha ndani ya CCM hakuna msafi kuanzia Mwenyekiti wao hadi wana chama wengine.

Kitendo cha kukaa kimya wakati mwanachama yupo ndani ya chama na kushindwa kutaja maovu yake akiwa ndani ya chama na kuyataja pale tu anapokihama chama hicho basi hii ni kiashiria CCM wote ni wezi,mafisadi,wala rushwa

Shida zote za nchi hii chanzo ni CCM ,walisaini mikataba ya kilaghai na wazungu kuhusu madini CCM ikishirikiana na wazungu wameibaaaa weee madini yetu saa hivi yamebaki mashimo linatokea jitu moja nafiki la CCM na kujifanya kusema tumeibiwa sana wakati ye mwenyewe alikuwepo wakati wanasainishana hiyo mikataba mibovu,halafu saa hivi wanataka kujifanya hawajui na kutuona watanzania ni wajinga

CCM kumejaa wajinga wao kila kitu ndio hata kama kina madhara kwao na kwa kizazi chao mfano upitishaji wa sheria mbovu zisizo na tija huu ni ujinga wa wanaCCM

Tusitegemee mabadiliko na maendeleo ya nchi chini ya CCM na Magufuli ni ndoto CCM ni ile ile Magufuli hawezi kuondoa rushwa wala mafisadi kwa sababu chama chake ndo wamejaa watu hao hao,ni WAJINGA pekee wenye imani na CCM na Magufuli wao

OVA
 
Back
Top Bottom