CCM Tuwe Macho na Mbinu Mpya ya CHADEMA

CCM Tuwe Macho na Mbinu Mpya ya CHADEMA

zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Posts
17,240
Reaction score
3,935
Nakumbuka nilivyokuwa kwenye mchezo wa soka, tuliwahi kutumia mbinu ya kisaikolojia inayofanana sana na mbinu wanayoitumia chadema hivi sasa. Iwe ni kwa umoja wao au kwa baadhi yao wenye kuijuwa hiyo siri.

Mbinu yenyewe ni sahali sana kuitekeleza lakini inadanganya sana washindani wenu na kuwafanya wabweteke na wawe "over confident". Tukumbuke kuwa kwenye mashindano yoyote hakuna kitu kibaya kama kuwa na "over confidence" inayokufanya umdharau mshindani wako, na huko ndiko wanakotupeleka chadema.

Chadema mpaka sasa wameshatuaminisha wengi wetu kuwa wameshasambaratika, wana ugomvi usio na ufumbuzi na wanafanya kila hila na kutuhakikishia kuwa kwenye kambi yao hakuna maelewano, wana fanya kila hila kutuhakikishia kuwa kwao kuna kambi tofauti na kuna mpasuko usio tibika.

Kinachofanywa sasa hivi na chadema ni hiyo mbinu, kuwafanya CCM wabweteke na kuona kuwa chadema imesambaratika na hakuna maelewano lakini ukweli ni kwamba, ndani ya chadema hakuna mpasuko, wala hakuna ugomvi, wala hakuna kutokuelewana sijui Kitila na uongozi wala hakuna kutokuelewana sijui Zitto Kabwe na uongozi, ni mbinu yao ya lala salama waliokuja nayo na hii mbinu ni safi sana na mara nyingi kama haikugundulika mapema huwa ni ya ushindi tu. CCM tunadhani wenzetu wanagombana kumbe wao wako kwenye harakati za kampeni.

Hivi kwa mtu mwenye kufikiri inakuingia akilini, kupinga hoja za kukufukuza wadhifa kwenye chama ukaitangaze katika moja ya hoteli kubwa nchini? Hivi umfukuze uongozi Naibu Katibu Mkuu halafu Katibu Mkuu uende jimboni kwake ukawaambie "ndio tmemfukuza" fanyeni mnachotaka?

Hivi inawaingia akilini kuwa habari nzito kama hizi za kusambaratika uongozi wa chama zitangazwe na walalahoi wa chadema kina Makene badala ya kutangazwa na akina Mbowe na Slaa? Na ukitazama kwa umakini utaona kuwa Mbowe na Slaa wako kimya kwenye suala nyeti kama hili. Umejiuliza kwanini?

Kilichonistuwa ni pale nilipoona kuwa Zitto Kabwe huko kwao Kigoma anajitangaza kama chadema lakini wananchi wanatangaziwa kuwa wasibebe bendera ya chadema, hii ni mbinu ya kuwapata na kuwavuta wale mashaabiki wote wa vyama vingine vyote na kudhani kuwa wanamhurumia kijana wa kwao. kumbe ni hila tu za chadema na imefanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Ukitazama kwa undani utakuta kuanzia tuhuma, mpaka kuvuana uongozi, mpaka mikutano, ziara zinazoendelea sasa kila upande. Utagunduwa kuwa chadema wamejipanga na wameanza kampeni kwa gea ya kuwa wana ugomvi na hawaelewani.

Wana CCM na viongozi wa CCM inabidi tujipange na tusifanye dharau hata kidogo, chadema hawana ugomvi wala hawana mpasuko ndani ya chama chao, wanatufanyia mchezo wa kuigiza na wanatuingiza kwenye mkenge huku tunajiona.

Ndugu zangu wana CCM, napenda muelewe kuwa mpaka sasa, chadema wametutupia chambo na tumesha kimeza, tusipokuwa makini tutameza vyote, chambo, ndoano, mshipi na chubwi.

