CCM toeni kwanza boriti kwenye jicho lenu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM toeni kwanza boriti kwenye jicho lenu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndibalema, Sep 8, 2010.

 1. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi karibuni CCM wameanzisha kampeni 'chafu' kwa kuingilia maisha binafsi ya ndoa ya mgombea urais wa CHADEMA, Dr. Slaa.
  Hivi kama kigezo ni hiko huyu JK alistahili hata kuwa waziri?
  CCM Ondoeni kwanza Boriti jichoni kwa mgombea wenu kabla ya kutolea mimacho kibanzi kwenye jicho la mgombea wa wapinzani wenu.
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nina hakika Chadema wangeanza siasa za maji machafu, siasa za vyumbani na vitandani mwa watu JK, Kinana, mropokaji Makamba, mwizi RA, na mhujumu uchumi EL hakuna angesalimika. Sema sasa muda hautoshi wa kufanya ujinga huo. Wao wanafanya kwasababu hawana lingine. Kwa sababu wamekosa dira. Au tuseme kwa sababu tangu mwanzo hawakuwa na dira. Wanavutwa na upepo.

  Ni bahati mbaya hata kwa familia zao kuwa na baba asiye na dira, kuwa na mume asiye na mikakati endelevu ya maendeleo ya familia, ambaye akiamka asubuhi hajui afanye nini isipokuwa kwenda kupata umbeya wa vyumbani mwa majirani na wajuani wake, kalala na nani? wapi? lini? Kisha huenda kupiga umbeya huo majukwaani na maofisi. Jaza mwenyewe kinachofuata kwa familia yake tu, sembuse taifa.

  Ni majambazi tu yanajengwa. Mwana wa nyoka ni nyoka, hatushangai na watoto wao watakuwa na mwelekeo huo huo.
   
Loading...