CCM tupo katika mwanguko mkubwa

Wewe bungeni wewe,we ni Mtz kweli? Naanza kuamini sasa kuwa kuna watu huwa wanalipwa kwa kupost ishu za kushabikia CCM,ndio maana mnakaa na kupanga sh.bilion 1 kwa ajili ya mazish ya viongozi,tuweni wazalendo tuache ushabik wa vyama jamani!
 

Naamini kulikuwa na mgongano wa lugha, ndughai alisisitiza mh lisu atoke nje hakufafanua kawa atoke nje aende wapi? Si abaki ndan?
kumwambia mtu toka nje manake nini kama si haingie au habaki ndani?
Elimu za maghamba ata kiswahili hakipandi tabu kweli kweli
 
UTASHI BINAFSI WA NDUGAI KUJIPANDISHA GHADHABU KUMFUKUZA MJUMBE BUNGENI NI UKIUKWAJI WA HAKI NA WAJIBU WA SPIKA KUSIMAMIA CHOMBO HIKI CHA UMMA

Kama kweli Mhe Tundu Lisu aliamriwa na 'Kiti Cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania' KUTOKA NJE kwa kuwekewa wazi kosa lake na kusomewa KIFUNGO fulani kinachotamka mbunge kufanya hivo kwa mujibu wa kifungu kinachojulikana wazi na bila ya kuwepo hata chembe cha ushawishi wa tofauti za kiitikadi hapo kidogo tungeelewa.

Lakini kitendo tu cha Mwana-CCM mmoja kwa jina la Job Ndugai kuhisi kwamba kikao cha bunge kimechukua muda mrefu sana kwisha hivyo akajiamulia tu kwa utashi wake tu mwenyewe na kuanza kukoromea mjumbe eti atoke nje bila hata ya kutamkiwa kosa wala kifungu cha kanuni za bunge zinazounga mkono uamuzi kama huo kamwe haikubaliki na wala bunge lisiendeshwe kwa misingi hii hata siku moja kwani kanuni zina kazi zake maalumu mle.
 
umenena hoja nzito..watu wanakushambulia?....tuitizame tanzania jamani ccm haitokupeleka popote pale...sante mchambuzi.
 

mkuu umemaliza yote sioni cha kujadili kwa sababu ccm wenyewe wanajua anguko lipo 2015 too late acha wafu wazikane hakuna marefu yasiyo na ncha ni mwisho wao ndo maana hawana cha kuchangia au kuwambia wananchi zaidi ya matusi makubwa bungeni alafu kiti cha spika kinafunika na wapinzani wanatolewa nje wao wajiona wajanja
kumbe ndo wanajimaliza wenyewe bila kujijua.da acha chama kife aje dk atuongoze sio kutawaliwa na ccm tena
 
Ushauli wameanza kupewa na mwl.Nyerere lakini responce ilikuwa zero.Hivyo kwa wewe hata ungewaimbia mashairi gani wasingekuelewa.Waache wakafie mbali.
 
Nilipofikia hapo, ndipo nikaamua kujiunga rasmi na CHADEMA! Nichukue nafasi hii kukukaribisha CDM kwa mikono miwili! Hamna dawa ya kuponya ccm! Ukiendelea kukaa huko utakufa kwa uchungu!
 
Leo wote humu jukwaani mtavaa kijani bila kupenda..kinana anazidi kuwacharaza mboko za mgongo huko morogoro..

Unajua linalozungumzwa katika thread hii lina asilimia nyingi za ukweli ndani yake. Mchangiaji anayeingiza mada ya KINANA AZIDI KUWACHARAZA MBOKO ZA MGONGO HUKO MOROGORO , kwa mtu mwenye kufikiria vizuri utagundua ni mmoja kati ya waliotajwa katika thread hii, kwani hatofautiani kabisa na mawazo ya mchangiaji aliyesema "sikio la kufa.........." Hakupaswa kuingiza jambo jipya la kina kinana badala ya kutafakari thread ile kwa undani na aondoe machungu kama imemtouch.
 
Umewasilisha ujumbe mzuri kwa chama cha zamani endapo watauzingatia maana anguko hili hata Mzee Mzindakaya ameliona japokuwa wenyewe wanajifanya hawaoni.
 
Dah kweli kabisa....atakaekupinga hana mapenzi mema na Chama cha Mapinduzi
 
hali sio nzuri chama kipo icu na nasikia wameshaanza kuchanganya dawa ya kumdunga akiwa mochuari lakini cha ajabu dawa yenyewe imegoma kuchanganyika. Rip chama changu ccm.:a s cry::a s cry::a s cry:

vp babuu rogger,hawa kuku chakachua kwenye mabaraza ya katiba ndugu,
 
Hali sio nzuri chama kipo ICU na nasikia wameshaanza kuchanganya dawa ya kumdunga akiwa mochuari lakini cha ajabu dawa yenyewe imegoma kuchanganyika. RIP chama changu CCM.:A S cry::A S cry::A S cry:

Huku mwenyekiti akiwa bize kuhudhuria mazishi ya wasanii!
 
wewe bungeni wewe,we ni mtz kweli? Naanza kuamini sasa kuwa kuna watu huwa wanalipwa kwa kupost ishu za kushabikia ccm,ndio maana mnakaa na kupanga sh.bilion 1 kwa ajili ya mazish ya viongozi,tuweni wazalendo tuache ushabik wa vyama jamani!

usipate sida mkuu,mtu yoyote leo ukimwona anashabikia ccm,ujue ni njaatu zinamsumbua alafu unazani wanapewa nini,2,000 na kuvalishwa kofia na tisheti,mtu mwanzo wa hasubui mpaka jioni utamkuta ofc za chama,na kushabikia ujinga wa ccm,huku ni kukosa akili na kufa kifikra,tunatakiwa kwanza tuwa fufue hawa watu wanamna hii,nape,akija wanakimbia mpaka wana anguka chini yaani wamelogwa kweli na chama cha wapiga dili,
 
Mkuu hapa unaipigia tarumbeta MAITI, sidhani kama utasikika. Tunawaacha wafu muwazike wafu wenzenu...
 
hali halisi ya maisha wanayo ish wanayo ishi watanzania...na upuuzi wa wabunge waccm hasa mwigulu..ndio vinafanya ccm ife
 
Napenda mawazo chanya kama haya. Ya kukubaliana na hali halisi
 
Haijalishi nani kaandika, awe ni magamba au magwandwa hiyo ndio hali halisi na kwa kweli ametoa changamoto kwa wahusika. Chukueni mkazifanyie kazi badala ya kuendesha ubabe. Ebu someni Mwongozo wa CCM wa 1981 Ibara 59. mnaoropoka tu eti mnategemea Nape, Mwigulu, Kigwangala, lusinde, Mkamia na Serukamba kukijengea hoja chama. Hao ni zero kabisa tena ndio wanaharakisha ANGUKO KUBWA LA CCM.
 


Haihitaji akili ya ziada kutambua kuwa wewe ni Mwanachama wa Chama cha KIGAIDI(cdm).
Hatuhitaji Mafumbo, jiweke wazi tu kuwa umetumwa au umejituma?
Kwakuwa Chama chako kimekosa mvuto sasa umeanza kuigiza Chama kubwa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…