CCM, Ufalme ukifitinika kamwe hauwezi kusimama tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, Ufalme ukifitinika kamwe hauwezi kusimama tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOZERDTEN, Aug 11, 2011.

 1. D

  DOZERDTEN New Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maandiko matakatifu yalishasema tangu kuumbwa kwa ulimwengu kuwa"Ufalme ukifitinika hausimami", CCM yametimia!dalili zote zimeonekana!nazo ni:

  Kwa uchache, Viongozi kupenda fedha(ufisadi) kuliko Mungu na watanganyika wenzao, kugombana wenyewe kwa wenyewe, kutukanana matusi makubwa hadharani, Wabunge kusaliti chama chao CCM ambako ni sawa na abiria kutoboa boti wanalosafiria kwenye ziwa lenye mamba,makada kuanzisha CCJ ndani ya CCM ambako ni sawa na kuvaa bomu katikati ya watoto wako, kutumia nguvu kuzima fikra zenye hekima, mtu mmoja kuitisha serikali na bunge,.... n.k

  Watanganyika tuamke saa ya ukombozi imefika!
   
 2. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Unachosema ni kweli, tatizo liko kwetu wenyewe maneno mengi kazi yetu tz tunalialia sana utendaji hakuna. Haya mambo yanayotokea hapa Tz ingekuwa nchi jirani kama Zambia, Kenya, Malawi ccm ingekuwa ni historia tu. Tambua kuwa ccm tusipoiondoa sasa hivi hii Tz itakuwa kama Somalia. Angalia zaidi ya nusu ya nchi yetu kuna njaa kali (Manyoni ni zaidi) lakini umesikia tamko lolote la serikali? Kilakitu sisi hovyo, hawa CCM hawana uzalendo kabisa. NAUMIA SANA. MUNGU TUSAIDIA CCM IFE.
   
 3. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hakuna namna wananchi wataufaidi uhuru kama ccm itaendelea kuwa madarakani kimetesa sana watu ,wamechoka hamna matumaini sababu ni ccm huyu rais amekosa mvuto kwa wananchi ,hakuna kipaumbele kilichofanikiwa nh mbaya sana kwa taifa si kwamba chadema ndio mbadala wa kutatua matatizo ya hii nchi ila wanaonekana wanaweza kutusogeza tulipo kuiona nuru ya mafanikio!
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Katika Maandiko Matakatifu ya Injili ya Luka

  Yesu alikuwa akitoa pepo na Baadhi ya watu wakasema kwamba "Atoa pepo kwa Beelzebuli" (Belzeebuli nalo ni Pepo a.k.a Shetwani a.k.a Jeen). Na Yesu akijua Mawazo yao akaambia kwamba kama "Yeye anatumia Pepo kutoa Pepo Ina Maana Ufalme wa Mapepo ( Mashetani) umefitinika maana Pepo hupenda liishi ndani ya mtu sasa ikiwa kuna pepo lingine linamtoa pepo Mwenzake ndani ya Mtu huo Ufalme Umefitinika Wenyewe kwa Wenyewe na Kamwe hauwezi kusimama"

  Tumeona jinsi CCM inavyofitinika yenyewe kwa Yenyewe.

  Wana CCM wakituhumiana kwa Ufisadi na kutoleana Mwito wa Kujivua Gamba, tumeona ya Lowasa, Chenge, Rostam na sasa Msekwa naye anaambiwa na wana CCM wenzake kwamba ni Gamba, Wengine wanasema Mkuu wa Kaya naye ni Gamba, Wengine wanasema Mzee makamba alikuwa Gamba naye anasema ndani ya CCM kuna Magamba.

  Tumeona Pinda ( Kiongozi wa Serikali Bungeni na Bosi wa Ngeleja) alisema kwamba kama angeweza angemfukuza Kazi Jairo lakini jana tumeona namna Jairo alipogeka kuwa Shujaa na kusukumwa na Wafanyakazi wake Kupongezwa na Ngeleja na kulifanya Bunge zima pamoja na Waziri Mkuu Kuonekana Vidampa tu. Haya yote yanatokea ndani ya Serikali moja ya CCM.

