Uchaguzi 2020 CCM tumezidiwa sana na tunaweza tusimalize vizuri. Huyu mtu kasi yake ya ajabu

Mitandao inawadanganya sana na mnaamini. Ukiingia Jamii Forums ukakuta threads za kumpa moyo Lissu unaona kama kashakuwa Rais na CCM imechemka.

Lissu hawezi kuja kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sio 2020 bali ni kamwe (NEVER). CCM sio wajinga wapo jikoni wanaset mitambo wakati nyie mmekazana na Mambo yasiyo na impact mpo bize kushangilia helicopter aliyokodi Lissu. Kwa akili hizi za kujipa moyo CCM itaondoka madarakani miaka 50 ijayo.
Mzee we unakwama wapi maana walipo JF ndo waliko mtaani na ni wapiga kura
 
Wanaccm woòoteeee
Someni Waraka wa Mtume Paulo kwa Wakolosai
Sura ya tatu , aya ya 25

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee we unakwama wapi maana walipo JF ndo waliko mtaani na ni wapiga kura
Uliwahi kuona post yoyote jamii forums ina likes milioni 1 ?!?... Ndo ujue wafuasi wa mitandaoni ni % ndogo sana. Halafu hata mkoa uliopo wote wampigie kura Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. NEVER.
 
Mitandao inawadanganya sana na mnaamini. Ukiingia Jamii Forums ukakuta threads za kumpa moyo Lissu unaona kama kashakuwa Rais na CCM imechemka.

Lissu hawezi kuja kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sio 2020 bali ni kamwe (NEVER). CCM sio wajinga wapo jikoni wanaset mitambo wakati nyie mmekazana na Mambo yasiyo na impact mpo bize kushangilia helicopter aliyokodi Lissu. Kwa akili hizi za kujipa moyo CCM itaondoka madarakani miaka 50 ijayo.
Law of the Universe haipo hivi, kuna mwisho wa kila kitu chini ya jua.
Kuhusu mitandao, kwa mujibu wa TCRA kuna watumiaji takribani 23 milioni hadi kufikia mwezi May 2020. Kwa sasa eneo la mitandao lina nguvu kubwa sana katika kutoa mwelekeo wa masuala mengi kwa jamii, taarifa ni silaha kubwa.

CCM haiwezi toka madarakani kwa usiku au asubuhi moja, ni suala la mchakato wa muda wenye hatua mbalimbali. Naweza kusema kwa sasa mchakato huo upo hatua nzuri, tunaona ukosoaji unaongezeka, makundi yenye ku-reason yanaongezeka, mawazo ya watu wengi yanapuuzwa, CCM inagawana mbao kadri muda unavyozidi kwenda. Niseme tu ni suala la muda, kama siyo CHADEMA basi umma utaitoa CCM madarakani au CCM itajitoa yenyewe kwa kugawana mbao kama KANU.

Haya ya helicopter ni mambo ya kawaida watu kufurahi na kushabikia kwenye kampeni wala siyo sababu ya chama kusahau kampeni. Kwa sasa swali muhimu kwa CCM ni Je KWA NINI UPINZANI UNAUNGWA MKONO KIASI HIKI?
 
Chadema pamoja na kubebwa jamii forum lkn hamna uwezo wa kumpigania mgombea wenu

Nyuzi za Ccm zinapigwa pin lkn Chadema ndio mpo hoi
 
Mitandao inawadanganya sana na mnaamini. Ukiingia Jamii Forums ukakuta threads za kumpa moyo Lissu unaona kama kashakuwa Rais na CCM imechemka.

Lissu hawezi kuja kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sio 2020 bali ni kamwe (NEVER). CCM sio wajinga wapo jikoni wanaset mitambo wakati nyie mmekazana na Mambo yasiyo na impact mpo bize kushangilia helicopter aliyokodi Lissu. Kwa akili hizi za kujipa moyo CCM itaondoka madarakani miaka 50 ijayo.
Mnategemea NEC wawafaulishe ila ccm imekufa wamebaki wale wenye maslahi binafsi.
 
Ndugu zangu wanaCCM mlioko humu ndani na kwingineko, hali ni ngumu sana huyu mtu anatuzidi kwa kiasi kikubwa sana kwa ninavyotazama mimi na msema kweli mpenzi wa Mungu.

Huyu ni ambaye ni sawa na Faru aliyejeruhiwa yupo Energetic, anaongea mambo magumu yanayogusa ndani, anaijua sheria sana anajiamini. Naomba sana kuelekea mwishoni tujitathmini.

Tusijipe moyo kwakuwa sisi ni Chama dola kwa maana kwamba tuna uwezo wa kufanya lolote tusalie madarakani, tufahamu kwamba huyu bwana katika hotuba zake kuna zaidi ya dakika 30 za kuelimisha umma namna ya kuzijua haki zao wakati wa uchaguzi. Hawa watu wanaojitokeza kumwangalia ni wengi na Ikumbukwe kwamba uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa watu walijitokeza kujiandikisha tena wengine wanalazimishwa na MaDC mwaka jana na wengi tunakumbuka vizuri. Kwahiyo waliojiandikisha ni wengi sana na serikali ilihamasisha hilo mwaka jana.

