Nimefanya utafiti kwa mikoa sita haraka haraka kwa kusafiri mwenyewe na mikoa mingine 15 kwa kufanya mawasiliano ya simu. Jumla nimejitahidi kuwafikia na kuwasiliana na wadau takribani katika wilaya 57 ya mikoa hiyo na kugundua jambo moja baya sana kwa CCM.
Uwezekano mkubwa asilimia zaidi ya 75 ya wabunge na madiwani wa CCM watarudi hao hao. Madiwani wengi wa CCM ni wazee wa zaidi ya miaka 55 na wengi ni wastaafu. Wote hawa wamechukua fomu na hakuna dalili vijana waliochukua fomu watafanikiwa kurudi kwani mazingira ni magumu sana.
Kwa CCM vijana wenye umri chini ya miaka 35 CCM waliochukua fomu wengi watashindwa kupenya kwa sababu madiwani wengi wameamua kutumia fedha walizopewa kama pensheni ya udiwani wameshatoa kwa wajumbe.
Katika mikoa niliyofikia ni mikoa ya Mbeya na Arusha tu ndiyo ambayo waliochukua fomu wapya kwa wageni wanaonekana kuwa na nguvu sawa kihoja na kiuchumi. Mikoa ambayo wanaoweza kurudi wabunge na madiwani asilimia 80 ni Shinyanga, Tanga, Tabora, Mtwara, Singida na Pwani.
Jambo hili ni baya kwani linaashiria kuwa CCM imeshajitengenezea kakundi fulani ambako kanataka kenyewe tu ndiyo kaongoze nchi. Bila viongozi wa CCM kuliona hili hivi punde kutakuwa na tabaka kubwa sana la CCM likakalolichukia kundi hili na hivo going forward kundi hili litakuja kukataliwa kwa aibu kubwa sana.
Mbaya zaidi kikundi hicho kinawaandaa watoto wao kuja kushika nafasi zao, kitu ambacho ni kibaya sana.