  Hakika Ufalme wa CCM Umefitinika ka Kamwe hautakaa Usimame
   
 5. H

  Honey K JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chadema, sasa kwa hakika ni ufalme uliofitinika ambao kwa mujibu wa Biblia hauwezi kusimama tena! Hakika UTASAMBARATIKA!(Mnaweza kunitukana mtakavyo,lakini kadri Mungu wangu aishivyo,ufalme huu LAZIMA utasambaratika)!

  Ugomvi mkubwa uliopo kati ya wakubwa watatu na wapambe wao yaani Mbowe, Zitto na Dr. Slaa ni uthibitisho tosha kuwa ufalme wa Chadema umefitinika!

  Mgogoro mkubwa sasa ndani ya Bavicha kiasi cha kuvuana nguo hadharani mpaka mapesa anayolipwa Heche na upuuzi wa kina Ben na Makam/mkiti wa Bavicha! Umeiacha Bavicha vipande viwili vikubwa.Huu ni ufalme uliofitinika! Hakika haiutasimama!

  Mpango ulioiva wa kumfukuza Shibuda na wenzake ni ushahidi tosha Ufalme umefitinika!
   
 6. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  dua la kuku halimpati mwewe....
   
 7. tameer

  tameer JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 703
  Trophy Points: 180
  Wanakuja,jiandae
   
 8. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  lete hicho kipengele kwenye biblia siyo kutuletea umbea hapa
   
 9. tetere

  tetere JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 962
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kwani ni lazima kila wazo linaloibuka kichwani mwako ni thread? CCM mbona haijafa na ina migogoro kibao??
  Migogoro iko vatican mbona vatican haijafa??Migogoro ni mizuri na ndio inayofanya watu wajipange. Na pia koma kutumia Bible kwenye hoja nyepesi kama
  hizi.
   
 10. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Mfikishie huu ujumbe, wakati anaandika hii thread alikuwa amebandika kichwa cha Nyau chake alikiacha Chooni.
   
 11. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  unaakili kama Matola wa jf.
   
 12. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Upuuzi wa taifa hili kwa watu wanaoishi mijini ni kwamba kila mtu amekuwa kwenye nafasi ya kutoa "uchambuzi" kiasi hadi cha neno uchambuzi limepoteza maana!
   
 13. t

  tenende JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CCM mene mene mene tekeli na peresi!.. Ufalme wako umepimwa na kuonekana haufai!... Wanyama wanaibiwa na CCM, pembe za ndovu zinauzwa china na ccm aka jangili! Nape katibu mwenezi wa CCJ na CCM!, Mwakyembe, na Sita! Wako CCM na CCJ inayojiita CCK!.. Chenge na LOWAsa magamba, msafi nani?! ..JANGILI!
   
 14. Django

  Django JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2013
  Joined: Apr 15, 2013
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  BAADHI ya mafarisayo walipomtuhumu Bwana Yesu kwamba anatoa pepo kwa uwezo wa Mkuu wa pepo, yaani Belizebuli, aliwaambia kuwa utawala unaofitinika wenyewe kwa wenyewe hauwezi kusimama.

  Alitaka kumaanisha kwamba, haiwezekani mamlaka moja ikawa na matokeo yanayokinzana, halafu ikaendelea kuwa moja, yaani kuwa na pepo wanaowavuruga watu halafu kuwa na nguvu ya kuwaondoa na kuwafukuzia mbali pepo hao, nguvu hizi haziwezi kukaa pamoja.

  Nimelazimika kuanza na mfano huu ili kueleza hali ilivyo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa, tofauti zilizomo ndani ya chama zimekisaidia kujenga nyufa ambazo zinasababisha wanachama na viongozi wake mbalimbali kufitiniana wao kwa wao kwa kiwango cha ajabu.

  Chama chochote tunaambiwa, ni mkusanyiko wa watu wenye itikadi moja na malengo yanayofanana, wananchi hawa wanaweza kutofautiana kwa namna ya kuyafikia malengo yao na hata jinsi ya utekelezaji wa kile wanachokiamini pamoja.

  Lakini cha msingi zaidi ni kutoruhusu tofauti hizo kuwagawa mpaka kwenye malengo ya msingi, ikitokea hivyo chama hicho kinabaki kikundi tu cha watu ambao hata ukiwauliza wanataka nini na kwa nini wako pamoja, hawawezi kukupatia jibu la uhakika.

