CCM vs CHADEMA:Kipi ni chama cha mafisadi?

CCM vs CHADEMA:Kipi ni chama cha mafisadi?

Siku za nyuma ilikuwa ni wazi kabisa kuwa CCM kilikuwa ni chama cha mafisadi,wezi wa mali ya nchi hii.Orodha ya mafisadi iliyotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mwanasheria wa chama Dr Slaa na Tundu Lissu kwa mpangilio ilikoleza ufisadi wa CCM.
Mchakato wa uchaguzi mkuu ulimtoa mmoja wa waliotajwa kwenye orodha kutoka CCM na kwenda CHADEMA.Huo ulikuwa ni mwanzo wa debate,kwamba ni chama kipi cha mafisadi? Mpaka sasa makada wa CCM wanawaona CHADEMA kama mafisadi kwa uwepo wa huyo mtu na kujaribu kuhamisha magoli!!
Kuondoa mzizi wa fitina,lazima namba zitumike kwa kutumia ileile orodha ya aibu ya Dr.Slaa ambayo wanaCCM ndio wanaitumia zaidi kuwashambulia CHADEMA.
  • Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu, Dk. Daudi Balali (CCM)
  • Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM)
  • Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM) na Waziri
  • Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina (CCM)
  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa(CCM)
  • Nazir Karamagi aliyewahi kuwa Mbunge(CCM)
  • Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM)
  • Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM)
  • Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CHADEMA)
  • Rais mstaafu, Benjamin Mkapa(CCM)
  • Rais wa Sasa, Jakaya Kikwete(CCM)
Kwenye orodha ya mafisadi 11 waliotajwa na Dr Slaa pale Mwembeyanga,kwa sasa CCM inao 9(+mareh.Balali!!) ilhali CHADEMA wanaye mmoja tu.Kama hii orodha ndio kigezo na kama kweli kila aliyetajwa alikuwa fisadi,ni wazi CCM bado wana kazi kubwa ya kuhusu ufisadi nchini.

mytake:Tumuunge mkono kila anayepiga vita ufisadi wakiongozwa kwa sasa na mh.JPM bila kuwabeza wapiga kelele kama Tundulisuu
Mbaya kushinda wote ni anayezalisha mafisadi
 
Kulinganisha ufisadi ndani ya ccm na chadema sawa na kulinganisha mashetani na malaika.
 
Kuna chama kati ya hivyo viwili, kina mamlaka ya kukamata na kufunga mafisadi wa ndani ya chama chenyewe, na nje ya chama yaani kwenye vyama vingine. Kiulizeni kimeshindwa nini kufanya hivyo. Hapo ndipo tatizo lilipo. Mnatupotezea tu muda na majadiliano yasiyokuwa na msingi lakini tatizo lilipo nyie wote mnalijua.
 
Habari wanajf!

Kutokana na wimbi la kuongeza kwa wala rushwa na mafisadi Tanzania, ningependa tujadili aina hii ya watu wanazalishwa wapi na kwa nini?

Karibuni
 
Habari wanajf!

Kutokana na wimbi la kuongeza kwa wala rushwa na mafisadi Tanzania, ningependa tujadili aina hii ya watu wanazalishwa wapi na kwa nini?

Karibuni
Kiwanda cha kuzalisha mafisadi Tanzania ni ccm, Lumumba na dodoma kwa sababu ni wavivu wa kufikiri njia bora ya kukuza uchumi
 
CCM yanazaliwa nakukua,yakipata hela yanaenda Chadema yanatoa fee kidogo ya kusafishwa,mara nyingi huwa ni 5% ya ufisadi waliofanya
 
Habari wanajf!

Kutokana na wimbi la kuongeza kwa wala rushwa na mafisadi Tanzania, ningependa tujadili aina hii ya watu wanazalishwa wapi na kwa nini?

Karibuni
CCM ndiyo kiwanda cha kuzalisha mafisadi Tanzania kwa kuwa wao ni chamadola.Chadema wanalea watuhumiwa wa ufisadi
 
CCM bila shaka yaani huko kuna mafisad yameifisad hii nchi an nchi inakonda yenyew yanavimbiana matumbo kama yapo leba hv
 
Ccm bingwa kuzalisha mafisadi na wanalindana kwa nguvu
 
Back
Top Bottom