Viongozi na wana CCM wote, naomba msichukulie huu kama ni mzaha, majuto huwa ni mjukuu.

CCM Daima.
 
mimi chadema nakiona kama chama ambacho hakina mwelekeo hata kidogo kazi yake ni kulaghai watu kupitia jukwaa la siasa lakini wao wanafanya mengine kabisa.
 
mimi chadema nakiona kama chama ambacho hakina mwelekeo hata kidogo kazi yake ni kulaghai watu kupitia jukwaa la siasa lakini wao wanafanya mengine kabisa.

Hivyo ndivyo wanavyotaka ieleweke na CCM ibweteke. Lakini ukweli ni kuwa wamejipanga kisawasawa na haitakiwi kuwadharau hata kidogo.
 
mimi chadema nakiona kama chama ambacho hakina mwelekeo hata kidogo kazi yake ni kulaghai watu kupitia jukwaa la siasa lakini wao wanafanya mengine kabisa.

Hapo ndipo ubongo wako ulipofikia kuelewa, nakupa pole sana
 
Kama great thinker ni vizuri kutafakari, sasa hivi chadema inatajwa zaidi popote kuliko ccm, hii inaifanya chadema kujulikana zaidi ya vyama vingine! Ingawa binafsi siamini kama sakata hili linaleta umoja na utengamano zaidi ndani ya chadema!
 
Gud analysis.. na kuna kaukweli flani.. tujiulize, siku 14 zimeisha lakini kiimyaaa!!

Na kwanini haya yote yametokea kipindi karibu na uchaguzi mkuu, na ule wa serikali za mitaa.. Jibu ni rahisi, Zito aonekane amesamehewa arudi kwa kishindo azunguke nchi nzima kutangaza CDM.. Hivyo kila mtu ataielewa chadema.. Na itashinda kirahisi kila chaguzi. Zito atawambia tu wafuasi wake kwamba ugomvi umeisha chamani, tupge kazi, tuwaunge mkono viongozi wetu.

Hii ni very advanced technic inayotumiwa na chadema..
Wait and u'll see!
 
Gud analysis.. na kuna kaukweli flani.. tujiulize, siku 14 zimeisha lakini kiimyaaa!!

Na kwanini haya yote yametokea kipindi karibu na uchaguzi mkuu, na ule wa serikali za mitaa.. Jibu ni rahisi, Zito aonekane amesamehewa arudi kwa kishindo azunguke nchi nzima kutangaza CDM.. Hivyo kila mtu ataielewa chadema.. Na itashinda kirahisi kila chaguzi. Zito atawambia tu wafuasi wake kwamba ugomvi umeisha chamani, tupge kazi, tuwaunge mkono viongozi wetu.

Hii ni very advanced technic inayotumiwa na chadema..
Wait and u'll see!
WE CDM ARE NOW AT THIS POINT
13564622-puzzled-confused-lost-signpost-shows-puzzling-problem.jpg
 
CHADEMA tunao mpasuko bwana, mbona mnaanza hizo? Wewe Zitto anafuata kila alipopita Katibu Mkuu wake, halafu unasema hakuna ugomvi hapo?
 
Huo ndio ukweli. CCM wanawasomba na kuwagharamia kila kitu kwenda kumpokea ZITTO. Unadhani baada ya mkutano hao wote watakuwa CCM au CDM baada ya kuhubiriwa UCDM?
 
hahahahahaha siasa za bongo ndizo zinazo changia umaskini kwa kiasi kikubwa......
 
Mh!! Inawezekana ikawa mdharau mwiba... Haya hakuna kisichowezekana chini ya jua!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
yote heri tu! ila tunataka ukombozi wa kweli wanafiki na wasaliti wote wafungiwe jiwe shingoni na watoswe kwenye kima cha maji kirefu
 
Back
Top Bottom