  Chama siyo jina au kusanyiko la watu tu, hivyo ni vitu vya ziada sana, uhai wa chama ni itikadi inayowaunganisha wanachama, ni lazima wawe na kitu muhimu na cha maana kinachowaunganisha. Kama wanaungana kwa sababu ya kuungana tu au kwa sababu ya maslahi hiyo, ni zaidi ya hatari kwa uhai wa chama hicho.

  Ni ukweli ulio wazi kwamba tofauti za wana CCM sasa zimefikia kiwango cha kugusa malengo ya msingi ya chama hicho na hapa ndipo hatari kwa mustakabali wa chama hiki ilipo.

  Wenyewe wanasisitiza kwamba lengo kuu ni kuchukua Dola. Inaonekana sasa wametimiza malengo yao, hivyo wanataka kuvuna kutokana na kuwa katika madaraka. Lakini kumbukumbu zinatuambia kwamba malengo ya msingi ya awali ya CCM ile iliyopotelea tusikokujua yalikuwa na kumkomboa Mtanzania kutoka katika unyonge uliomfanya kuonewa, kunyanyaswa na kuteswa.

  Kuondoa unyonge wa maradhi, ujinga na umaskini ndiyo yalikuwa malengo ya msingi ya CCM hapo awali, ambacho kilizaliwa ili kuleta ukombozi huo. Na kwa kuwa wazazi wake TANU na ASP waliasisiwa ndani ya ukoloni, ndiyo maana wakapigania uhuru kwa nguvu zote.

  Malengo, hata hivyo hayakuwa uhuru kama uhuru, ilikuwa uhuru upatikane ili tuwe na mamlaka yetu wenyewe ambayo yatatuwezesha kupanga namna ya kujikomboa kutoka katika unyonge wetu kama taifa.

  Ndiyo maana baada tu ya uhuru, maadui waliotangazwa walikuwa ni wale wale ambao ndiyo kiini cha unyonge wetu kama taifa. Hawa ni ujinga, umaskini na maradhi. Hawakutangazwa kwa bahati mbaya, yalikuwa ni malengo ya msingi ya kuanzishwa kwa TANU.

  Ndiyo maana hata misingi yake ililenga kuyatekeleza haya. Usawa wa binadamu ndiyo ulikuwa msingi wa kwanza ili kuwawezesha watu kuthaminiana wao kwa wao na kuondoa tofauti zao ili waweze kukusanya nguvu zao kwa msingi kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

  Kusema kweli daima na fitna mwiko, kutumia cheo kwa manufaa ya umma, kujiendeleza kwa kadri ya uwezo kwa ajili ya manufaa ya jamii nzima na zaidi sana rushwa ni mwiko, kutotoa wala kupokea rushwa.

  Haya ndiyo yaliyoifanya CCM iwe ilivyokuwa, maadili ya viongozi yalitaka kuwafanya viongozi watambue kwamba wanapokuwa katika dhamana wanakoma kuwa watu binafsi, wanakuwa taasisi na wenye wajibu mkubwa zaidi kwa jamii kuliko watu wengine kwa sababu wameaminiwa na kupewa majukumu ya kuongoza njia.

  Hapa kilipo leo CCM kimetupa misingi yote iliyokianzisha na badala ya vyeo kuwa dhamana, sasa ni dili na mitaji ya watu. Ugomvi na mivutano yote tunayoiona, vijana kuwakosea adabu wazee wao, wazee kwa wazee kukoseana adabu hayatokani na kitu kingine chochote, isipokuwa uroho na tamaa ya madaraka.

  Uongozi katika Tanzania sasa ni moja ya biashara nono na kubwa zinazolipa bila jasho, kuwa kikaragosi wa kiongozi fulani kunakufanya na wewe kuwa bosi wa vikaragosi wenzako. Ndiyo maana tunaona watu ambao tulitambua wana akili na uwezo wa kujisimamia, ghafla wanakuwa na akili za kushikiwa.