Tusijivunie wanachama wetu zaidi ya milioni 11 tulionao, wengi ni majeruhi wa kura za maoni wako nasi kwenye nyuso tu lakini moyoni hawapo na tunawaona. Huu umati ukimpiga kura nyingi huyu bwana hatutaweza kulazimisha kumzuia tutaumiza watu. Kama kuna makosa ya kimkakati naona tunataka kuchelewa Muda unayoyoma chama ndio halitajwi sana siyo mitandaoni wala mitaani zaidi utamsikia Tundu Lissu tu. Ukisikia CCM kinatajwa labda siku hiyo kuna kampeni mahali flani.

Mara nyingi CCM tumekua wagumu hatushauriani na tunajiona tunajua sana hasa katibu wetu wa Itikadi na wenezi , tunaenda kuumia na mimi naenda kukata tamaa walai.

Shida ya Chama chetu ni wengine kujiona ndio wenye chama zaidi na kuwapuuza wengine. Badala ya kujibu hoja zinazotolewa na wapinzani wetu tumekuwa tukitumia vyombo vya dola, hususan jeshi la polisi, kuzikandamiza hoja hizo. Hilo halifai na kauli za kubeza sio silaha muafaka kwa wakati huu kwani watu wanweza kupambanua na kuona hatuna hoja.

Nashauri Sekretariet chini ya Komredi Bashiru ilipange sawa kwa kipindi kilichobaki kisichozidi saa 150 kufikia siku ya uchaguzi, kuja na mikakati thabiti ya kupenya mioyo ya wapiga kura badala ya kubweteka na kudhani tunapendwa "automatic".

Komredi Polepole aachane na vijembe vya waimba-taarabu. Havitusaidii sana tunapokumbana na watoa hoja makini wa upande wa pili kwenye vijiwe huku mtaani (site) waliko wapiga kura halisi.

Ma-DC kama Ole Sabaya wanafanya harufu ya chama chetu kuwa mbaya puani mwa jamii na kuonekana kina elements na ujasusi wa kipuuzi. Huyo akemewe mara moja na asiendeleze ujinga huo wa uhuni wa magenge ya kialifu. Ushindi wa damu sio ushindi.
 
Ndugu zangu wanaCCM mlioko humu ndani na kwingineko, hali ni ngumu sana huyu mtu anatuzidi kwa kiasi kikubwa sana kwa ninavyotazama mimi na msema kweli mpenzi wa Mungu.

Huyu ni ambaye ni sawa na Faru aliyejeruhiwa yupo Energetic, anaongea mambo magumu yanayogusa ndani, anaijua sheria sana anajiamini. Naomba sana kuelekea mwishoni tujitathmini.

Tusijipe moyo kwakuwa sisi ni Chama dola kwa maana kwamba tuna uwezo wa kufanya lolote tusalie madarakani, tufahamu kwamba huyu bwana katika hotuba zake kuna zaidi ya dakika 30 za kuelimisha umma namna ya kuzijua haki zao wakati wa uchaguzi. Hawa watu wanaojitokeza kumwangalia ni wengi na Ikumbukwe kwamba uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa watu walijitokeza kujiandikisha tena wengine wanalazimishwa na MaDC mwaka jana na wengi tunakumbuka vizuri. Kwahiyo waliojiandikisha ni wengi sana na serikali ilihamasisha hilo mwaka jana.

Tusijivunie wanachama wetu zaidi ya milioni 11 tulionao, wengi ni majeruhi wa kura za maoni wako nasi kwenye nyuso tu lakini moyoni hawapo na tunawaona. Huu umati ukimpiga kura nyingi huyu bwana hatutaweza kulazimisha kumzuia tutaumiza watu. Kama kuna makosa ya kimkakati naona tunataka kuchelewa Muda unayoyoma chama ndio halitajwi sana siyo mitandaoni wala mitaani zaidi utamsikia Tundu Lissu tu. Ukisikia CCM kinatajwa labda siku hiyo kuna kampeni mahali flani.

Mara nyingi CCM tumekua wagumu hatushauriani na tunajiona tunajua sana hasa katibu wetu wa Itikadi na wenezi , tunaenda kuumia na mimi naenda kukata tamaa walai.
Mwana UHONGO
 
Huyu sasa ndo Polepole mwenyewe sasa, utopolo huu sijui umeutoa wapi unasema watu wanaenda kushangaa helicopter kana kwamba Lissu kaanza zamani sana kutumia huo usafiri kumbe ni jana tu. Lakini kiwewe kimekushika hadi unafikiri kwa tumbo badala ya kichwa...
Ukweli unauma
 
Back
Top Bottom