CCM Taifa badilikeni

CORONAZ

Senior Member
Joined
Apr 26, 2020
Posts
179
Reaction score
346
CCM ni tasisi na kila tasisi ina mfumo wa ukuaji wa wafanyakazi wake kivyeo. Ila CCM kuna maeneo inafikirisha.

Nimefuatilia kwa muda teuzi za nafasi mbalimbali ndani ya CCM haswa ya Katibu Mkuu Kitaifa, kwa kawaida ya taasisi ungetegemea Katibu Mkuu Kitaifa apatikane miongoni mwa Makatibu bora wa Mkoa au Sekretariati za Makao Makuu.

Hivi tuseme kweli, katika Makatibu wote na Wakuu wa Idara za Makao Makuu hakuna mwenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya Katibu Mkuu?

Maana ukiangalia Makatibu Wakuu 3 wa mwisho nyadhifa zao kabla ya uteuzi unabaki na maswali sana, au Mwenyekiti za wasaidizi wake wanaweka hawa jamaa kwa maslahi fulani huku wakijua kuna uwezekano wa kupwaya?

Haya CCM nafasi nyingine tena, hebu tuone atakayechukua mikoba, wa ndani au nje?
 
CCM ni taasisi kubwa iliyopitwa na wakati, na inategemea udhaifu wa katiba iliyopo kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti. Kizazi kimebadilika yenyewe imebakia kutegemea vyombo vya Dola kukaa madarakani.
 
Tamaa si kitu kizuri.
Ridhika kwa ulichoaminiwa , kukodoa mimacho kewenye nafasi nyingine ni tamaa na uroho wa vyeo.

CCM ina watu wengi mno tena wa kutosha sana, wengine wapo ndani ya uongozi wa ccm ngazi mbalimbali, lakini pia wapo watu wengi sana wenye sifa za ukatibu mkuu ccm Taifa miongoni mwa wanachama wa ccm nchi nzima.

so,
Yeyote anaweza kuteuliwa kushika nafasi hiyo miongoni mwa makundi hayo mawili.
Hakuna haja ya kumpigia chapuo fulani kwasababu yawezekana ni kweli anaweza kua na sifa lakini pia wapo wengine pia wenye sifa kama hizo...
 
Tlaatlaah, ina maana una ndoto za kupewa cheo ndani ya chama? CCM ilipofikia inabaki madarakani kwa nguvu ya vyombo vya dola (bunduki), na ndiyo sababu mnazimia mkisikia neno katiba mpya! Nje na hapo kwenya sanduku la kura ni chama kilichojifia siku nyingi. Kila chawa wa CCM yuko ndani ya chama kwa nia ya cheo au favour fulani, na viongozi wenu wanalijuwa hilo ndiyo maana wanatumia njaa zenu kama mtaji.
 
Usiwaamshe.Waache wajifie.
 
Kwa nini nafasi ya Katibu mkuu haitokani na ushindani na uchaguzi wa wajumbe?
 
Katibu mkuu anagepatikana kwa njia ya kura za wajumbe.
 
Tumeshindwa kuwa na mfumo mzuri wa kuandaa viongozi wa kitaifa,ndo tutakuwa na mfumo wa kuandaa viongozi kwenye chama(vyama),hii nchi inahitaji ukombozi wa kifikra.
 
ndrotroooo πŸ˜€
nilipo na nilivyo hivi naishi katika ndoto yangu, hiyo nyingine si muhimu japo inafaa kua ziada..

kuhusu katiba mpya,
hilo liko wazi tukimaliza uchaguzi 2025, mchakato katiba mpya unaanza upya 2026mara moja na hautasimama kwa sababu yeyote mpaka utakapokamilika.

lengo ni uchaguz wa 2030 ukute tayari tuna uzoefu kidogo na matumizi ya hiyo katiba mpya.

hizo nyingine sijua rasimu ya nani na sijui alikua nani bakini nayo for refference ngoma inaanza upya....

Hivyo visingizio vyenu, sijui kuibiwa kura, sijui kusaidiwa na dola n.k bakini nayo kwenye kumbukumbu zenu.

CCM iko siriaz mno na masuala siriazi yanayohusu nia , malengo na madhumuni ya kushika dola.

Lia kwa sauti zote, lalama utakavyo, tukana, kejeli, beza, zodoa but kwenye uchaguzi na kura, CCM haitamuonea haya wala huruma chama au mtu yeyote mshindani,

CCM itapiga kampeni ya nguvu nyumba kwa nyumba kama kawaida, tutagalagala kwa vumbi mbele ya wananchi, tutawapigia magoti wananchi kama tumechanganyikia ili tusimbakizie mshindani wetu kakura hata kamoja...

CCM itasomba wananchi kwa malori na matrekta,bodaboda, mikokoteni na bajaji kwa mamilioni yao tuwakusanye pamoja tuwaelezee uzuri wa ilani ya ccm kwenye maisha yao, umuhimu na uzuri wa sera za ccm, umahiri, umakini na umadhubuti wa viongozi ccm, na kuwafundisha kuepuka kitapeliwa na vibaraka na wasaka tongeπŸ˜€

hakuna mzaha wala huruma katka suala la uchaguzi na kura hata kidogo.
Ni kuchukua kuweka waaa.....

Dhumuni la ccm ni kushinda uchaguzi, kushika dola, kuunda serikali na kuwatumikia wananchi....
 
CCM ina wenyewe.
Wanajuana
Wanachaguana
Wanateuana
Wanaiba pamoja
 
Tunga ngonjera, andika mashairi, imba mapambio lakini haibadili hali halisi kwamba CCM tuliyonayo leo kimekuwa chama chakavu baada ya kuvamiwa na watu wenye tamaa ya vyeo na utajiri wa wizi. Ni chama kilichojaa watu wenye hila, majungu, majivuno, makatili, fitina, majungu, mafisadi walafi wasiotosheka na hakipo tena kwa mnufaa ya ustawi wa taifa na wananchi wake. Kwasasa chama kina viongozi walio wengi na watendaji wenye giriba, waongo, wavivu, wababaishaji, wanafiki, wasanii nk. Niambie bunge ni CCM watupu, kuna la maana la kujivunia?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…