  Wanafanya kitu siyo kwa sababu wanaamini katika kitu hicho, isipokuwa kwa sababu anayewalipa ndivyo anavyotaka, wamejigeuza vinubi ambavyo mpigaji wake analazimika kuimba wimbo chaguo la aliyemlipa na kwa sababu ya njaa na upofu wa tamaa ya ukwasi wa haraka, wanaimba hata nyimbo ambazo ni marufuku kwenye jamii yao.

  Tunaambiwa wapo baadhi yao ambao wametambua makosa yao ya kuwachafua wenzao na wamejirudi, wamekwenda kuomba radhi au wengine wanajuta kwa nini walijiingiza huko, lakini hiyo ndiyo kawaida ya majuto huja baadaye, mambo yakishakuwa yeshaharibika.

  Haya yote maana yake ni dalili za kukosa kitu kinachowaunganisha kwa dhati ya itikadi zao, chama sasa kinaonekana ni kundi kubwa la watu wenye malengo tofauti na tofauti zake ni kama giza na nuru. Kundi moja liko tayari kuliharibia au hata kudhuru kundi jingine kwa gharama yoyote ili mradi lisiwaharibie.

  Chama sasa kimeligeuza taifa kama mpira wa gombania goli, kila mtu anataka afunge yeye, kwa sababu goli la mtu mwingine yeye halimsaidii hata kama ni mwanachama mwenzake, badala yake linaweza hata likamletea shida kubwa.

  Ndiyo maana hakuna uchezaji wa kitimu, hakuna kupeana pasi kwa wachezaji wa timu moja, badala yake wanalambana buti wao kwa wao. Mpira akiupata winga wa kushoto anamgeukia beki kulia wa timu yake, anamlamba chenga na kumchungulia alipo mlinda mlango wake ili atikise nyavu na akifunga anashangilia kuliko hata timu pinzani.

  Huyu beki naye akipata mwanya wa kumdhibiti winga wa timu yake anahakikisha akimchapa buti siyo ya kugugumia tu na maumivu kidogo, halafu arudi uwanjani, anamkata buti itakayompeleka nje ya uwanja kwa wiki kadhaa au hata ikibidi ‘kwa msimu’ mzima wa ligi.

  Hiki ndicho kiwango cha kufitinika kwa wana CCM wa leo, wamekuwa maadui wao kwa wao zaidi kuliko hata walivyo na vyama vingine. Bila shaka unaweza ukamwita mtabiri, lakini kwa aina ya mtu aliyekiasisi chama na kukilea, Mwalimu Julius Nyerere, alijua wazi kwamba chama kimezika misingi iliyokuwa inakifanya kisimame, ndiyo maana aliona dalili za anguko lake mapema.

  Ingawa wenyewe wanafarijiana kwamba migogoro na kutofautiana ni sehemu ya ukomavu wa demokrasia na kwamba migogoro ndani ya chama haijaanza leo, ni kweli hayo yote ni sahihi, lakini kwa hali ilivyo sasa, kama hakutatafutwa mbinu mpya inayokwenda na mahitaji ya mazingira ya sasa ya hali halisi ilivyo ndani ya CCM na kumpata kiongozi jasiri kwa maana halisi ya neno jasiri, kukemea na kuchukua hatua kali, ngumu na nzito kukihuisha chama, hali ya chama siyo nzuri.

  Sipendi kuwapa wana CCM matumaini na faraja za hewani, bila hatua za namna hiyo, hali ya kufitiniana ndani ya chama chao zina kila dalili za kuashiria mwanzo wa mwisho wa chama chao, la waamue kuchukua hatua za haraka na za makusudi kukinusuru.
   
 15. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2013
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mada za namna hii zimepitwa na wakati, jana ilikuwa kwenye gazeti la Mtanzania.
  Shame on you.
   
 16. M

  Maswala JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2013
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 561
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Habari hii iliyochapishwa katika gazeti na Tanzania Daima Jumapili 13/10/2013 inayasema ni sawa na maneno ya Yesu Matt. 12:25-26, "Every kingdom divided against itself will be ruined, and every city or household divided against itself will not stand."

  Naagalia barabara nyingi zimejengwa na hata kuna mambo mengi CCM wamefanya lakini kila wakijitahidi kuyanadi, hayanadiki. Kweli CCM mwisho wake umefika, ni ufalme uliofitinika.

  Soma Zaidi habari hii uone mikinzano hii ya hivi karibuni:

  SERIKALI INAKUFA

  na Josephat Isango-

  HALI ya utendaji ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), si shwari kutokana na mawaziri, manaibu wao na watendaji wengine kufanya kazi kwa visasi, chuki na kutoaminiana, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.

  Kutoaminiana huko na utendaji wa kusuasua kunaelezwa ni dalili za kufa kwa serikali hiyo iliyodumu madarakani kwa muda usiopungua miaka 35.

  Wakizungumza na Tanzania Daima Jumapili, wasomi, wanasiasa na wadau mbalimbali wameshtushwa na uendeshwaji wa serikali ambapo kila mtendaji huamua au kutoa kauli kwa utashi binafsi.

  Miongoni mwa mambo yanayoelezwa kutia hofu ni kupingana kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli juu ya uzito unaoruhusiwa kwa wasafirishaji wa mizigo ya ndani na nje.

  Hata hivyo Waziri Mkuu Pinda, aliufuta uamuzi huo huku akitaka watendaji wa serikali kuacha kutoa uamuzi bila kuwashirikisha wadau wa sekta husika.

  Ingawa Pinda hakumtaja Waziri Magufuli kuwa ni mbabe, lakini mara kwa mara amekuwa akitajwa kufanya uamuzi unaokiumiza chama, wananchi na serikali yake.

  Waziri Magufuli alitangaza kufuta msamaha wa asilimia tano uliokuwepo kwa magari yanayozidisha mzigo unaotakiwa katika mizani mbalimbali za hapa nchini, akisisitiza anasimamia sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ya 2001 na kanuni zake.

  Kanuni hizo zinataka malori kutozidisha uzito ghafi ambao kwa Tanzania ni tani 56 na endapo itatokea gari limezidisha basi usizidi asilimia tano ya unaotakiwa.

  Uamuzi huo uliwafanya wamiliki wa malori nchini kupitia chama chao, TATOA, kugoma na hivyo kusababisha mizigo kukwama kuingia na kutoka jijini Dar es Salaam sambamba na bandari kuelemewa.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana alisema yanayofanyika ndani ya serikali yanatokana na ulegevu unaosababishwa na wachambuzi wa sera na sheria za nchi kufanya kazi hiyo chini ya kiwango.

  Alisema tatizo la mawasiliano kutoka idara moja hadi nyingine linamaanisha kifo cha utawala unaofanya kazi kwa mazoea.

  “Hata sisi tulioko nje ya wigo wa serikali suala hili linatupa tabu sana, sheria ni ya serikali inapotungwa, Bunge linakuwa limeitunga na serikali kazi yake ni kuitekeleza.

  “Inashangaza tunawapinga wanaosimamia sheria kwa kufuata masuala ya kisiasa, nadhani labda kuna tatizo la mawasiliano au tunaendesha nchi bila sheria kwa kuogopa kupoteza kura wakati wa uchaguzi,” alisema Dk. Bana.

  Aliongeza kuwa waziri anapotoa tangazo la sheria kutekelezwa halafu mwingine anampinga au kutengua, inamaanisha wale waliokuwa wanapinga wana akili kuliko washauri wa serikali.

  Dk. Bana alisema alishangaa kumsikia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wassira akisema kuwa wapinzani wasitarajie kuitwa tena Ikulu kuzungumzia mchakato wa katiba mpya kama vile alishaongea na Rais Jakaya Kikwete.

  Alisema Wassira aliwafungia milango wapinzani, lakini Rais Kikwete amewaita keshokutwa azungumze nao, hivyo kumfanya waziri huyo aonekane alikurupuka kuzungumzia jambo hilo.

  “Waziri wa Katiba na Sheria naye alijitokeza kuongelea jambo hilo zito, mimi nikajua kuwa huenda wameshaongea na rais kumbe hawajaongea naye ila walikurupuka tu, hii ni hatari kwa uongozi,” alisema.

  Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema kupingana huko ni dalili ya ugonjwa unaosababishwa na kutokuwepo miiko ya uongozi iliyowekwa na Azimio la Arusha.

  “Wote wanaopingana labda wana nia nzuri ya kujenga taifa letu, lakini hakuna dira na mwelekeo, tumekuwa katika utawala wa familia ya kambale ambapo mjukuu na babu wote wana sharubu,” alisema.

  Mnadhimu wa Upinzani, Tundu Lissu (CHADEMA), alipohojiwa kuhusu serikali kupingana alisema maana yake ni kushindwa kazi.

  “Mimi nilitarajia waliotoa matamko yaliyopingwa na wakubwa zao hadharani walipaswa kujiuzulu kulinda heshima,” alisema.

  Aliongeza kuwa anamshangaa Rais Kikwete ambaye baada ya kugundua kuwa watendaji wake wana kasoro ameshindwa kuwafukuza na badala yake amebaki anapingana nao.

  CCM yawakingia kifua

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu viongozi hao kupingana, alisema haoni tatizo kwakuwa mfumo wa utawala bora una fursa hiyo.

  “Sioni tatizo kiongozi wa juu kumpinga kiongozi wa chini, muundo huo upo na unazingatia ngazi za kiutendaji kwa mkubwa kutengua mamlaka ya aliye chini yake, hata hivyo sheria ni lazima zitumikie wananchi sio wananchi kutumikia sheria,” alisema.

  Kauli za mawaziri zilizotenguliwa

  Machi 2011, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli alinukuliwa akisema: “Mheshimiwa rais, niliapa kulinda sheria na katiba ya nchi, hivyo ninaomba nipewe ruhusa kutekeleza sheria ya kubomoa nyumba zilizojengwa ndani ya hifadhi ya barabara, kwa madai kwamba waliojenga ndani ya barabara wamevunja sheria namba 13 ya mwaka 2007 na kwamba hawastahili kulipwa fidia.”

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa mbele ya wananchi wa Chato licha ya kumsifu Magufuli, alisema serikali imemuagiza asimamishe zoezi hilo hadi litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri.

  Rais Kikwete pia akiwa jijini Dar es Salaam alimzuia asiendelee na ubomoaji huo huku akimtaka pia aangalie ubinadamu katika bomoabomoa hiyo pamoja na historia ya eneo husika.

  Wiki chache zilizopita, Waziri Mkuu Pinda alitengua tangazo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki la kuligawa eneo la Pori Tengefu la Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro, kwa kutenga kilomita za mraba 1,500 kwa ajili ya uhifadhi na kilomita za mraba 2,500 kuwa chini ya serikali za vijiji.

  Machi 19, mwaka huu, Waziri Kagasheki alitoa tangazo la serikali la kuligawa pori hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 4,000 ili serikali iweze kuhifadhi eneo la kilomita za mraba 1,500 ambalo alieleza kuwa ni mapito na mazalia ya wanyamapori, pia kutunza ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Tangazo hilo liliibua mgogoro mkubwa.

  Hali hiyo haijaisha ambapo hata kwenye suala la mchakato wa mabadiliko ya katiba kumeonekana kupingana wazi wazi kati ya Rais Kikwete na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wassira, waliobeza kuhusu uwezekano wa rais kuonana na wapinzani kujadili suala la mchakato wa katiba.

  Wassira alisema: “Wanasiasa wa upinzani kususia na kutoka ndani ya Bunge kwa hoja ya kutowashirikisha wananchi wa Zanzibar, hili si kweli, kwa sababu Kamati ya Katiba na Sheria ilikwenda huko, sasa wasitake kulalamika na kutaka kukutana na Rais Kikwete.

  “Hawa tumewalea siku nyingi na sasa wanafanya mazoea, ninachotaka kuwaeleza wasitarajie tena kuitwa Ikulu, nchi hii inaongozwa na misingi na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.”

  Chikawe alisema endapo Rais Kikwete hatasaini muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013, kama wapinzani wanavyotaka atakuwa ameingia kwenye mgogoro na Bunge.

  Kuyumba yumba kwa serikali pia kumeonekana siku za hivi karibuni katika suala la kufunga na kufungulia magazeti ya Mwananchi na Rai.

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 17. House of Commons

  House of Commons JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2013
  Joined: Oct 1, 2013
  Messages: 1,689
  Likes Received: 415
  Trophy Points: 180
  Wakati ni ukuta, ukipambana nao utaumia...no longer at ease...misemo hii inaihusu ccm &co..
   
Loading...